Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Bandiko lako limekaa kisomi saa.sijui kama hpa akina Wakudadavua, NdegeJohn na kifupikirefu kama watachomoka.
Dah! Hao uliowataja hawajaingia lakini wengine sawa na hao imekuwa taabu tupu!!!
 
unamuuliza Chige au serikali?
Nilimuuliza Yule aliyekuwa akifokea ufafanuzi wa JPM kuhusu mradi huu, a nilijua labda yeye anao huo Mkataba na ndio Maana labda imempa uhalali wa kumfokea aliyejaribu kutufafanulia Kwa kiduchu kuhusu mashariti ya Mkataba huo

Je, umewahi kuusoma Mkataba mkuu
 
NAOMBA MSAADA WA KUNITAJIA BEBERU MMOJA TU AMBAYE TANZANIA TUNAPASWA KUTOSHIRIKIANA NAYE KWA LOLOTE
HAKUNA!!

What matters ni maslahi ya taifa! So, any beberu endapo atakuwa na proposal itakayokuwa na maslahi kwa taifa, tunapaswa kushirikiana nae!! Na "mjomba" yeyote kama ataleta proposal isiyo na maslahi kwa taifa, hatupaswi kushirikiana nae, at least kwenye hiyo propasal yake!

Ndugu yangu MALCOM LUMUMBA anafahamu kwamba mimi ni kibaraka kindakindaki wa mabeberu, lakini huwa nagawa mstari kati ya international cooperation, and international relations!

Huku kwenye international cooperation, I don't care "Ubeberu" wako provided you have something tangible to offer that defines our national interests!

Hawa wajomba ninaowaweka kwenye kundi la international relations, nitaendelea kuwaheshimu kama wajomba zangu, na nitadumisha udugu wetu daima dumu, but if they can't offer what defines our national interests, wanisamehe tu kwa kweli... tutakutana na kupiga michapo wakati wa misiba, harusi na shughuli za jando na unyago!!

Udugu haufi!!
 
Nilimuuliza Yule aliyekuwa akifokea ufafanuzi wa JPM kuhusu mradi huu, a nilijua labda yeye anao huo Mkataba na ndio Maana labda imempa uhalali wa kumfokea aliyejaribu kutufafanulia Kwa kiduchu kuhusu mashariti ya Mkataba huo

Je, umewahi kuusoma Mkataba mkuu
Na mimi nlitaka kuuliza hichi kitu, je ameuona mkataba au anandika kwa hisia...
Kumtuhumu mtu km kakoko aliekua jikoni na mwenye access ya Mkataba kua ana toa Maoni ki Mataga ili hali mtoa uzi hajauona mkataba sio sawa...
Unaweka screenshot za mchina akikanusha...kwani ulitaka afanyeje, hio ndio PR yenyewe, does it prove anything? No, iv he has guts ange screeshoy vipengele vya mkataba aviweke then inge make sense, ila haya mambo ya his words aginst their doesnt prove anything.
Whatever it is huu mradi tuujenge wenyewe..km tumeweza kufanya miradi mingine mikubwa ht huu hautatushinda.
 
Kwahiyo unaamini kabisa kwamba kuna siku watakuonesha huo mkataba?!

Btw, how come unasema "Watu wako tayari kutuonyesha uzuri wa mradi na manufaa yake, lakini hawako tayari kabisa kuzungumzia Mkataba na masharti yake, unajiuliza ni Kwa nini?" wakati nimesema wazi ni mambo gani LAZIMA China wata-demand, na yapi yanapaswa kuwapa na yapi hayapaswi kuwapa?

The problem wengi wenu ni wavivu wa kusoma, na kwahiyo wala hamjasoma kilichoandikwa!!! Hata mngewekewa huo mkataba, wala msingesoma!!!

