Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Jiwe alisaga akili za watu wengi hapa nawaza angekuwa hai mpaka amalize muda wake nakujiongezea sijui tungekuwa na Taifa la watu gani

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
Na wanasahau ni huyu huyu ndie alituambia serikali wenyewe tuna uwezo wa kujenga copper smelter inayohitajika na Acacia. Na watu tuliposema kwamba hizo ni porojo tu, misukule yake kama kawaida ikaishia kumwaga matusi tu!

Matokeo yake, hadi umauti umemkuta, hata "tofali" moja hawajajenga!
 
Wachina walivyo, kwenye hiyo $67 yake, atataka asikatwe income tax. Study ya Piraeus pia inaonesha China ilitaka isamehewe income tax, lakini hakuna taarifa za ndani kuangalia ni income tax ipi, kwa sababu bandarini kuna income generation sources nyingi!
Asante sana, Mkuu kwa maelezo yako.

Redbold: Ukosefu huu wa taarifa za ndani ndiyo unasababisha stofahamu kwenye mradi wa Bagamoyo. Kutegemea kuunganisha dots pekee kufanya majumuisho ya jumla ni kunaongeza urefu wa mjadala. Kwa sababu watu wengi wanao uwezo na mbinu za kuunganisha dots ili wafanye majumuhisho wanayoyataka. Nina imani tupo pamoja katika hili.

Jambo rahisi kabisa kupunguza urefu wa mjadala huu ilikuwa ni kuweka makubaliano kwenye suala/mradi hili/huu wazi. Hivi kitu chema kwa nini kifichwefichwe...! Najua itasemwa, kuweka wazi kila kitu kitasababisha 'insecurity of project integrity specifically kwenye techno-economic strategies '.Sisi hatuhitaji technical and economic aspects za mradi tunataka kujua 'legal bound agreement' ya namna gani tutanufaika kama taifa vile vile si vibaya kujua China atanufaikaje. Mbona kwenye madini nchi na Barrick mambo yako wazi kiasi? Huku kuna nini kiasi tunategemea kuunganisha dots badala ya kupata taarifa za ndani?

Mkuu nadhani sasa umeelewa 'wasiwasi' wangu.
 
Wanyonge wanatapatapa walishazoea propaganda.Zama za camera za show off zilishapita
 
Hakuna evidence aliyokupa, soma vizuri amesema kwa taarifa zisizo rasmi... Na amesema siyo rasmi kwa kuwa alishindwa kupata taarifa rasmi. Tumia akili kibaraka wa beberu na Mchina wewe.
Uelewa wako mdogo mno!!!

Kila taasisi ina wasemaje wake!! Kwahiyo taarifa ukipewa na asiye msemaji, hiyo inaitwa taarifa zisizo rasmi! Usidhani taarifa zisizo rasmi za bandari zinatolewa na makuli, au watu wasio kwenye system!!!

Secretary anaweza kukupa taarifa! Wakati mwingine anaweza kukuonesha hata doc, lakini asikuachie kama attachment yako!

Kwavile huwezi kuitumia kama supporting doc, na aliyekupa hana mamlaka ya kufanya hivyo! Hiyo inaitwa taarifa isiyo rasmi, na wala huwezi kutaja source ya taarifa hiyo!!!
 
SEHEMU YA PILI.

Hoja zinazotolewa na Wazalendo Kupinga Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.

Wachina Watachukua Mapato YOTE ya Bandari ya Bagamoyo.

Hii ni moja ya hoja zinazotolewa na Wazalendo wetu wanaopinga Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Bandari, Deusdedit Kakoko nae alipata kusema “…Wachina wanataka kuchukua mapato yote, na wanataka wasilipe kodi kwa miaka 30.”

Ukweli ni kwamba, haya ni madai ya kushangaza!

Ni madai ya kushangaza kwa sababu ni jambo lisiloingia akilini. Na ikitokea Wachina wakachukua MAPATO YOTE basi Tanzania tutaweka historia mpya duniani kwa sababu hakuna kitu kama hicho popote pale duniani!

Labda niseme jambo moja! Aya yangu hiyo hapo juu ni namna tu ya kusema kiungwana kwamba MADAI HAYO NI UONGO!

Kakoko kasema Wachina wanataka wasamehewe kodi kwa miaka 30! Hata hivyo, hatuambii ni kodi ya aina gani wanayotaka wasamehewe!

Kubwa zaidi, maelezo ya Kakoko yalikuwa yamekaa ki-propaganda mno… propaganda zile zile za ki-MATAGA za kujifanya wao ndo Wazalendo sana na wana uchungu sana na hii nchi wakati ni WANAFIKI tu, ambao “uzalendo” wao ulikuwa kwa JPM, na sio kwa nchi!

Ni kutokana na uongo huu wa Kakoko ndo maana haikushangaza kwa mara ya kwanza kuwaona Wachina wakioka mbele na kumshutumu Kakoko kwamba ni MWONGO.

Kwa mfano, gazeti la The Citizen la October 28, 2019 lilimnukuu Mwakilishi wa Uwekezaji wa China Merchant Group, Mr. Moosa Mao akisema:-


Na hata kupitia ukurasa wake wa Twitter, Mr. Mao aliandika:-

View attachment 1765244

China Merchant Group ndio walitarajiwa kuwekeza kwenye Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.

