Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Kwanza kuna kila dalili, hujasoma!!

Nilichofanya mimi ni kupangua hoja za wanaopinga mradi!

Kwa mfano, Kakoko amesema Wachina wanataka wasemehewe kodi kwa miaka 30! Nimehoji, ni kodi ipi kwa sababu pale bandarini kuna kodi za aina nyingi!!

Aidha, kote duniani zipo kodi unazoweza kusamehewa, na zipo kodi ambazo katu huwezi kusamehewa kwa sababu ni mali ya serikali!!

Sasa huwezi tu kusema wanataka msamaha wa kodi bila kutaja ni kodi zipi!

Sasa kujadili hoja kama hiyo nako kunahitaji kuona mkataba?!

Na katika hilo nimesema wazi, based on case studies za Bandari ya Piraeus, Greece na Hambantota, nimesema wazi kwamba ni kweli Wachina huwa wanataka msamaha wa Income Tax!

Hata hivyo, haiwezekani, mathalani wewe uagize magari na yakapitia Bagamoyo halafu VAT on imported cars ichukuliwe na Wachina... hakuna kitu kama hicho!!!

Sasa hilo nalo linahitaji kusoma mkataba hilo?

Na hata kwenye VAT nimesema wazi Wachina wanaweza kuomba msamaha kwenye imported capital goods zitakazotumika kwenye ujenzi... sasa hilo nalo linahitaji kuona mkataba hilo wakati lipo kwenye sheria ya kodi ya mwaka 2017, 2018, na 2019?!
Kakoko kasema kwa kuwa kaona mkataba maana yeye yuko selikalini na ndio ilikuwa sehemu ya majukumu yake hayo...

Wewe unapinga kwa kusema Kakoko ni muongo,.. Na umesapoti hoja yako kwamba Kakoko ni muongo kwa kuwa umefanya sijui utafiti wapi na wapi!

Tukakuuliza umeuona mkataba wenyewe mpaka unasema Kakoko na selilakali ni waongo? Huna jibu!

Ndio maana tunasema hii mada yako imeegemea upande mmoja wa wachina hivyo haina maana.
 
Na ndio hicho wanataka watu mkuu! MKATABA basii..
Wewe huna hoja, na ni kawaida yako kutojadili hoja!!! Nimekuuliza, unahitaji kuona mkataba kufahamu Sheria ya Kodi inatoa mwanya wa msamaha wa kodi on imported capital goods?!

Unahitaji kuona mkataba kufahamu bandarini kuna aina nyingi za kodi, and always, kodi on imported goods ni mali ya serikali?!

Unahitaji kuona mkataba kufahamu sheria ya ardhi inatoa mwanya kwa mwekezaji kupata hatimiliki ya miaka 33 (renewable), au miaka 66 (renewable), au miaka 99?!

Unahitaji mkataba kufahamu kwamba mradi utatoa ajira za kutosha?!

Narudia, huna hoja na ndo maana unajificha kwenye mkataba!!!

Na unachosema ni kwamba, hata Wabunge wasijadili suala la bandari kwa sababu hata wao, katu hawataweza kuona huo mkataba!!!
 
Upende usipende bandari lazima itajengwa tu: Haya unayoleta wewe ni kelele za mbwa asiye na meno.
Hivyo nimeamua kukupuuza kwasababu nimepima na kuona uko na uelewa finyu mno....
Itajengwa lakini mashariti ya kinyonyaji hayatakuwepo.
 
Kakoko kasema kwa kuwa kaona mkataba maana yeye yuko selikalini na ndio ilikuwa sehemu ya majukumu yake hayo...

Wewe unapinga kwa kusema Kakoko ni muongo,.. Na umesapoti hoja yako kwamba Kakoko ni muongo kwa kuwa umefanya sijui utafiti wapi na wapi!

Tukakuuliza umeuona mkataba wenyewe mpaka unasema Kakoko na selilakali ni waongo? Huna jibu!

