Mabenki na mikopo ya biashara kwa graduates

Mabenki na mikopo ya biashara kwa graduates

Mkuu benki haiwezi kukubali ACADEMI CERTIFICATE per see

Ila serikali kama ina nia ya dhati inaweza kushirikiana na hawa graduates kwenye kukopa, soma vizuri post ya entreprenuer

All in all mtoa hoja ana point muhimu sana..try to get him

Kitu kingine kinachoweza kufanyika ni kushusha riba ambayo bado iko juu sana ukilinganisha na nchi za wenzetu. Katika baadhi ya nchi za wenzetu kama credit record yako ni nzuri katika kulipa bills zako basi unaweza kupata mkopo kwa bei poa sana. Kwa mfano sasa hivi katika baadhi ya nchi unaweza kukopa kwa riba ya 2% na kutakiwa kurudisha ndani ya miezi 24 ila kama unataka kulipa kwa muda mrefu zaidi basi riba itaongezeka kidogo. Mikopo kama hii ingekuwepo nchini ingesaidia sana katika kunyanyua viwango vya maisha ya wengi na pia kusaidia kuinua uchumi ulioanguka.
 
Tatizo lako moja tu Mkuu! Wewe unaangalia upande mmoja tu, wa mabenki!!! Kama umepitia vizuri thread yangu, ungegundua lengo hapo ni pawe na partneship kati ya mabenki na serikali. Serikali ina wajibu wa ku-create ajira, hivyo inatakiwa i-play role yake hapo including kuwa guarantor!

Na ndio maana nikasema, "mabenki kwa kushirikiana na serikali"!! Simaanishi, kesho Standard Chartered waamke na kwenda kwenye media na kutangaza kwamba graduates wanaweza kwenda kukopa kwa ku2mia certificates zao kama security!!!! Lazima pawe na institutional and structural change, as well enforcement! Mbona hutaki kuelewa mkuu?! yale mabilioni ya JK yalikuwa na dhamana gani?!

Sehemu ambayo mimi nilikuwa nafanyia, mikopo ile ilikuwa recovered kwa asilimia kubwa sana!!! Tena ile mikopo ilikuwa too poloitical.....unakuta mbunge au mkuu wa wilaya anakuja na watu wake pale analazimisha wapewe mikopo. Sehemu ambapo taratibu za utoaji wa mikopo ile zilifuatwa, program ilikuwa succesful.

Kilichokuwa kinatakiwa ni mtu kuonesha ana uwezo wa kufanya biashara au tayari ana biashara lakini tatizo ni security! Sehemu ambako ili-fail si kwa sababu wakopaji hawakuwa na security, bali siasa ilitawala zaidi na kushindwa kuangalia biashara ya mkopaji!

Sasa, ikiwa kwa watu kama wale ambao hata elimu ya kutosha iliwezekana, itashindikana nini kwa msomi kama wewe?! Wewe ukipewa 20m na ukashindwa kurudisha si kwa sababu umeweka dhamana ya cheti, bali hata ungeweka ghorofa, ungesumbua tu.

You are such amazing!

Kitu kingine kinachoweza kufanyika ni kushusha riba ambayo bado iko juu sana ukilinganisha na nchi za wenzetu. Katika baadhi ya nchi za wenzetu kama credit record yako ni nzuri katika kulipa bills zako basi unaweza kupata mkopo kwa bei poa sana.

Kwa mfano sasa hivi katika baadhi ya nchi unaweza kukopa kwa riba ya 2% na kutakiwa kurudisha ndani ya miezi 24 ila kama unataka kulipa kwa muda mrefu zaidi basi riba itaongezeka kidogo.

Mikopo kama hii ingekuwepo nchini ingesaidia sana katika kunyanyua viwango vya maisha ya wengi na pia kusaidia kuinua uchumi ulioanguka.

Spendi BAK.....unajua benk zetu kama vile maadui vile...yaani ni mafisadi wengine
 
Sijapata muda wa kusoma hii thread lakini SUA kuna kitu kama hiki kinaendelea, na kipo katika hatua za mwisho waweze kupatikana beneficiaries wa kwanza, original academic certificate ndo imetumika kama collateral, wana waregards graduates kama SME so wana umezo wa kukopeshwa kuanzia mil 20 - mil 300..,

Mkuu, haya mambo ni possible kabisa sema tunayakuza kwamba hayawezekani!! tatizo watu wanaangalia upande mmoja wa shilingi! Nakumbuka nili-introduce hii idea kwa baadhi ya graduate wa SUA about 7 years ago coz' nami nilimaliza pale some years back. Inawezekana mmoja wao nae akaipeleka mezani na wasioamini ktk kushindikana wamekata shauri la ku-put into practice!
 