Hapa tuweke kumbukumbu sawa linapokuja suala la kodi kwa kuangalia muktadha wa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.

Katika hali ya kawaida, kutakuwa na awamu mbili zinazohusiana na kodi kwenye mradi huu.

Awamu ya kwanza ni wakati wa shughuli za ujenzi wa bandari, na awamu ya pili ni pale bandari itakapoanza kufanya kazi.

Wakati wa ujenzi, tunatarajia vifaa vingi vitaagizwa kutoka nje, ingawaje tutakuwa Viumbe wa Ajabu sana endapo tutaruhusu uingizaji hadi wa vifaa ambavyo wenyewe tunavyo, kama vile saruji.

Kuhusu hilo la vifaa, hapa Mchina namtarajia atakuwa ameomba asemehewe kodi ya uingizaji wa hivyo vifaa!

Na kwa bahati, hatakuwa amefanya dhambi yoyote kwa sababu Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, yaani VAT Sura ya 148, na Sheria ya Fedha ya mwaka 2017, 2018 na 2019 zinatoa mwanya kwa Mwekezaji kuomba msamaha wa kodi “on imported capital goods”.

Hata ukiingia kwenye tovuti kuu ya serikali utakuta maneno haya:-


Hivyo, hapo utaona wazi kwamba ni suala la kisheria! Na jambo kama hilo sio Tanzania tu bali sehemu mbalimbali duniani huwa wanafanya hivyo ili kuvutia uwekezaji!!

Kitaalamu, suala hilo linaitwa Tax Incentives. Na hata uki-Google “Tax Incentives in Tanzania”, moja kwa moja utakutana na link ya TRA ikiwa juu kabisa ya matokeo ya utafutaji; yaani Google Search Results!

Suala la kodi na ushuru bandari itakapoanza kufanya kazi.

Kama nilivyosema hapo awali, Mhandisi Kakoko alituambiwa “Wachina wanataka wasamehewe kodi kwa miaka 30,” huku Wazalendo wengine wakituambia TRA hawataruhusiwa hata kutia pua hapo bandarini!

Hapa ieleweke kwamba, popote pale duniani kodi ni MALI YA SERIKALI, na ndio maana, ukisoma hiyo screenshot ya Twitter kutoka kwa Moosa Mao, amekanusha suala la eti TRA hawataruhusikiwa kukusanya kodi!

Na ndio maana, wewe milikishwa ekari 1000 na baba yako, kisha tumia pesa zako mwenyewe kufanya uwekezaji bila kuomba hata senti moja kutoka popote pale!

Pamoja na yote hayo, ukimaliza tu uwezekaji wako na kuanza kufanya biashara, TRA wanakuwa wageni wako wa kudumu, ingawaje hukuchangiwa chochote na yeyote!

Lakini kwa upande mwingine, popote pale duniani, serikali huwa zinasamehe baadhi ya kodi. Bandari ya Bagamoyo ikishaanza kufanya kazi, tunatarajia kuwepo angalau kodi zifuatavyo:-

  • Kodi ya Ongezeko la Thamani… VAT on imported goods
  • Kodi ya Mapato (Income Tax)
  • Ushuru wa Uingizaji Bidhaa (Import Duty)
  • Ushuru wa Forodha, na zingine.
Sasa basi, tuseme wewe na mimi, or anyone ameagiza magari au bidhaa yoyote ambayo sio miongoni mwa bidhaa zilizo kwenye kundi la msamaha wa kodi!

Hilo likifanyika, Importer atalazimika kulipa angalau moja ya kodi nilizotaja hapo juu! Kodi hiyo ni LAZIMA IKUSANYWE NA TRA kwa sababu, kama nilivyosema awali, always, Kodi ni Mali ya Serikali.

Sasa je, kuna uwezekano Mchina akataka msamaha wa kodi baada ya bandari kufanya kazi?

Jibu ni NDIYO!

Kutokana na uzoefu niiopata kutoka kuwa Mbeba Mikoba wa Beberu, na kwa kuangalia “case studies” za bandari zingine ambako Mchina amewekeza, hapo kuna uwezekano mkubwa Mchina akaomba msamaha wa Income Tax. HOW?

Bandari ikishaanza kufanya kazi, Mchina atakuwa anatoa huduma kadhaa kama vile kuhifadhi mizigo, kupandisha na kupakuwa mizigo, kuzitoza meli ambazio zitakuwa zinafunga nanga hapo bandarini, n.k.

Kwa kutoa huduma hizo, ina maana Mchina atakuwa analipwa pesa!! Katika mazingira ya kawaida, pesa anazopata ni mapato yanayostahili kukatwa kodi!

Ni hiyo kodi itakayotokana na hizo huduma ndiyo ambayo sina shaka Mchina atataka asamehewe!! Na huu ndio ukweli ambao kwa makusudi, Mzalendo Kakoko hakutaka kusema ukweli, na badala yake akafanya majumuishi kwamba Mchina anataka kusamehewa kodi kwa miaka 30, bila kutaja ni kodi ipi!

Katika hili la kodi, nililazimika kumtumia email yule Researcher niliyekuwa nae, kwa sababu mimi binafsi sikupata fursa ya kuonana na watendaji wa serikali!