Ndio maana tunasema hii mada yako imeegemea upande mmoja wa wachina hivyo haina maana.
Kafanya utafiti wapi huyu bwege, anajifagilia ili aonekane yupo juu.
 
Kakoko kasema kwa kuwa kaona mkataba maana yeye yuko selikalini na ndio ilikuwa sehemu ya majukumu yake hayo...

Wewe unapinga kwa kusema Kakoko ni muongo,.. Na umesapoti hoja yako kwamba Kakoko ni muongo kwa kuwa umefanya sijui utafiti wapi na wapi!

Tukakuuliza umeuona mkataba wenyewe mpaka unasema Kakoko na selilakali ni waongo? Huna jibu!

Ndio maana tunasema hii mada yako imeegemea upande mmoja wa wachina hivyo haina maana.
Kasemaje?

Hata huyo Moosa Mao nae anao mkataba, sasa hoja yako hapo ni ipi?!

Btw, kwanini nimuamini mtu ambae tayari mamlaka ina mashaka nae, kiasi cha kufikia kumsimamisha kazi?
 
Kinacho tugarimu watanzania ni kule kutegemea Wanasiasa wasio na utaalamu wa kila jambo kutuamulia kila jambo.

Hii itatupelekea kuwa hapa hapa tulipo Kama sio kurudi nyuma hali wenzetu wanasonga mbele kwa kasi Sana.

Siasa zetu Tanzania zimekua za ovyo zinazoelemea ukabila ukanda ubinafsi na kila aina ya udhaifu wa kibinadamu badala ya maendeleo ya taifa kwa nyakati zijazo.

Kwa mfano wa serikali ya awamu iliopita ilifanya mambo yake kana kwamba yenyewe ndio ilikua ya Kwanza na ya mwisho, ilivunja vunja kila lililokua limepangwa na kupanga yake mapya na kwa bahati mbaya Sana awamu ile imemalika ikiwa na matokeo tofauti na matarajio.

Wakati ule wa mkapa tuliona mpango walioupanga wa dira ya maendeleo ya taifa kwa miaka 25 mbele .
Na kila serikali iliofuatia ilipaswa kua kutembea katika mpango ule, badala yake wenzetu Hawa wa awamu ya 5 wameenda ndivyo sivyo na gharama yake sio ya kidogo kuilipa Kama taifa.

Mradi wa bagamoyo unafaida Sana kwa taifa kwa vizazi vijavyo, serikali iliopo ikae tena ijadiliane kuliko na makosa kurekebishwe faida ipatikane, mwekezaji apate na taifa lipate, huo ndio zalendo!

Hii kusema sijui mtoto wa fulani alikamatwa kwa uhalifu na fidia ya adhabu ya uhalifu wake ndio bandar ya bagamoyo hizi ndizo fikra duni za kiubinafsi kiubaguzi ambao hazita tufikisha popote Kama taifa.
Wewe naweee...!
Hata kama huna, jifanye basi kama unazo jamani..! Sasa ulichojadili hapo ndio kitu gani sasa mkuu!

Umepooonda...! Cha maana ni
kuleta Mkataba hapa tuone ndipo itawapa credit ya nyinyi kuonekana mnazo nyingi kuliko mnawaponda!!

Mada nzuri kama Hizi za kimaendeleo, ni mhimu kuweka viambatanisho Vyote, hasahasa Mkataba na masharti yake!!

Sasa sijui moob Mao, kasemaji sjui, Kwa Dunia hii ya technologia kubwa, Kwani mbongo anashindwa kujipachika majukumu ya mchina na akatumia picha na Jina la kichina kufikisha anachotaka Kwa manufaa yake?

Mkataba, Mkataba, Mkataba ndio kila kitu
 
Una serious problem, hujijui tu! Na yote hii ni kwa sababu tu suala zima linamhusu JPM, nawe umeapa kumtetea kwa mabaya na mazuri!!