Na hili la kutosoma linawafanya Wabongo wawe victims wa urongo wa viongozi kwa sababu wanajua wanaweza kudanganya, na watu hawatahangaika kuuafuta ukweli... ukweli ambao mara nyingi tu unakuwa kwenye public domain!!
Sasa...! Kwani tuko hapa Leo Kwa sababu gani mkuu, Ni Kwa sababu ya kuonekana masharti yaliyoko Kwa Mkataba hayana tija ingawa uwekezaji huo Una tija

Tunauliza Mkataba Kwa sababu kuna aliyewahi kuusoma na akatoa Kwa kidogo ubaya uliomo katika Mkataba huo,

Hoja nyingi hapa, ni kupinga udokezi wa masharti hayo ni Kwa sababu aliyedokeza, hamkumwamini, sasa nyinyi mnaotaka tuwaamini, ndio tunaomba viambatanisho Vya Mkataba mtuonyeshe,

Mnapoulizwa, mnarudi kulekule kwamba, Mkataba upo Kwa mwanasheria, Kwa nini sasa hamuwaamini waliousoma na kutuambia ubaya na uzuri wake??

Shida iko wapi, Bado nazidi kuhitimisha kwamba, kama kweli mnataka Tumpuuze JPM, leteni Mkataba hapa, la sivyo mnajifunza umbea wenye Mashaka ya Kula pesa za mchina
 
Bandari ya bagamoyo ni muhimu sana kwa sasa maana tayari zilizopo zina limitations kuweza kufanya mabadiriko kuja kwenye mifumo ya bandari ya kisasa...

Either tuangalie namna ya kuijenga wenyewe kidogokidogo au tutafute uwekezaji wenye masharti rafiki kwa pande zote..

Issue ya wachina vs bandari ya bagamoyo tayari hakuna anayeujua ukweli zaidi ya propaganda hasa za awamu ya tano...Rais wetu kipenzi hayati JPM alikuwa anaongea mambo mengi kwa propaganda in public kiasi cha kutengeneza chuki baina yetu...hali imesababisha sintofahamu na propaganda nyingi kwenye ujenzi wa bandari hii....naamini tuna watalaam kama mambo hayako sawa ni vyema wakajifungia kujadiliana kuliko kutoka mbele na kuwaita wengine wajinga na wapumbavu..
 
"Pamoja na yote hayo, katu simaanishi kwamba Mkataba wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo upo PERFECT, au ni mkataba bora… la hasha!! Tanzania haijawahi kusaini mkataba ulio bora!"
nimeishia hapa!
 
Sasa...! Kwani tuko hapa Leo Kwa sababu gani mkuu, Ni Kwa sababu ya kuonekana masharti yaliyoko Kwa Mkataba hayana tija ingawa uwekezaji huo Una tija

Tunauliza Mkataba Kwa sababu kuna aliyewahi kuusoma na akatoa Kwa kidogo ubaya uliomo katika Mkataba huo,

Hoja nyingi hapa, ni kupinga udokezi wa masharti hayo ni Kwa sababu aliyedokeza, hamkumwamini, sasa nyinyi mnaotaka tuwaamini, ndio tunaomba viambatanisho Vya Mkataba mtuonyeshe,

Mnspouluzwa, mbarudi kilekile kwamba, Mkataba upo Kwa mwanasheria, Kwa nini sasa hamuwaamini waliousoma na kutuambia ubaya na uzuri wake??

Shida iko wapi, Bado nazidi kuhitimisha kwamba, kama kweli mnataka Tumpuuze JPM, leteni Mkataba hapa, la sivyo mnajifunza umbea wenye Mashaka ya Kula pesa za mchina
Hao waliokuambia masharti ya mkataba hayana tija wamekuonesha mkataba?

Na kama unataka nimuamini Kakoko kwa sababu yeye ndo kaona mkataba, sasa kwanini na wewe hutaki kumwamini Moosa Mao wakati na yeye kaona mkataba, na anao?
 
Moosa Mo he just a PR guy...that's what they supposed to do...minimize the demage and keep the company image clean.
 
Hao waliokuambia masharti ya mkataba hayana tija wamekuonesha mkataba?

Na kama unataka nimuamini Kakoko kwa sababu yeye ndo kaona mkataba, sasa kwanini na wewe hutaki kumwamini Moosa Mao wakati na yeye kaona mkataba, na anao?
Mkuu, habari za Moosa Mao, ni habari ambazo siwezi kuzipa nafasi Kwa kipindi hiki ambapo kama Taifa tumegawanyika sehemu mbili, naweza kudhani labda huyo Mao ni wa kutengeneza tu ili kuleta ushawishi Kwa mradi huu, tutajuaje..! Technologia ilivyopanuka kiasi hiki!!