Nililazimika kumtumia email na kumuuliza ingawaje tayari nilishakuwa nafahamu majibu ya maswali yangu. Hata hivyo, nilitaka tu kujiriidhisha kutoka kwake, kwa sababu yeye ni mzoefu sana kwenye haya mambo ya uwekezaji duniani!

Jibu lake lilikuwa hili hapa chini:-

View attachment 1765245
Swali hilo nilimuuliza miaka 2 iliyopita, na mtaona jibu lake linaenda sawa na jibu la Moosa Mao!

Aidha, miongoni mwa maswali ambayo watu wamekuwa wakijiuliza ni kwamba: Sasa kama TRA watakuwa wanachukua kodi, Mchina atarudisha vipi pesa yake!

Jibu la hilo swali unatakiwa kujiuliza: Je, Mamlaka ya Bandari huwa wanakusanya kodi? Kama hawakusanyi, je mapato yao yanatoka wapi? Jibu la swali la pili ndilo jibu la swali la Mchina atarudisha vipi mapato yake!
tunashukuru had
UTANGULIZI

Amini usiamini, wale wale ambao wamekuwa wakijivika uzalendo, linapokuja suala la Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, ndiyo hao hao wanaotumikia Mabeberu bila wao kujijua!

Nitajadili mada hii katika sehemu mbili:-
  • Kwanini wale wanaoitwa Mabeberu hawawezi kuwa tayari kuona miradi kama ya Bandari ya Bagamoyo inafanikiwa, na
  • Hoja zinazotolewa na Wazalendo Kupinga Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.
Kwa bahati, binafsi mwaka 2016 nilikuwa “Mbeba Mikoba” wa Researcher mmoja wa Kimarekani (Beberu?) aliyekuwa anafanya utafiti kuhusu Belt and Road Initiative (BRI).

Kazi yangu kubwa ilikuwa Literature Review!

Kwa wanaofahamu mambo ya Resech, ukifanya Literature Reviews, hususani ya wasomi kama huyu bwana, basi unapata fursa ya kufahamu mambo mengi zaidi yaliyopata kutokea hapo kabla kwenye eneo husika!

Kwa wasiofahamu, Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni matokeo ya (BRI) ambayo, Rais wa China, Xi, anailezea BRI kwamba:


Kwa lugha nyepesi, malengo ya China kupitia BRI ni kuiunganisha nchi hiyo na sehemu zingine duniani, hususani Asia, Afrika, na Ulaya! Uunganishaji huo ni kwa ujenzi wa miundombinu, hususani ya bandari, reli, na viwanja vya ndege.

Ndugu yangu MALCOM LUMUMBA alipata kuchambua kwa undani kabisa suala la Belt and Road Initiative!!

Na hapo sidhani kama mtu anahitaji kuwa na Shahada ya Diplomasia ya Uchumi na Ushikirikiano wa Kimataifa kunusa “threat” ya mpango huo wa China kwa mataifa makubwa, hususani Marekani!

Kutokana na ukweli huo, ndo maana haishangazi mara tu BRI ilipotangazwa, Waandishi na Watafiti mbalimbali kutoka nchi za magharibi wakaanza kulivalia njuga suala hilo.

Makala zikaandikwa, na tafiti zikafanywa kuhusu BRI, lakini makala nyingi kama sio zote zililenga kuyatisha mataifa mengine kuwa makini na BRI!

Watu hawa wakageuka kuwa “Wajomba Zetu” Afrika, huku wakituasa tusije tukaingia kwenye mtego huo hatari wa China!

Ni kupitia hizo tafiti ndipo nami nikajikuta nipo na huyo Mtafiti Msomi kweli kweli wa Kimarekani.

Huyu Bwana case studies zake zilikuwa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, Bandari ya Hambantota (Sri-Lanka), pamoja na Bandari ya Piraeus (Ugiriki).

Ukweli ni kwamba, ilinichukua chini ya dakika 3 kugundua Mtafiti huyu ni kama tayari alishakuwa na “matokeo” ya utafiti wake hata kabla kazi haijaanza! Kwa kifupi, alionesha dalili zote za kutounga mkono Mradi wa Bandari ya Bagamoyo!

Hata "beberu" niliyekuwa namtumikia, nae alikuwa pamoja na "Wazalendo" wetu!!

Binafsi, nilikuwa “in favor of” Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, kwahiyo tukaanzisha kimdaharo kisicho rasmi!

Baada ya kuona hoja zake nyingi nazipangua, akaishia kuuliza ikiwa nadhani ni busara kwa taifa maskini kama Tanzania kuwa na bandari kubwa kama ya Bagamoyo!!

Jibu langu kwake lilikuwa rahisi sana, kwamba: Bandari ya Bagamoyo itakuwa ni kubwa mno kwa Tanzania endapo tu unaamini Tanzania na majirani zake wataendelea kuwa maskini kwa miongo kadhaa ijayo, vinginevyo, huwezi kusema ni “kubwa mno”!

Kwa ufupi, Mheshimiwa huyu, kama walivyokuwa wenzake wengine, nyimbo zao zilikuwa ni agenda ya siri ya China kuitumia BRI kama Mtego wa Madeni kwa nchi maskini!