Narudia, suala la kutaka mkataba linathibitisha wazi huna hoja, kwa sababu hoja zangu hazihitaji kuona mkataba!

On top of that, nimekuuliza Kakoko aliyewaambia Mchina anataka asemehe kodi kwa miaka 30, amewaonesha mkataba?
Aghrrrrr!

Wewe bwana! Wote sio wajinga humu! Tunajua misimamo yako na wewe ni kumkosoa Magufuli basii.

Sasa ni hivi, kwa kuwa Kakoko hakuweka mkataba kusapoti hoja yake, na wewe pia hujaweka mkataba kusapoti hoja yako nyie wote ni wa kupuuzwa.
 
Pole sana!!!
 
Wewe huna hoja, na ni kawaida yako kutojadili hoja!!! Nimekuuliza, unahitaji kuona mkataba kufahamu Sheria ya Kodi inatoa mwanya wa msamaha wa kodi on imported capital goods?!

Unahitaji kuona mkataba kufahamu bandarini kuna aina nyingi za kodi, and always, kodi on imported goods ni mali ya serikali?!

Unahitaji kuona mkataba kufahamu sheria ya ardhi inatoa mwanya kwa mwekezaji kupata hatimiliki ya miaka 33 (renewable), au miaka 66 (renewable), au miaka 99?!

Unahitaji mkataba kufahamu kwamba mradi utatoa ajira za kutosha?!

Narudia, huna hoja na ndo maana unajificha kwenye mkataba!!!

Na unachosema ni kwamba, hata Wabunge wasijadili suala la bandari kwa sababu hata wao, katu hawataweza kuona huo mkataba!!!
Kwanini maneno mengi yote ya nini?

Hao wachina wamekupa kitu gani?

Ukiweka mkataba hapa hutapoteza muda kuandika maneno yote haya,
 
Wewe naweee...!
Hata kama huna, jifanye basi kama unazo jamani..! Sasa ulichojadili hapo ndio kitu gani sasa mkuu!

Umepooonda...! Cha maana ni
kuleta Mkataba hapa tuone ndipo itawapa credit ya nyinyi kuonekana mnazo nyingi kuliko mnawaponda!!
Basiii..

Na mada itakuwa imefungwa na wote tutaungana kutaka bandari ijengwe.
 
Kasemaje?

Hata huyo Moosa Mao nae anao mkataba, sasa hoja yako hapo ni ipi?!

Btw, kwanini nimuamini mtu ambae tayari mamlaka ina mashaka nae, kiasi cha kufikia kumsimamisha kazi?
Sasa unataka na sisi tusimuamini kwa blaa blaa zako hizi?

Leta mkataba hapa ili tuungane na wewe kumbeza Kakoko na utakuwa umetukata ngebe kabisa.
 
Sasa unataka na sisi tusimuamini kwa blaa blaa zako hizi?

Leta mkataba hapa ili tuungane na wewe kumbeza Kakoko na utakuwa umetukata ngebe kabisa.
Kwavile umeshindwa kujadili hoja zilizotolewa, wacha niendelee kujibu hoja zinazojadili hoja!! That being said, stay blessed!!!
 
Sasa unataka na sisi tusimuamini kwa blaa blaa zako hizi?

Leta mkataba hapa ili tuungane na wewe kumbeza Kakoko na utakuwa umetukata ngebe kabisa.
Huu mradi Mkataba wake utakapokuwa wazi bila udanganyifu kabisa, tutataka uchunguzi wa Hizi kelele nyingi kutoka Kwa Watanzania hawa,

Watu wako tayari kutuonyesha uzuri wa mradi na manufaa yake, lakini hawako tayari kabisa kuzungumzia Mkataba na masharti yake, unajiuliza ni Kwa nini?

Spika naye, badala ya kuanza na Mkataba mle bungeni, anaanza kutuonyesha utamu wa mf wa Bandari iliyoko China yenye mfano kama hii itayojengwa Bagamoyo na jinsi itakavyoinufaisha nchi, ni Jambo jema, lakini Kwa nini asianze na kiini??