Najua naweza kuwa kero kwako, lakini, ili kurudisha Imani Kwa Watanzania wote, Mkataba upelekwe bungeni na uwe wazi ndipo tuwapuuze zaidi kina kakonko
 
Bandari ya bagamoyo ni muhimu sana kwa sasa maana tayari zilizopo zina limitations kuweza kufanya mabadiriko kuja kwenye mifumo ya bandari ya kisasa...

Either tuangalie namna ya kuijenga wenyewe kidogokidogo au tutafute uwekezaji wenye masharti rafiki kwa pande zote..

Issue ya wachina vs bandari ya bagamoyo tayari hakuna anayeujua ukweli zaidi ya propaganda hasa za awamu ya tano...Rais wetu kipenzi hayati JPM alikuwa anaongea mambo mengi kwa propaganda in public kiasi cha kutengeneza chuki baina yetu...hali imesababisha sintofahamu na propaganda nyingi kwenye ujenzi wa bandari hii....naamini tuna watalaam kama mambo hayako sawa ni vyema wakajifungia kujadiliana kuliko kutoka mbele na kuwaita wengine wajinga na wapumbavu..
Nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa sana, ingawaje nina mashaka ikiwa tutaijenga wenyewe, halafu kwa ukubwa ule ule aliotaka Mchina, je, tutaweza kui-utilize?

Unajua anachofanikiwa Mchina kwenye miradi mikubwa kama hii ni kwa sababu ana percentage share kubwa sana ya mzigo unaosafiri duniani!

Kuna mamia ya meli kutoka sehemu mbalimbali duniani zinaoingia na kutoka China kila mwezi!! Kutokana na hili, China ana uwezo wa ku-influence bandari zake kuwa busy!!

Sasa assume, sisi tunajenga bandari kuuubwa kama Bagamoyo, na Mchina anajenga bandari kuuubwa Lamu! Hapo ni obvious meli nyingi za China zitaenda Lamu! Hili ndilo liliwakwamisha Bandari ya Hambantota na Piraeus!!

Kuna watu wamekuwa wakihoji kwamba: Hivi huko duniani wakisema "madini yenu hatuyataki tena", hivi tutyayafanyia nini wenyewe kama wenyewe?!

Au ndo itakuwa mwendo wa kuning'iniza vito kwa kwenda mbele?!

Mfano huo wa madini ndo kama bandari! Mchina hamtegemei someone else aje ku-utilize bandari zake bali ni yeye mwenyewe ndie mwenye uwezo wa kufanya hivyo!!!
 
HITIMISHO

Tukubali tusikubali, fursa ya Bandari ya Bagamoyo ikituponyoka tutakuja kuijutia pale Mchina atakapoamua kurejea tena Lamu, au popote pale kwenye ukanda huu wa Bahari ya Hindi!

Inashangaza sana karne ya 21 bado kuna Watanzania wana mawazo yale yale ya Ujima kwamba, eti “madini hayaozi”, na tutakuja kuchimba wenyewe tukishapata uwezo!

Injinia Kakoko na mwenyewe aliwahi kunukuliwa akisema “…na sisi bandari ile (Bagamoyo), tulifanya feasibility study na TPA. Na TPA kupitia serikali, itawekeza na kuijenga wakati utakapokuwa umefika.

Ni wazo zuri kama serikali itakuwa na uwezo wa kujenga hiyo bandari wao wenyewe haidhuru hata kama tumeshindwa kujenga bandari yoyote ndani ya miaka 60 ya uhuru!

Hata hivyo, Kakoko na wengine wanatakiwa kufahamu kwamba, hoja sio kuwa na uwezo wa kujenga bandari bali uwezo wa ku-utilize bandari husika!

Nimetoa mfano wa Bandari ya Piraeus huko Ugiriki ambayo kabla ya uwekezaji wa China, bandari hiyo ilikuwa haifanyi vizuri. Hata hivyo, baada ya Mchina kuingia, Bandari ya Piraeus imegeuka na kuwa ndiyo bandari kubwa kuliko zote Ukanda wa Mediterranean, huku ikichukua nafasi ya 5 Barani Ulaya!

Na ndivyo hivyo kwa Bandari ya Hambantota ambayo na yenyewe ilikuwa haifanyi vizuri lakini hivi sasa hali imebadilika.