Lilipokuja suala la Bandari ya Hambantota kule Sri-Lanka, propaganda zikasambazwa kwamba China IMEITWAA bandari ya Sri Lanka ili kufidia deni lake!

Wazalendo wetu nao wakazidaka propaganda hizo, na bila kufanya utafiti, wakaanza kutueleza kwamba “tukishindwa kulipa deni, Wachina wataichukua Bandari ya Bagamoyo kama walivyofanya kule Sri-Lanka.”

Kuweka kumbukumbu sawa, habari za Wachina KUITWAA bandari hiyo zilipotoshwa. Nitaeleza hili kinaga ubaga hapo baada kwenye makala hii.

Pamoja na suala la “Debt Trap”, watu hawa tunaowaita Mabeberu ambao kwa hili tunawaona wanajali maslahi yetu, pia wakawa wanatuambia agenda nyingine ya siri ya China ya kuanzisha “military base” kupitia BRI.

Hapa wakawa wanalenga kutuambia, hata mradi kama wa Bandari ya Bagamoyo, lengo lake ni Wachina kutaka kuweka kambi za kijeshi eneo hili la Afrika Mashariki!

Hata hivyo, hawatuambii ukweli kwamba, ni wao wenyewe ndio wanaozihofia hizo “military bases” za China endapo zitawepo!

Kila mfuatiliaji wa mambo duniani, anafahamu Marekani ina kambi za kijeshi sehemu kadhaa duniani, lakini linapokuja suala la China au mataifa mengine kufanya yale yale ambayo yeye keshayafanya kwa miongo kadhaa, hapo inageuka kuwa nongwa!

Waingereza wana msemo “If you can’t beat them, join them.”

Guys, amini usiamini, juzi yule Mtafiti niliyekuwa nae ametoa makala kwenye moja ya majarida maarufu sana duniani! Baada ya kuisoma makala ile, hapo hapo nikajisikia uchungu, na kumhurumia!

Yaani yule yule aliyekuwa anaipinga BRI, kwenye hiyo makala anaulaumu wazi wazi Utawala wa Trump kwa kutumia kete ya Debt Trap kama njia ya kuidhoofisha BRI.

Kwenye makala hiyo, kuna sehemu anahoji “Kama kweli BRI ni kitu kibaya kiasi hicho, ni kwanini basi China inaendelea kutafuta Washirika walio tayari kujiunga na BRI.”

Mwishowe, Mtafiti huyu anaisemanga serikali yake kwamba ”USA haitaweza kumzuia Rais wa China kuwekeza kupitia BRI endapo US haitakuwa na mbadala kwa mataifa yanayoshirikiana na China!

Ufaransa, imeanza kuliona hilo kama ilivyowahi kuripotiwa na France24 kwamba:


Desperation ya Mtafiti huyu bila shaka inatokana na vile anavyoona jinsi ambavyo nchi mbalimbali duniani jzinavyojiunga na BRI, kinyume na matarajio ya USA ambayo ilikuwa ina-lobby nchi zingine, hususani Washirika wake kutojiunga na BRI.

Kwa bahati mbaya sana, si Afrika, si Asia! Hadi baadhi ya nchi za Ulaya na Carribean zinaingia kwenye BRI. Mbaya zaidi, miradi ya BRI inaonekana kufanya vizuri sana!

Kwa mfano, mwaka 2016 Bandari ya Piraeus ilikuwa ndio ya kwanza barani Ulaya kubinafsishwa chini ya BRI. Bandari hii ndiyo bandari kubwa kuliko zote nchini Ugiriki, na ndio langu kuu la bahari linalounganisha nchi za EU na Asia!

Hapo kabla, bandari hii ilikuwa haifanyi vizuri, na ripoti za nyuma zilikuwa zinaiweka bandari hiyo kama bandari ya 17 barani Ulaya!

Baada ya Wachina kuchukua 51% ya hisa za bandari hiyo, na hatimae hisa hizo kufikia 67%; ripoti ya mwaka huu kupitia Port Economics inasema kwa sasa Bandari ya Piraeus ndiyo bandari kubwa zaidi (kwa kiwango cha makontena) kwenye ukanda wa Bahari ya Mediterranean, na ya 5 Barani Ulaya!!

Sasa haya ndo mambo ambayo watu hawakuyataka! Yaani bandari iliyo kwenye ardhi ya Mzungu, 67% imilikiwe na Mchina, na hapo hapo inaanza kutishia ushawishi wa bandari zingine zinazomilikiwa na Wazungu wenyewe!

JokaKuu
Tunashukuru kwa hadithi yako nzuri tu
Sasa ili mradi wa Bandari ufanikiwe ni lazima I mizigo iwepo ya kutosha, je kwa ilivyo tunayo mizigo kiasi hicho kihalali uwepo wa Bandari ya Bagamoyo wawekezaji ni hapa naona tunataka kuleta hadithi ua yai ns kuku mama alianza
Pili tuna Bandari tatu ya Mtwara Dar na Tanga, je hizo hazitoshi

Tatu kama hizo 4th generation ships haiwezi kuingia Bandari tulizo nazo , kwanini hiyo Bandari ya Bagamoyo tusijenge in phases mfano ghati number moja kwanza n.k
 
Kwavile huwezi kuitumia kama supporting doc, na aliyekupa hana mamlaka ya kufanya hivyo! Hiyo inaitwa taarifa isiyo rasmi, na wala huwezi kutaja source ya taarifa hiyo!!
Labda kwenye counter-intel na mambo mengine kama hayo mbinu hii inaweza kufaa kwa sababu nidhamu ya uaminifu ni kubwa kwa wahusika. Lakini, kwenye 'public hearing' ambapo watu wanataka kushinda 'political trust' kwa wananchi, mbinu hii inaweza kutumika kama kichaka cha kusukuma ajenda ambazo zaweza kuwa na 'ill au healthy motive'. Sasa kuepusha mkanganyiko, mambo yawekwe wazi.