Maana mradi haujijengi wenyewe, na kama ni hivyo, tunataka sasa Mkataba utakoingiwa Kwa makubaliano basi!!!

Uzuri na manufaa ya mradi yananafasi ya pili baada ya Jambo mhimu ambalo ni Mkataba na masharti yake,
 
Umeongea ukweli kabisa mkuu!
 
Kwahiyo unaamini kabisa kwamba kuna siku watakuonesha huo mkataba?!

Btw, how come unasema "Watu wako tayari kutuonyesha uzuri wa mradi na manufaa yake, lakini hawako tayari kabisa kuzungumzia Mkataba na masharti yake, unajiuliza ni Kwa nini?" wakati nimesema wazi ni mambo gani LAZIMA China wata-demand, na yapi yanapaswa kuwapa na yapi hayapaswi kuwapa?

The problem wengi wenu ni wavivu wa kusoma, na kwahiyo wala hamjasoma kilichoandikwa!!! Hata mngewekewa huo mkataba, wala msingesoma!!!

Na hili la kutosoma linawafanya Wabongo wawe victims wa urongo wa viongozi kwa sababu wanajua wanaweza kudanganya, na watu hawatahangaika kuuafuta ukweli... ukweli ambao mara nyingi tu unakuwa kwenye public domain!!
 
Kwavile umeshindwa kujadili hoja zilizotolewa, wacha niendelee kujibu hoja zinazojadili hoja!! That being said, stay blessed!!!
Mkuu Chige, labda niseme hivi, hayupo Mtanzania yeyote anayeweza kupinga mradi mradi mzuri kama huo, Ila kuna Mtanzania anayepinga uwepo wa mradi huo Kwa sababu ya fununu za masharti yaliyopo kwenye Mkataba,

Na hata wewe mkuu, Kwa nini haukuwa tayari kuambatanisha na vipengere Vya Mkataba wa mradi unaousifia Sana?

Bila kukufahamu Mkataba na masharti yake, ni kupigia Kampeni shetani ili awe mlinzi wa familia yako
 
SEHEMU YA PILI.

Hoja zinazotolewa na Wazalendo Kupinga Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.

Wachina Watachukua Mapato YOTE ya Bandari ya Bagamoyo.

Hii ni moja ya hoja zinazotolewa na Wazalendo wetu wanaopinga Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Bandari, Deusdedit Kakoko nae alipata kusema “…Wachina wanataka kuchukua mapato yote, na wanataka wasilipe kodi kwa miaka 30.”

Ukweli ni kwamba, haya ni madai ya kushangaza!

Ni madai ya kushangaza kwa sababu ni jambo lisiloingia akilini. Na ikitokea Wachina wakachukua MAPATO YOTE basi Tanzania tutaweka historia mpya duniani kwa sababu hakuna kitu kama hicho popote pale duniani!

Labda niseme jambo moja! Aya yangu hiyo hapo juu ni namna tu ya kusema kiungwana kwamba MADAI HAYO NI UONGO!

Kakoko kasema Wachina wanataka wasamehewe kodi kwa miaka 30! Hata hivyo, hatuambii ni kodi ya aina gani wanayotaka wasamehewe!

Kubwa zaidi, maelezo ya Kakoko yalikuwa yamekaa ki-propaganda mno… propaganda zile zile za ki-MATAGA za kujifanya wao ndo Wazalendo sana na wana uchungu sana na hii nchi wakati ni WANAFIKI tu, ambao “uzalendo” wao ulikuwa kwa JPM, na sio kwa nchi!

Ni kutokana na uongo huu wa Kakoko ndo maana haikushangaza kwa mara ya kwanza kuwaona Wachina wakioka mbele na kumshutumu Kakoko kwamba ni MWONGO.