mkuu, mboa unachekesha

neno dhamana unalirudia rudia katika mada yako lakini nahisi unaficha maana yake halisi, je Academic certificate ina actual value?nini maana ya asset, nini maana ya security?je mkopaji aki default how can you recover the liability from an Academic certificate?, mkuu kumbuka original academic certificate is not an issue, a CV sells the job seeker that means unaweza kuajiriwa mahali popote pasipo hitaji ku verify originals plus most important in recruitment is capability in job responsibilities

mkuu mbona hayo mavyeti nimefungia kabatini miaka mingi tuu, wala siyatumii hayo mavyeti, tena kama unavitaka njoo nikupatie ukakope benki na ni vyeti viwili vya first degree na post graduate dip, well nilitumia just once nikajiriwa tena sikupeleka orginal na ni ilikuwa foreign company, kwa sasa ninajiajiri, k

we have to value what we have from our education and use it to empower ourself

mkuu naona unataka kuongeza wingi wa defrauders tena graduate

haya ni mawazo yangu binafsi

Nakuunga mkono 100%! Thamani ya cheti (karatasi) ni ZERO, thamani ipo kwenye elimu uliyoipata, elimu haiwezi kuhamishwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Mleta mada amekosea kwenye "utafiti" wake, ameangalia mwuzaji anataka 50 million kuuza cheti ila mteja yuko teyari kulipia kiasi gani? Mtu akinipa cheti chake hata bure sichukui, hakina maana kwangu.

Zaidi ya hapo practically haileti sense kabisa, nikikupa cheti changu kesho naweza kuingia website ya chuo nikaprint kingine.

Kama Watanzania tunataka uwezo wa kuchukua mikopo kirahisi zaidi tuahitaji credit rating system na tracking ya wananchi, kwa mfano Marekani kila mwananchi ana Social Security Number na namba hiyo unakuwa nayo tangu uzaliwe hadi kifo, pia namba hiyo iko linked na credit rating yako, credit rating ndo inamjulisha mkopeshaji kama unakopesheka so kwa mfano usipolipa madeni yako credit rating inashuka.

Kuingia mitini baada ya kupata mkopo ni kitu kigumu sana, maana hauwezi kurent nyumba, kununua gari, na hata siku hizi kupata kazi kabla ya watu hawajaangalia credit rating yako.
 
Kitu kingine kinachoweza kufanyika ni kushusha riba ambayo bado iko juu sana ukilinganisha na nchi za wenzetu. Katika baadhi ya nchi za wenzetu kama credit record yako ni nzuri katika kulipa bills zako basi unaweza kupata mkopo kwa bei poa sana.

Kwa mfano sasa hivi katika baadhi ya nchi unaweza kukopa kwa riba ya 2% na kutakiwa kurudisha ndani ya miezi 24 ila kama unataka kulipa kwa muda mrefu zaidi basi riba itaongezeka kidogo.

Mikopo kama hii ingekuwepo nchini ingesaidia sana katika kunyanyua viwango vya maisha ya wengi na pia kusaidia kuinua uchumi ulioanguka.
Upo mpango wa kuanzisha database ambayo itakuwa na record za watu mbalimbali ambazo zitakuwa zinatumiwa na commercial banks ku-evaluate credibility ya mkopaji...

Sijui kwa sasa mpamgo wenyewe umefikia wapi!!! Hata hivyo, kwa kiasi kikubwa, nahisi hapa itatumika sana kuangalia kama unafaa kuaminiwa kupewa loan au hapana kwa kuangalia hiyo history. Suala la riba, hilo kweli ni tatizo kwani kinachotokea ni kwamba wanalipia defaulters....!!!
 
Nakuunga mkono 100%! Thamani ya cheti (karatasi) ni ZERO, thamani ipo kwenye elimu uliyoipata, elimu haiwezi kuhamishwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Mleta mada amekosea kwenye "utafiti" wake, ameangalia mwuzaji anataka 50 million kuuza cheti ila mteja yuko teyari kulipia kiasi gani? Mtu akinipa cheti chake hata bure sichukui, hakina maana kwangu.

Zaidi ya hapo practically haileti sense kabisa, nikikupa cheti changu kesho naweza kuingia website ya chuo nikaprint kingine.