Kumbuka kwa namna yoyote ile sipingi jambo lolote litakalowezesha Tanzania kustawi katika nyanja zote lakini ikiwa imekita mizizi yake katika kujitegemea ki-kweli kweli.
 
HITIMISHO

Tukubali tusikubali, fursa ya Bandari ya Bagamoyo ikituponyoka tutakuja kuijutia pale Mchina atakapoamua kurejea tena Lamu, au popote pale kwenye ukanda huu wa Bahari ya Hindi!

Inashangaza sana karne ya 21 bado kuna Watanzania wana mawazo yale yale ya Ujima kwamba, eti “madini hayaozi”, na tutakuja kuchimba wenyewe tukishapata uwezo!

Injinia Kakoko na mwenyewe aliwahi kunukuliwa akisema “…na sisi bandari ile (Bagamoyo), tulifanya feasibility study na TPA. Na TPA kupitia serikali, itawekeza na kuijenga wakati utakapokuwa umefika.

Ni wazo zuri kama serikali itakuwa na uwezo wa kujenga hiyo bandari wao wenyewe haidhuru hata kama tumeshindwa kujenga bandari yoyote ndani ya miaka 60 ya uhuru!

Hata hivyo, Kakoko na wengine wanatakiwa kufahamu kwamba, hoja sio kuwa na uwezo wa kujenga bandari bali uwezo wa ku-utilize bandari husika!

Nimetoa mfano wa Bandari ya Piraeus huko Ugiriki ambayo kabla ya uwekezaji wa China, bandari hiyo ilikuwa haifanyi vizuri. Hata hivyo, baada ya Mchina kuingia, Bandari ya Piraeus imegeuka na kuwa ndiyo bandari kubwa kuliko zote Ukanda wa Mediterranean, huku ikichukua nafasi ya 5 Barani Ulaya!

Na ndivyo hivyo kwa Bandari ya Hambantota ambayo na yenyewe ilikuwa haifanyi vizuri lakini hivi sasa hali imebadilika.

Na sababu kubwa ya China kuwa na uwezo wa kuzifanya bandari anazoendesha kufanya vizuri inatokana na ukweli kwamba China ina-handle biashara kubwa sana duniani. Kwa maana nyingine, China ina uwezo wa ku-utilize bandari zake kupitia mizigo yake tu.

Lakini kwa upande mwingine, Mradi wa Bandari ya Bagamoyo pia unahusisha Industrial Complex kubwa sana! Lengo la Mchina ilikuwa ni kujenga viwanda kwenye eneo la bandari, ili baadhi ya bidhaa zake anazosafirisha kutoka China hadi Afrika ziwe zinazalishwa Bagamoyo.

Ninachotaka kusema ni kwamba, pamoja na suala la kodi, mradi huu endapo ungekamilika, ungekuwa chanzo kikubwa cha ajira kwa wananchi!

Bandari ya Bagamoyo sio kama Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chato! Hivyo basi, hata kama tuseme Mzee wa Msoga alilenga kupendelea kwao, hivi kuna mwenye akili timamu anayeweza kuthubutu na kudai kwamba, watakaofaidika na bandari hiyo ni Wakwere na Wazaramo wa Bagamoyo?

Halafu hii nchi ilivyo na viumbe wa ajabu, hao hao wanaosema JK alikuwa anataka kupendelea kwao, kwa kiasi kikubwa ndo hao hao wanaodharau watu wa Pwani kwamba HAWAJASOMA, na kwamba wanaishia kuendekeza madrasa!

Sasa kwavile nyie ndio mliosoma, hamuoni kwamba ni nyinyi wenyewe ndio mtakaofadika na mradi huo huku Wakwere na Wazaramo wakiishia kuwauzia kahawa?

Ukubwa wa mradi ule unaweza kuzalisha Pay As You Earn (PAYE) kutoka kwa wafanyakazi ambayo ni kubwa kuzidi hata thamani ya ukodishaji wa ardhi!

Na hii PAYE ni endelevu kwa miaka na dahari!

Pamoja na yote hayo, katu simaanishi kwamba Mkataba wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo upo PERFECT, au ni mkataba bora… la hasha!! Tanzania haijawahi kusaini mkataba ulio bora!

Ambacho ningependa kukiona kwenye hili ni Watendaji na Wafanya Maamuzi kuwa “objective”, na pia waache kusambaza habari za uongo ili mradi tu kuhalalisha ajenda zao.

Wengine ajenda zao ni aibu hata kuzitaja hadharani!

Watu hawa wanatakiwa kukaa na wadau, na kuangalia ni kwa namna gani huu mradi unaweza kufanyika huku tukiacha kile kiburi chetu cha Uzalendo Fake Uliopandikizwa na Mfumo wa Ujamaa!