Kwa mfano, gazeti la The Citizen la October 28, 2019 lilimnukuu Mwakilishi wa Uwekezaji wa China Merchant Group, Mr. Moosa Mao akisema:-

Na hata kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mr. Mao aliandika:-

View attachment 1765244

China Merchant Group ndio walitarajiwa kuwekeza kwenye Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.

Hapa tuweke kumbukumbu sawa linapokuja suala la kodi kwa kuangalia muktadha wa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.

Katika hali ya kawaida, kutakuwa na awamu mbili zinazohusiana na kodi kwenye mradi huu.

Awamu ya kwanza ni wakati wa shughuli za ujenzi wa bandari, na awamu ya pili ni pale bandari itakapoanza kufanya kazi.

Wakati wa ujenzi, tunatarajia vifaa vingi vitaagizwa kutoka nje, ingawaje tutakuwa Viumbe wa Ajabu sana endapo tutaruhusu uingizaji hadi wa vifaa ambavyo wenyewe tunavyo, kama vile saruji.

Kuhusu hilo la vifaa, hapa Mchina namtarajia atakuwa ameomba asemehewe kodi ya uingizaji wa hivyo vifaa!

Na kwa bahati, hatakuwa amefanya dhambi yoyote kwa sababu Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, yaani VAT Sura ya 148, na Sheria ya Fedha ya mwaka 2017, 2018 na 2019 zinatoa mwanya kwa Mwekezaji kuomba msamaha wa kodi “on imported capital goods”.

Hata ukiingia kwenye tovuti kuu ya serikali utakuta maneno haya:-

Hivyo, hapo utaona wazi kwamba ni suala la kisheria! Na jambo kama hilo sio Tanzania tu bali sehemu mbalimbali duniani huwa wanafanya hivyo ili kuvutia uwekezaji!!

Kitaalamu, suala hilo linaitwa Tax Incentives. Na hata uki-Google “Tax Incentives in Tanzania”, moja kwa moja utakutana na link ya TRA ikiwa juu kabisa ya matokeo ya utafutaji; yaani Google Search Results!

Suala la kodi na ushuru bandari itakapoanza kufanya kazi.

Kama nilivyosema hapo awali, Mhandisi Kakoko alituambiwa “Wachina wanataka wasamehewe kodi kwa miaka 30,” huku Wazalendo wengine wakituambia TRA hawataruhusiwa hata kutia pua hapo bandarini!

Hapa ieleweke kwamba, popote pale duniani kodi ni MALI YA SERIKALI, na ndio maana, ukisoma hiyo screenshot ya Twitter kutoka kwa Moosa Mao, amekanusha suala la eti TRA hawataruhusikiwa kukusanya kodi!

Na ndio maana, wewe milikishwa ekari 1000 na baba yako, kisha tumia pesa zako mwenyewe kufanya uwekezaji bila kuomba hata senti moja kutoka popote pale!

Pamoja na yote hayo, ukimaliza tu uwezekaji wako na kuanza kufanya biashara, TRA wanakuwa wageni wako wa kudumu, ingawaje hukuchangiwa chochote na yeyote!

Lakini kwa upande mwingine, popote pale duniani, serikali huwa zinasamehe baadhi ya kodi. Bandari ya Bagamoyo ikishaanza kufanya kazi, tunatarajia kuwepo angalau kodi zifuatavyo:-

  • Kodi ya Ongezeko la Thamani… VAT on imported goods
  • Kodi ya Mapato (Income Tax)
  • Ushuru wa Uingizaji Bidhaa (Import Duty)
  • Ushuru wa Forodha, na zingine.
Sasa basi, tuseme wewe na mimi, or anyone ameagiza magari au bidhaa yoyote ambayo sio miongoni mwa bidhaa zilizo kwenye kundi la msamaha wa kodi!

Hilo likifanyika, Importer atalazimika kulipa angalau moja ya kodi nilizotaja hapo juu! Kodi hiyo ni LAZIMA IKUSANYWE NA TRA kwa sababu, kama nilivyosema awali, always, Kodi ni Mali ya Serikali.