Kama Watanzania tunataka uwezo wa kuchukua mikopo kirahisi zaidi tuahitaji credit rating system na tracking ya wananchi, kwa mfano Marekani kila mwananchi ana Social Security Number na namba hiyo unakuwa nayo tangu uzaliwe hadi kifo, pia namba hiyo iko linked na credit rating yako, credit rating ndo inamjulisha mkopeshaji kama unakopesheka so kwa mfano usipolipa madeni yako credit rating inashuka.

Kuingia mitini baada ya kupata mkopo ni kitu kigumu sana, maana hauwezi kurent nyumba, kununua gari, na hata siku hizi kupata kazi kabla ya watu hawajaangalia credit rating yako.

Nazani hujapitia post zote, na hili ndilo tatizo la JF! Unaweza kukuta thread imechangiwa kwa posts kama mia moja hivi, lakini utakuta karibu nusu yake zinaibua ki2 ambacho kilishaongelewa!
 
Nazani hujapitia post zote, na hili ndilo tatizo la JF! Unaweza kukuta thread imechangiwa kwa posts kama mia moja hivi, lakini utakuta karibu nusu yake zinaibua ki2 ambacho kilishaongelewa!

Nimepita post zote mkuu, naona baada ya kuona idea yako haiko feasible unaanza kuongelea in generalities, serikali ishirikiane na wahitimu na mabenki, hakuna kitu concrete unachokisema.

Kwenye post yako ya kwanza umesisitiza kuwa kutumia Academic Certificate kama DHAMANA inawezekana, hili haliwezekani kwa sababu Academic Certificate haina thamani inayohamishika, ina thamani kwa yule aliyeipata tu, na hata kwa yule aliyeipata sio rahisi kumpokonya ukilichukua karatasi ukalifungia benki unakuwa haujafanya lolote, hakuna motivation ya kwenda kuikomboa.

Kwa hiyo Certificate kama dhamana inafeli kwa pande zote mbili, benki haiwezi kuiuza ikarecover mkopo, na haiimpi mkopaji incentive ya kulipa deni.

Nia ya kuwawezesha watu wengi zaidi kukopa ni nzuri lakini ina hatari kubwa sana pale unapoanza kulegeza requirements, ndo moja ya sababu ya kilichotokea Marekani, serikali ilipitisha sheria ambayo ilikusudia kuwawezesha watu ambao wana credit rating mbovu (hawakopesheki) kuweza kupata mikopo ya nyumba, kumbe walikuwa hawakopesheki kwa sababu nzuri tu, mwishoni wengi wao wakashindwa kulipa.
 
Mkuu, sawa "umepitia" post zote! The question follow, uli-take time kuzi-digest na kuzielewa hususani post # 28?! Kukupunguzia kazi ya kuanza kuitafuta, wacha niinukuu hapa hapa...!

"Nilichotarajia mimi, endapo mtu atasema kikwazo ni XYZ, nami nikasema hiyo XYZ inaweza kuwa treated this way; then mtu aanze tena kui-crticise hiyo "this way" na sio tena kurudi kwenye XYZ! Na hicho ndicho ninachokiomba wewe na crtitics wengine wakifanye! u know wht i mean?!

Asume issue under question ni tatizo la maji. Nikisema tatizo la maji tunaweza kutatua kwa kuchimba visima, critic asirudi tena kwa tatizo la maji, bali aseme hiyo issue ya visima haiwezekani due to ABC....(say) ardhi ya hapa ngumu sana kuweza kuchimba visima. Kama nitakuja tena na kusema suala la ardhi kuwa ngumu tunaweza kukabiliana nalo kwa kule strong drilling machines; then sitarajii tena mtu alete hoja ya kwamba ardhi ngumu....
Natarajia alete hoja kwamba kupata drilling machine ni ngumu sana....nikisema we can get drilling machine by doing XYZ, then reasonable criticism hapo isiwe na ni hard kupata strong drilling machine, bali hoja hapo iwe how hard doing XYZ.....mkienda that way, mtafika mwisho na ku-conclude kwavile mtakuwa mme-analyse all possible obstacles step by step!!"

Mkuu, hicho ndicho ninachosisitiza kwenye mjadala huu!!! Wewe umeleta suala la kwamba Certificate haiuziki; jambo ambalo nami nimeshalikubali na ku-suggest wht if likifanyika jambo fulani ku-cover hilo la certificate kutouzika! Nimekuambia am afraid hukuzisoma post zingine coz' nilitarajia uanzie pale mimi nilipoishia....u criticise ule mbadala wa kutouzika kwa certificate! Otherwise, itakuwa kila wakati narudia jambo lile lile ki2 ambacho kimsingi si lengo la mjadala huu! Lengo la mjadala huu ni kutafuta mawazo mbadala ambayo mwenye kupenda kuyatumia, ayatumie na asiyeyataka na ayaache! Tatizo liko wapi?