Aidha, wanatakiwa kukaa na wadau kuangalia ni mfumo upi utaweka mbele maslahi mapana ya taifa.

Na kama nilivyosema kwenye utangulizi wangu, Wapinzani wa Bandari ya Bagamoyo wanawatumikia wale wale wanaowaita Mabeberu bila wao kujijua! Mabeberu walianza kuipinga Belt and Road Initiative ya China tangu kuanzishwa kwake!

Kwa bahati mbaya sana, hao hao waliokuwa wanapinga BRI, hivi sasa wanaanza kuingia mmoja mmoja! Kuna dalili zote kwamba Marekani imeanza kusalitiwa na Washirika wake, hata wale wa Jumuiya ya Ulaya.

Kwa mfano, Jarida la The Diplomat la March 23, 2021 linatueleza kwamba:-


Aidha, wakati Marekani ikihangaika na BRI, mwaka juzi tu hapa, huko China ulifanyika mkutano mkuuubwa wa BRI kama ilivyoripotiwa na UNDP-Asia kwamba:-



Na kwa mujibu wa Serikali ya China, kupitia Belt and Road Portal, wanasema kwamba:-

Mzee wa Msoga aliwahi kutujuza kwamba: Akili za Kuambiwa, Changanya na Zako!
Ila sie Afrika tusifanye miradi kwa sababu mchina kasema hv,au mzungu beberu kasema hv,na sie si tuna akili,tukune bongo,tutumie think tanks wetu ambao hawajawa compromised,maana nchi hii watu wananunuliwa kirahisi kweli,kwa kujengewa vyoo kwenye majimbo yao.
Ila huyu mchina unayemsifia ana tofauti na mchina aliyepo pale Urafiki Textile?
Maana wabongo wanaofanya kazi pale ni kama wapo utumwani,kuna umaskini wa kutisha,na kila spea mpaka fagio za chooni zinatoka China!!
 
Uelewa wako mdogo mno!!!

Kila taasisi ina wasemaje wake!! Kwahiyo taarifa ukipewa na asiye msemaji, hiyo inaitwa taarifa zisizo rasmi! Usidhani taarifa zisizo rasmi za bandari zinatolewa na makuli, au watu wasio kwenye system!!!

Secretary anaweza kukupa taarifa! Wakati mwingine anaweza kukuonesha hata doc, lakini asikuachie kama attachment yako!

Kwavile huwezi kuitumia kama supporting doc, na aliyekupa hana mamlaka ya kufanya hivyo! Hiyo inaitwa taarifa isiyo rasmi, na wala huwezi kutaja source ya taarifa hiyo!!!
And so hauwezi kutupa evidence... Hiyo haina tofauti na stori za vijiweni. Una shida gani kibaraka?
 
Tunashukuru kwa hadithi yako nzuri tu
Sasa ili mradi wa Bandari ufanikiwe ni lazima I mizigo iwepo ya kutosha, je kwa ilivyo tunayo mizigo kiasi hicho kihalali uwepo wa Bandari ya Bagamoyo wawekezaji ni hapa naona tunataka kuleta hadithi ua yai ns kuku mama alianza
Pili tuna Bandari tatu ya Mtwara Dar na Tanga, je hizo hazitoshi
Mkuu nadhani haya mambo ameyafafanua. Wachina watakuja kujenga viwanda kwa ajili ya bidhaa zao hapo Bagamoyo....Sina hakika kama mizigo yetu pia itakuwa inapita hapo!
 
Asante sana, Mkuu kwa maelezo yako.

Redbold: Ukosefu huu wa taarifa za ndani ndiyo unasababisha stofahamu kwenye mradi wa Bagamoyo. Kutegemea kuunganisha dots pekee kufanya majumuisho ya jumla ni kunaongeza urefu wa mjadala. Kwa sababu watu wengi wanao uwezo na mbinu za kuunganisha dots ili wafanye majumuhisho wanayoyataka. Nina imani tupo pamoja katika hili.
Man, haya mambo mnayakuza bure tu, na matokeo yake mnashindwa kuweka productive inputs!!! Hili taifa tayari lina sheria zake!!! Sheria zetu tayari zinataja ni kodi zipi huwa zina msamaha!!

Sihitaji kuona mkataba kutetea hoja kwamba, kodi zinazosemwa kutaka msamaha haziwezi kuwa kodi za uagizaji bidhaa, kama vile VAT on imported goods!!!

VAT always husamehewa kwenye imported capital goods!!

HAIWEZEKANI eti wewe uagize gari, halafu VAT achukue Mchina... hakuna kitu kama hicho!!

Ukiona umeagiza bidhaa, halafu hulipii VAT serikalini basi fahamu bidhaa hiyo tayari ipo kwenye kundi la bidhaa zinazosamehewa VAT!

Ingawaje kwa makusudi tu Kakoko hakusema ni kodi ipi, lakini nina uhakika mkubwa kwamba kodi kubwa kabisa anayoisema ni income tax!!!

Na income tax husamehewa ili kutompungumzia mwekezaji mapato yake anayopata kupitia dividends, cargo and ships handling, warehousing, n.k!