Sasa je, kuna uwezekano Mchina akataka msamaha wa kodi baada ya bandari kufanya kazi?

Jibu ni NDIYO!

Kutokana na uzoefu niiopata kutoka kuwa Mbeba Mikoba wa Beberu, na kwa kuangalia “case studies” za bandari zingine ambako Mchina amewekeza, hapo kuna uwezekano mkubwa Mchina akaomba msamaha wa Income Tax. HOW?

Bandari ikishaanza kufanya kazi, Mchina atakuwa anatoa huduma kadhaa kama vile kuhifadhi mizigo, kupandisha na kupakuwa mizigo, kuzitoza meli ambazio zitakuwa zinafunga nanga hapo bandarini, n.k.

Kwa kutoa huduma hizo, ina maana Mchina atakuwa analipwa pesa!! Katika mazingira ya kawaida, pesa anazopata ni mapato yanayostahili kukatwa kodi!

Ni hiyo kodi itakayotokana na hizo huduma ndiyo ambayo sina shaka Mchina atataka asamehewe!! Na huu ndio ukweli ambao kwa makusudi, Mzalendo Kakoko hakutaka kusema ukweli, na badala yake akafanya majumuishi kwamba Mchina anataka kusamehewa kodi kwa miaka 30, bila kutaja ni kodi ipi!

Katika hili la kodi, nililazimika kumtumia email yule Researcher niliyekuwa nae, kwa sababu mimi binafsi sikupata fursa ya kuonana na watendaji wa serikali!

Nililazimika kumtumia email na kumuuliza ingawaje tayari nilishakuwa nafahamu majibu ya maswali yangu. Hata hivyo, nilitaka tu kujiriidhisha kutoka kwake, kwa sababu yeye ni mzoefu sana kwenye haya mambo ya uwekezaji duniani!

Jibu lake lilikuwa hili hapa chini:-

View attachment 1765245
Swali hilo nilimuuliza miaka 2 iliyopita, na mtaona jibu lake linaenda sawa na jibu la Moosa Mao!

Aidha, miongoni mwa maswali ambayo watu wamekuwa wakijiuliza ni kwamba: Sasa kama TRA watakuwa wanachukua kodi, Mchina atarudisha vipi pesa yake!

Jibu la hilo swali unatakiwa kujiuliza: Je, Mamlaka ya Bandari huwa wanakusanya kodi? Kama hawakusanyi, je mapato yao yanatoka wapi? Jibu la swali la pili ndilo jibu la swali la Mchina atarudisha vipi mapato yake!
Bandiko lako limekaa kisomi sana sijui kama hapa akina Wakudadavua, NdegeJohn na kifupikirefu kama watachomoka.
 
UTANGULIZI

Amini usiamini, wale wale ambao wamekuwa wakijivika uzalendo, linapokuja suala la Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, ndiyo hao hao wanaotumikia Mabeberu bila wao kujijua!

Nitajadili mada hii katika sehemu mbili:-
  • Kwanini wale wanaoitwa Mabeberu hawawezi kuwa tayari kuona miradi kama ya Bandari ya Bagamoyo inafanikiwa, na
  • Hoja zinazotolewa na Wazalendo Kupinga Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.
Kwa bahati, binafsi mwaka 2016 nilikuwa “Mbeba Mikoba” wa Researcher mmoja wa Kimarekani (Beberu?) aliyekuwa anafanya utafiti kuhusu Belt and Road Initiative (BRI).

Kazi yangu kubwa ilikuwa Literature Review!

Kwa wanaofahamu mambo ya Resech, ukifanya Literature Reviews, hususani ya wasomi kama huyu bwana, basi unapata fursa ya kufahamu mambo mengi zaidi yaliyopata kutokea hapo kabla kwenye eneo husika!