Na sababu kubwa ya China kuwa na uwezo wa kuzifanya bandari anazoendesha kufanya vizuri inatokana na ukweli kwamba China ina-handle biashara kubwa sana duniani. Kwa maana nyingine, China ina uwezo wa ku-utilize bandari zake kupitia mizigo yake tu.

Lakini kwa upande mwingine, Mradi wa Bandari ya Bagamoyo pia unahusisha Industrial Complex kubwa sana! Lengo la Mchina ilikuwa ni kujenga viwanda kwenye eneo la bandari, ili baadhi ya bidhaa zake anazosafirisha kutoka China hadi Afrika ziwe zinazalishwa Bagamoyo.

Ninachotaka kusema ni kwamba, pamoja na suala la kodi, mradi huu endapo ungekamilika, ungekuwa chanzo kikubwa cha ajira kwa wananchi!

Bandari ya Bagamoyo sio kama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chato! Hivyo basi, hata kama tuseme Mzee wa Msoga alilenga kupendelea kwao, hivi kuna mwenye akili timamu anayeweza kuthubutu na kudai kwamba, watakaofaidika na bandari hiyo ni Wakwere na Wazaramo wa Bagamoyo?

Halafu hii nchi ilivyo na viumbe wa ajabu, hao hao wanaosema JK alikuwa anataka kupendelea kwao, kwa kiasi kikubwa ndo hao hao wanaodharau watu wa Pwani kwamba HAWAJASOMA, na kwamba wanaishia kuendekeza madrasa!

Sasa kwavile nyie ndio mliosoma, hamuoni kwamba ni nyinyi wenyewe ndio mtakaofadika na mradi huo huku Wakwere na Wazaramo wakiishia kuwauzia kahawa?

Ukubwa wa mradi ule unaweza kuzalisha Pay As You Earn (PAYE) kutoka kwa wafanyakazi ambayo ni kubwa kuzidi hata thamani ya ukodishaji wa ardhi!

Na hii PAYE ni endelevu kwa miaka na dahari!

Pamoja na yote hayo, katu simaanishi kwamba Mkataba wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo upo PERFECT, au ni mkataba bora… la hasha!! Tanzania haijawahi kusaini mkataba ulio bora!

Ambacho ningependa kukiona kwenye hili ni Watendaji na Wafanya Maamuzi kuwa “objective”, na pia waache kusambaza habari za uongo ili mradi tu kuhalalisha ajenda zao.

Wengine ajenda zao ni aibu hata kuzitaja hadharani!

Watu hawa wanatakiwa kukaa na wadau, na kuangalia ni kwa namna gani huu mradi unaweza kufanyika huku tukiacha kile kiburi chetu cha Uzalendo Fake Uliopandikizwa na Mfumo wa Ujamaa!

Aidha, wanatakiwa kukaa na wadau kuangalia ni mfumo upi utaweka mbele maslahi mapana ya taifa.

Na kama nilivyosema kwenye utangulizi wangu, Wapinzani wa Bandari ya Bagamoyo wanawatumikia wale wale wanaowaita Mabeberu bila wao kujijua! Mabeberu walianza kuipinga Belt and Road Initiative ya China tangu kuanzishwa kwake!

Kwa bahati mbaya sana, hao hao waliokuwa wanapinga BRI, hivi sasa wanaanza kuingia mmoja mmoja! Kuna dalili zote kwamba Marekani imeanza kusalitiwa na Washirika wake, hata wale wa Jumuiya ya Ulaya.

Kwa mfano, Jarida la The Diplomat la March 23, 2021 linatueleza kwamba:-

Aidha, wakati Marekani ikihangaika na BRI, mwaka juzi tu hapa, huko China ulifanyika mkutano mkuuubwa wa BRI kama ilivyoripotiwa na UNDP-Asia kwamba:-

Na kwa mujibu wa Serikali ya China, kupitia Belt and Road Portal, wanasema kwamba:-

Mzee wa Msoga aliwahi kutujuza kwamba: Akili za Kuambiwa, Changanya na Zako!
Mzee, wewe kweli mwana research, liteeature review uko vizuri inashawishi.
Wengine huchagua siasa ya nguvu badala ya nguvu ya siasa kuamua mambo.
Yaani kwangu mimi mtu aaminiye uwepo wa mabeberu ni sawa tu na mkemea mapepo. Dunia hii ni kupambana. Yeyote aweza bila ya visingizio...
 