Baada ya kuona watu wengi tunashindwa kuelewana, nikajaribu kutafuta kwenye mtandao endapo ipo sehemu inakofanyika ki2 kama hiki...nazani hamna, ingawaje kutokuwepo sio lazima iwe ni bad idea kwani si kila ki2 lazima kianzie kwa wenzetu ndipo nasi tufuate. Hata hivyo, hebu msome huyu jamaa hapa chini. Huyu kakieleza ki2 ambacho nami nimekidokeza kwenye main tread. Nilichokieleza, ilikuwa ni about 4 years ago, lakini kwa wenzetu kimetokea almost a year. Tumsome:

"
arjun_singh - Member Since: Mar 2011
Subject - Holding Educational Certificate as collateral for Unsecured Loan
I am working for Pvt sector Bank (ICICI) from a long time.. Very recently bank top Mgt (HR) instructed to all the bank staff those who are borrowed Staff Personal Loan from the Bank to submit the Original Education Certificate as a collateral secutiries for their Personal Loan...

Though we (Bank Staff) have availed the Staff Personal Loan as a unsecured loan and given 2 surity as per the Agreement while borrowing Loan...
Now the Mgt as well as HR putting pressure on all the staff to submit the Original Marks Card as collateral....If not they are asking us to repay the entire Loan Amount...
As every one knows that, ICICI Bank is doing this kind practice only to Retain their Employees....
Kindly let me know whether a Company / bank can hold the Education Certificate of their employee... that to as a collateral for Staff Loan..."

Unaweza ku-copy na ku-paste Holding Educational Certificate as collateral for Unsecured Loan kwenye status bar!

Je, hayo maelezo ya huyo Mhindi anayejiita arjun_singh yanakupa picha gani kwa kuzingatia main thread niliyoitoa?! Wakati idea ya kuwabana staff wakorofi kwenye mikopo waliyoichukua nilitoa miaka minne iliyopita (ingawaje i developed the wholly idea since 2004) Wahindi wameiona chini ya mwaka mmoja uliopita!!! Why? wameona it can work! Na wenzetu walivyo aggressive wataifanyia pilot testing lakini baada ya ku-analyse all possible risks!

Ngoja nikuambie kitu kimoja! wakati nikiwa benki hiyo hiyo, niliwahi kumshauri bosi wangu kwamba hivi ina maana gani kumsubiria mfanyakazi wa serikali, hususani mwalimu wa shule ya msingi hadi amalize miaka mitatu ndipo awe na sifa za kupata mkopo wa wafanyakazi wa serikali?! Nikamwambia, kwanini tusiende halmashauri na kuomba Idadi ya walimu ambao huwa wanaajiriwa na wangapi kati yao wanaacha kazi ili tuangalie employment turnover ni kiasi gani? Nilimwambia hili kwa sababu nafahamu employement turnover kwa upande wa walimu wa shule ya msingi ni ndogo hivyo risk ya mtu kuacha kazi na mkopo kupotea vile vile ni ndogo! Kama ilivyo kawaida ya maboss wetu, akapuuza! Leo hii, hizi MFI zilizoibuka kila mahali sizani endapo zinasubiria angalau hiyo miaka 2!!! What For?! Unaogopa nini wakati huo?

NasDaz idea yako nimeikubali na itapunguza tatizo la ajira kwa magraduate we2. But baadhi yao wana akili ya kitoto ukimpa pesa anaenda kutesa na kujenga heshima baa kwani 2nawaona vyuoni. All in all your idea is good.

na wewe wacha kuja na hoja nyepesi hapa. Tofautisha mwanafunzi na mhitimu. Akili zao japo ni mtu mmoja, ni vitu viwili tofauti. Sijawahi kusikia mhitimu kakopa mtaji akaenda kujenga heshima baa. Labda mtaji utakufa kwa yeye kukosa maarifa ya biashara na si vingine
 