Kwa wasiofahamu, Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni matokeo ya (BRI) ambayo, Rais wa China, Xi, anailezea BRI kwamba:

Kwa lugha nyepesi, malengo ya China kupitia BRI ni kuiunganisha nchi hiyo na sehemu zingine duniani, hususani Asia, Afrika, na Ulaya! Uunganishaji huo ni kwa ujenzi wa miundombinu, hususani ya bandari, reli, na viwanja vya ndege.

Ndugu yangu MALCOM LUMUMBA alipata kuchambua kwa undani kabisa suala la Belt and Road Initiative!!

Na hapo sidhani kama mtu anahitaji kuwa na Shahada ya Diplomasia ya Uchumi na Ushikirikiano wa Kimataifa kunusa “threat” ya mpango huo wa China kwa mataifa makubwa, hususani Marekani!

Kutokana na ukweli huo, ndo maana haishangazi mara tu BRI ilipotangazwa, Waandishi na Watafiti mbalimbali kutoka nchi za magharibi wakaanza kulivalia njuga suala hilo.

Makala zikaandikwa, na tafiti zikafanywa kuhusu BRI, lakini makala nyingi kama sio zote zililenga kuyatisha mataifa mengine kuwa makini na BRI!

Watu hawa wakageuka kuwa “Wajomba Zetu” Afrika, huku wakituasa tusije tukaingia kwenye mtego huo hatari wa China!

Ni kupitia hizo tafiti ndipo nami nikajikuta nipo na huyo Mtafiti Msomi kweli kweli wa Kimarekani.

Huyu Bwana case studies zake zilikuwa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, Bandari ya Hambantota (Sri-Lanka), pamoja na Bandari ya Piraeus (Ugiriki).

Ukweli ni kwamba, ilinichukua chini ya dakika 3 kugundua Mtafiti huyu ni kama tayari alishakuwa na “matokeo” ya utafiti wake hata kabla kazi haijaanza! Kwa kifupi, alionesha dalili zote za kutounga mkono Mradi wa Bandari ya Bagamoyo!

Hata "beberu" niliyekuwa namtumikia, nae alikuwa pamoja na "Wazalendo" wetu!!

Binafsi, nilikuwa “in favor of” Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, kwahiyo tukaanzisha kimdaharo kisicho rasmi!

Baada ya kuona hoja zake nyingi nazipangua, akaishia kuuliza ikiwa nadhani ni busara kwa taifa maskini kama Tanzania kuwa na bandari kubwa kama ya Bagamoyo!!

Jibu langu kwake lilikuwa rahisi sana, kwamba: Bandari ya Bagamoyo itakuwa ni kubwa mno kwa Tanzania endapo tu unaamini Tanzania na majirani zake wataendelea kuwa maskini kwa miongo kadhaa ijayo, vinginevyo, huwezi kusema ni “kubwa mno”!

Kwa ufupi, Mheshimiwa huyu, kama walivyokuwa wenzake wengine, nyimbo zao zilikuwa ni agenda ya siri ya China kuitumia BRI kama Mtego wa Madeni kwa nchi maskini!

Lilipokuja suala la Bandari ya Hambantota kule Sri-Lanka, propaganda zikasambazwa kwamba China IMEITWAA bandari ya Sri Lanka ili kufidia deni lake!

Wazalendo wetu nao wakazidaka propaganda hizo, na bila kufanya utafiti, wakaanza kutueleza kwamba “tukishindwa kulipa deni, Wachina wataichukua Bandari ya Bagamoyo kama walivyofanya kule Sri-Lanka.”

Kuweka kumbukumbu sawa, habari za Wachina KUITWAA bandari hiyo zilipotoshwa. Nitaeleza hili kinaga ubaga hapo baada kwenye makala hii.

Pamoja na suala la “Debt Trap”, watu hawa tunaowaita Mabeberu ambao kwa hili tunawaona wanajali maslahi yetu, pia wakawa wanatuambia agenda nyingine ya siri ya China ya kuanzisha “military base” kupitia BRI.