Huko kote Mwekezaji huwa anaingiza pesa ambazo kimsingi zinatakiwa zikatwe income tax!! Lakini Bakhresa kaingiza scania 200, halafu VAT on imported Scanias iende kwa Mchina? Hakuna kitu kama hicho!

Na usisahau, hii ni research iliyoongozwa na mtu mwenye uzoefu na miradi ya China Ulaya, Asia, na Afrika, kwahiyo anaongea kitu alicho na uzoefu nacho!!

Na hata anaposema "taarifa isiyo" rasmi, haina maana kwamba ni taarifa isiyo sahihi!

Aidha, nikipata wasaa, nitatafuta PR ya Mwakilishi wa China Merchant Group, ambae kwa kujiamini kabisa, alisema wazi wazi kwamba Kakoko ni muongo, na wala hakuwepo siku ya majadiliano!!!

Mbona Kakoko hakujitokeza tena mbele kupinga madai ya Mr. Moosa Mao?
Jambo rahisi kabisa kupunguza urefu wa mjadala huu ilikuwa ni kuweka makubaliano kwenye suala/mradi hili/huu wazi. Hivi kitu chema kwa nini kifichwefichwe...! Najua itasemwa, kuweka wazi kila kitu kitasababisha 'insecurity of project integrity specifically kwenye techno-economic strategies '.Sisi hatuhitaji technical and economic aspects za mradi tunataka kujua 'legal bound agreement' ya namna gani tutanufaika kama taifa vile vile si vibaya kujua China atanufaikaje. Mbona kwenye madini nchi na Barrick mambo yako wazi kiasi? Huku kuna nini kiasi tunategemea kuunganisha dots badala ya kupata taarifa za ndani?

Mkuu nadhani sasa umeelewa 'wasiwasi' wangu.
Kwa bahati mbaya sana, HILO HALITAKUJA KUTOKEA... anyway, labda kwavile kuna utawala mwingine! Usisahau suala la mikataba kuwekwa wazi kimekuwa ndio kilio cha muda mrefu cha Wabunge, manake hata wenyewe wanashindwa kupewa hii mikataba!!
 
Ila sie Afrika tusifanye miradi kwa sababu mchina kasema hv,au mzungu beberu kasema hv,na sie si tuna akili,tukune bongo,tutumie think tanks wetu ambao hawajawa compromised,maana nchi hii watu wananunuliwa kirahisi kweli,kwa kujengewa vyoo kwenye majimbo yao.
Ila huyu mchina unayemsifia ana tofauti na mchina aliyepo pale Urafiki Textile?
Maana wabongo wanaofanya kazi pale ni kama wapo utumwani,kuna umaskini wa kutisha,na kila spea mpaka fagio za chooni zinatoka China!!
Ni wapi hapo nilipomsifia?! Na kama nimemsifia, hizo sifa ni sifa fake, au?!

Hivi kusema Bandari zinazoendeshwa na Mchina huwa zinafanya vizuri kwa sababu ana advantage ya ku-handle percent kubwa ya shehena inayopita baharini, hiyo ni kumsifia au ndo ukweli wenyewe?!

Au kuna mahali nimesema Mchina ni mtu mzuri kweli kweli?!
 
Ni ujinga kusifia uzuri wa matokeo ya mradi badala ya ubora wa Mkataba!!
 
Huu mradi Mkataba wake utakapokuwa wazi bila udanganyifu kabisa, tutataka uchunguzi wa Hizi kelele nyingi kutoka Kwa Watanzania hawa,

Watu wako tayari kutuonyesha uzuri wa mradi na manufaa yake, lakini hawako tayari kabisa kuzungumzia Mkataba na masharti yake, unajiuliza ni Kwa nini?

Spika naye, badala ya kuanza na Mkataba mle bungeni, anaanza kutuonyesha utamu wa mf wa Bandari iliyoko China yenye mfano kama hii itayojengwa Bagamoyo na jinsi itakavyoinufaisha nchi, ni Jambo jema, lakini Kwa nini asianze na kiini??

Maana mradi haujijengi wenyewe, na kama ni hivyo, tunataka sasa Mkataba utakoingiwa Kwa makubaliano basi!!!

Uzuri na manufaa ya mradi yananafasi ya pili baada ya Jambo mhimu ambalo ni Mkataba na masharti yake,

Spika ni clueless kabisa, haya ni maoni binafsi. Naamini hajui pa kusimamia na ni mtu wa kuendeshwa tu asiyejua uzito wa nafasi yake.

Najiuliza hivi contents za mkataba yeye hana? Kwamba hajui vipengele vya hiyo mikataba hadi kusema walishauriwa vibaya, kwamba baada tu ya JPM kufariki ndio wamepata clue ya nini kilichojiri wakati ule! Ni watu wajinga tu ndio watawaamini watu wa nature ya Ndugai.
 
Kama hakushiriki katika kusaini na haui kilichokuwemo kwanini anashikia bango jambo asililolijua?

Aliyesaini mkataba huo ni Dr Mary Nagu (Waziri Uwekezaji na Uwezeshaji) mbele ya Rais wa Tanzania J Kikwete na Rais wa China Xi Jinping mwaka 2013.