NasDas

I have an idea

nadhani inaweza kuwa possible kukawa na program kwa ajili ya wahitimu wa vyuo mbali mbali itakayo wahusisha na kwa ushirikiano na serikali kupitia kitengo chake cha uwezeshaji, mabenki, vyuo vya biashara, donor countries na sponsor companies, program hii ikaitwa enterpreneurship facilitation program ambayo itakuwa na stages, kwanza ni incubation program stage ambapo katika stage hii utapewa elimu ya ujasiriamali na ku develop a viable and bankable business plan out of your own brilliant business idea, pia utawezeshwa kufungua kampuni yenye lengo halisi halafu ukafungua pia na bank account in one of the banks zilizo kwenye program hii, business lisence na TIN , stage ya pili ni baada ya kuwa umekubalika na panel katika stage ya kwanza ya incubation hiyvo basi program partners wote wataku quarantee kama security kwa mabenki ili uweze kupata mkopo na uweze kuanzisha pilot au sample business model, baada ya hapo if the business sounds profitable then stage ya tatu ni you jump in full implementation stage ambapo now you are bankable and trusted with bank hivyo basi wale partners wanajitoa na unasimama wewe mwenyewe kujidhamini katika bank kwa kutumia dhamana ya biashara uliyo ianza kuifanya na hapo pia utakuwa na credit record inayoeleweka ambayo itakuwa pia ni kigezo cha mhusika kudhaminika

ni hayo tu machache ambayo nimefikiria kidogo

wazo hili linaweza kuboreshwa zaidi kwa kuongezea au kutoa baadhi ya mambo
 
Upo mpango wa kuanzisha database ambayo itakuwa na record za watu mbalimbali ambazo zitakuwa zinatumiwa na commercial banks ku-evaluate credibility ya mkopaji...

Sijui kwa sasa mpamgo wenyewe umefikia wapi!!! Hata hivyo, kwa kiasi kikubwa, nahisi hapa itatumika sana kuangalia kama unafaa kuaminiwa kupewa loan au hapana kwa kuangalia hiyo history. Suala la riba, hilo kweli ni tatizo kwani kinachotokea ni kwamba wanalipia defaulters....!!!

Nimeanza kusoma hili la kuanzisha huo mpango muda mrefu kidogo lakini naona siku zinayoyoma tu sijui tatizo liko wapi. hili litawasaidia wengi kuweza kupata mikopo, lakini kama riba zitakuwa bado ziko juu sana kama ilivyo sasa basi mafanikio ya mpango huu kama utaanzishwa yatakuwa ni madogo sana.

na wewe wacha kuja na hoja nyepesi hapa. Tofautisha mwanafunzi na mhitimu. Akili zao japo ni mtu mmoja, ni vitu viwili tofauti. Sijawahi kusikia mhitimu kakopa mtaji akaenda kujenga heshima baa. Labda mtaji utakufa kwa yeye kukosa maarifa ya biashara na si vingine

Mkuu , nakuomba msome LAK kwenye post # 50. I hope if we go this way tunaweza kufika sehemu moja muhimu sana! Binafsi nimemsoma harakahara nikiwa completely tired......nimeiweka kipolo nii-digest baadae nikiwa nimetulia zaidi coz' nimeona something very constructive!
 
Nimeanza kusoma hili la kuanzisha huo mpango muda mrefu kidogo lakini naona siku zinayoyoma tu sijui tatizo liko wapi. hili litawasaidia wengi kuweza kupata mikopo, lakini kama riba zitakuwa bado ziko juu sana kama ilivyo sasa basi mafanikio ya mpango huu kama utaanzishwa yatakuwa ni madogo sana.

Kumbukumbu zangu zinanionesha kwamba mwishoni mwa 2009 PSPF walitoa Business Plan Competitio. One of competitor alikuja na hiyo kitu (but it wasn't new idea coz sehemu nyingi inafanyika). So, yule mdau alikuwa ni miongoni mwa watu waliochaguliwa kwenye initial stage, so am not sure kama bado idea ipo mikononi mwake au iko chini ya mikono mingine. Myself, hata mimi nashangaa ni kwanini inachelewa sana kwani sioni kamani complicated kiasi hasa nikizingatia kwamba endapo commercil banks zingehusishwa vizuru wangeweza hata ku-finance hiyo project kv kwao itakuwa ni muhimu sana!
 
Mkuu , nakuomba msome LAK kwenye post # 50. I hope if we go this way tunaweza kufika sehemu moja muhimu sana! Binafsi nimemsoma harakahara nikiwa completely tired......nimeiweka kipolo nii-digest baadae nikiwa nimetulia zaidi coz' nimeona something very constructive!

anachokiongea LAT kipo kwenye post yangu ya 11. Achukue muda kusoma na post zingine. Na najua umechoka mbaya kutokana na hoja uliyoianzisha kule politika.
 
Back
Top Bottom