Hapa wakawa wanalenga kutuambia, hata mradi kama wa Bandari ya Bagamoyo, lengo lake ni Wachina kutaka kuweka kambi za kijeshi eneo hili la Afrika Mashariki!

Hata hivyo, hawatuambii ukweli kwamba, ni wao wenyewe ndio wanaozihofia hizo “military bases” za China endapo zitawepo!

Kila mfuatiliaji wa mambo duniani, anafahamu Marekani ina kambi za kijeshi sehemu kadhaa duniani, lakini linapokuja suala la China au mataifa mengine kufanya yale yale ambayo yeye keshayafanya kwa miongo kadhaa, hapo inageuka kuwa nongwa!

Waingereza wana msemo “If you can’t beat them, join them.”

Guys, amini usiamini, juzi yule Mtafiti niliyekuwa nae ametoa makala kwenye moja ya majarida maarufu sana duniani! Baada ya kuisoma makala ile, hapo hapo nikajisikia uchungu, na kumhurumia!

Yaani yule yule aliyekuwa anaipinga BRI, kwenye hiyo makala anaulaumu wazi wazi Utawala wa Trump kwa kutumia kete ya Debt Trap kama njia ya kuidhoofisha BRI.

Kwenye makala hiyo, kuna sehemu anahoji “Kama kweli BRI ni kitu kibaya kiasi hicho, ni kwanini basi China inaendelea kutafuta Washirika walio tayari kujiunga na BRI.”

Mwishowe, Mtafiti huyu anaisemanga serikali yake kwamba ”USA haitaweza kumzuia Rais wa China kuwekeza kupitia BRI endapo US haitakuwa na mbadala kwa mataifa yanayoshirikiana na China!

Ufaransa, imeanza kuliona hilo kama ilivyowahi kuripotiwa na France24 kwamba:

Desperation ya Mtafiti huyu bila shaka inatokana na vile anavyoona jinsi ambavyo nchi mbalimbali duniani jzinavyojiunga na BRI, kinyume na matarajio ya USA ambayo ilikuwa ina-lobby nchi zingine, hususani Washirika wake kutojiunga na BRI.

Kwa bahati mbaya sana, si Afrika, si Asia! Hadi baadhi ya nchi za Ulaya na Carribean zinaingia kwenye BRI. Mbaya zaidi, miradi ya BRI inaonekana kufanya vizuri sana!

Kwa mfano, mwaka 2016 Bandari ya Piraeus ilikuwa ndio ya kwanza barani Ulaya kubinafsishwa chini ya BRI. Bandari hii ndiyo bandari kubwa kuliko zote nchini Ugiriki, na ndio langu kuu la bahari linalounganisha nchi za EU na Asia!

Hapo kabla, bandari hii ilikuwa haifanyi vizuri, na ripoti za nyuma zilikuwa zinaiweka bandari hiyo kama bandari ya 17 barani Ulaya!

Baada ya Wachina kuchukua 51% ya hisa za bandari hiyo, na hatimae hisa hizo kufikia 67%; ripoti ya mwaka huu kupitia Port Economics inasema kwa sasa Bandari ya Piraeus ndiyo bandari kubwa zaidi (kwa kiwango cha makontena) kwenye ukanda wa Bahari ya Mediterranean, na ya 5 Barani Ulaya!!

Sasa haya ndo mambo ambayo watu hawakuyataka! Yaani bandari iliyo kwenye ardhi ya Mzungu, 67% imilikiwe na Mchina, na hapo hapo inaanza kutishia ushawishi wa bandari zingine zinazomilikiwa na Wazungu wenyewe!

JokaKuu
NAOMBA MSAADA WA KUNITAJIA BEBERU MMOJA TU AMBAYE TANZANIA TUNAPASWA KUTOSHIRIKIANA NAYE KWA LOLOTE
 
Back
Top Bottom