Na ajabu zaidi, hata huyo wanaemtetea, hajawaonesha mkataba licha ya kuwaambia tu, mara mradi hivi, mara mradi vile!!!
Jiwe alisaga akili za watu wengi hapa nawaza angekuwa hai mpaka amalize muda wake nakujiongezea sijui tungekuwa na Taifa la watu gani

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Kama hakushiriki katika kusaini na haui kilichokuwemo kwanini anashikia bango jambo asililolijua?

Aliyesaini mkataba huo ni Dr Mary Nagu (Waziri Uwekezaji na Uwezeshaji) mbele ya Rais wa Tanzania J Kikwete na Rais wa China Xi Jinping mwaka 2013.

Acheni kupigia chapuo suala la msingi kama hilo ambalo undani wake hauelewi kinagaubaga
Jamaa ameongea kwa namna alivyoshiriki kwenye hizo Tafiti ameongea anachokijua hakusema ameona mkataba kilichotakiwa mnaopingana nae mje pingamizi zenu with evidence kumpinga bila Hoja ndio mkwere alisema msiipige RUNGU maana haitakufa isipokuwa Hoja itakufa kwa Hoja iliyobora zaidi so kwa mfano alichoandika jamaa hakitafutika kwa jazba kama anavyofanya mchangiaji mmoja humu....
hili jukwaa lilikuwa na mijadala ya maana watu walikuwa wanaArgue mtu anashindwa kwa Hoja sasa hii imekuja sasa watu kuporomosha matusi sidhani kama inatusaida kama Taifa

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Porojo at work!

Kila mwenye akili timamu anafahamu Jiwe nae ni miongoni mwa wezi wakubwa waliopata kutokea nchi hii.

Katumia billions of TZS kununua ndege, hata nikikuuliza wewe na ukoo wako wote ni wapi tenda ilitangazwa, hamuwezi kuwa na majibu! Ili asikaguliwe, akaamua kuhamishia Wakala wa Ndege za Serikali Ikulu, huku akiacha misukule yake ikiimba nyimbo za mapambio!!

Halafu hivi hujishtukii unavyosema "tunataka kila kitu wazi wazi" wakati utawala wa JPM ndio uliongoza kuficha yale yanayofanyika huko serikalini?!
Kawaambie hao mabwana wako Wachina Mzalendo wetu JPM alishatufungua macho. Wakitaka mradi uendelee waje na masharti yatakayokuwa na manufaa kwa pande zote mbili. Hatupo tayari kuwauzia nchi. Kumchafua JPM hakusaidii.
 
Mkuu umeeleza Jambo kwa uzuri kadiri ulivyohusika ktk research, ni wakati sasa serikali kuangalia mapungufu yaliyomo kwenye mkataba na kuyafanyia kazi ili mradi huu uanze.
 
Kawaambie hao mabwana wako Wachina Mzalendo wetu JPM alishatufungua macho. Wakitaka mradi uendelee waje na masharti yatakayokuwa na manufaa kwa pande zote mbili. Hatupo tayari kuwauzia nchi. Kumchafua JPM hakusaidii.
Unaonaje nikikupuuza hasa baada ya kuonesha wazi ni namna gani ulivyo na upeo finyu?!
 
Jamaa ameongea kwa namna alivyoshiriki kwenye hizo Tafiti ameongea anachokijua hakusema ameona mkataba kilichotakiwa mnaopingana nae mje pingamizi zenu with evidence kumpinga bila Hoja ndio mkwere alisema msiipige RUNGU maana haitakufa isipokuwa Hoja itakufa kwa Hoja iliyobora zaidi so kwa mfano alichoandika jamaa hakitafutika kwa jazba kama anavyofanya mchangiaji mmoja humu....
hili jukwaa lilikuwa na mijadala ya maana watu walikuwa wanaArgue mtu anashindwa kwa Hoja sasa hii imekuja sasa watu kuporomosha matusi sidhani kama inatusaida kama Taifa

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
Hakuna evidence aliyokupa, soma vizuri amesema kwa taarifa zisizo rasmi... Na amesema siyo rasmi kwa kuwa alishindwa kupata taarifa rasmi. Tumia akili kibaraka wa beberu na Mchina wewe.
 
Back
Top Bottom