Acheni kupigia chapuo suala la msingi kama hilo ambalo undani wake hauelewi kinagaubaga
Ikiwa inajulikana NAGU na JK ndio wenye majibu inakuwaje wadau wanataka mleta mada ndio awaoneshe mkataba at

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
tunashukuru had

Tunashukuru kwa hadithi yako nzuri tu
Unajua nini?

I can understand you guys... thread yangu ni ndefu mno, na wengi wenu mmeshindwa kuisoma yote!!! Maswali uliyouliza nimeshayadili tayari!!!

Lakini kwavile I usually respect anayetoa hoja, tofauti na wale wengine wanaokuja hapa na kuanza matusi, bila kuzungumzia hoja yoyote, wacha niseme kwa uchache!
Sasa ili mradi wa Bandari ufanikiwe ni lazima I mizigo iwepo ya kutosha, je kwa ilivyo tunayo mizigo kiasi hicho kihalali uwepo wa Bandari ya Bagamoyo wawekezaji ni hapa naona tunataka kuleta hadithi ua yai ns kuku mama alianza
Nimeshasema plan ilikuwa kuifanya bandari kuwa transshipment port, na pili, ku-handle cargo itakayotokana na Industrial Complex.

We all know kwamba bidhaa za China ndizo zimesambaa kila kona Afrika kama sio duniani. Sasa kwa mfano, ukiona meli inatoka US kufuata mzigo China, usidhani zote zinafika China bali zinaishia Singapore ambayo ndiyo largest transshipment port!

Kinachotokea ni kwamba, mega ships kutoka Mashariki ya Mbali zinapakia mzigo China, Korea Kusini na Japan hadi Singapore ambako mzigo utapakuliwa na kuingizwa kwenye meli zingine kutoka sehemu mbalimbali duniani!!

Lengo la Bagamoyo, ilikuwa ndio hilo! Kwamba, badala ya meli kutoka SA, Mozambique, Kenya na sehemu zingine Afrika kwenda hadi Singapore au China, meli hizo zitafuta mzigo Bagamoyo unaoshushwa na meli kubwa kutoka Uchina!!

Lakini hata suala la transshipment lisipoanza mapema, bado tukumbuke bidhaa nyingi zinazoingia Afrika Mashariki na Kati, pamoja na Ukanda wa Maziwa Makuu zinatoka China!

Ni kutokana na hilo ndo maana mradi wa bandari ulikuwa uende sambasamba na ujenzi wa SGR ambao ingeiunganisha Bagamoyo, na zingine! Which means, mizigo ya China inayotoka China kuingia ukanda wetu, yote ingeshushwa Bagamoyo, na kutokea hapo ingesambazwa kwa njia ya reli kwenda nchi mbalimbali!

Lakini kwa upande mwingine, mradi pia ilikuwa uende sambasamba na ujenzi wa industrial complex kubwa sana. Kama plan ingeenda kama ilivyotarajiwa, ile complex ingezalisha bidhaa nyingi sana ambazo zingine zingesafirishwa kwa meli for export!
Pili tuna Bandari tatu ya Mtwara Dar na Tanga, je hizo hazitoshi
Nimeshasema, Mtwara ipo reserved for gas tankers, Tanga kuna miradi miwili. Je, HAZITOSHI?

Kwavile nimeshataja Tanga na Mtwara, swali liwe je, Dar haitoshi?!

Ngoja nikuulize: Tanzania ni maskini! Malawi ni Maskini! Rwanda, Burundi na Uganda ni maskini! In short, nchi zote zinazotumia bandari ya Dar es salaam ni maskini!

Pamoja na umaskini wetu huo, lakini bado bandari ya Dar wakati mwingine huelemewa! Sasa jiulize, endapo uchumi wa nchi unafikia angalau kama tu ule wa South Africa ambayo na yenyewe ni maskini; je unaamini Bandari ya Dar itaweza ku-handle uchumi kama huo?

REMEMBER... uchumi wa nchi hizi ukikua, utachochea more imports and exports! That being said, kama tunataka kuangalia miaka 50 ijayo, au angalau 25, I can confidently say HAZITOSHI!
Tatu kama hizo 4th generation ships haiwezi kuingia Bandari tulizo nazo , kwanini hiyo Bandari ya Bagamoyo tusijenge in phases mfano ghati number moja kwanza n.k
Sijakuelewa! Halafu tukishajenga in phase ndo inakuaje?! Kwamba ili tuijenge wenyewe, au?! Kama ndiyo, rudia swali lako la kwanza, kwamba, je, tutaweza kui-utilize?

Kumbuka, Mchina tayari ana mzigo unaosubiri kwenda sehemu mbalimbali duniani!! So, kama nasi tutakuwa na assurance ya mzigo, kujenga wenyewe itakuwa ni jambo bora lakini Sri Lanka walishindwa kui-utilize bandari yao, na hata Piraeus ya Ugiriki ilianza kupata mzigo wa kutosha baada ya kuingia Mchina!
 
Hakuna evidence aliyokupa, soma vizuri amesema kwa taarifa zisizo rasmi... Na amesema siyo rasmi kwa kuwa alishindwa kupata taarifa rasmi. Tumia akili kibaraka wa beberu na Mchina wewe.
Kwa comment hii tu ndio imeua Hoja ya jamaa asee watz nani kawaroga? hebu tuwekee hapa Mkataba wa Uwanja wa Chato ununuzi wa ndege

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom