BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Mkuu benki haiwezi kukubali ACADEMI CERTIFICATE per see
Ila serikali kama ina nia ya dhati inaweza kushirikiana na hawa graduates kwenye kukopa, soma vizuri post ya entreprenuer
All in all mtoa hoja ana point muhimu sana..try to get him
Kitu kingine kinachoweza kufanyika ni kushusha riba ambayo bado iko juu sana ukilinganisha na nchi za wenzetu. Katika baadhi ya nchi za wenzetu kama credit record yako ni nzuri katika kulipa bills zako basi unaweza kupata mkopo kwa bei poa sana. Kwa mfano sasa hivi katika baadhi ya nchi unaweza kukopa kwa riba ya 2% na kutakiwa kurudisha ndani ya miezi 24 ila kama unataka kulipa kwa muda mrefu zaidi basi riba itaongezeka kidogo. Mikopo kama hii ingekuwepo nchini ingesaidia sana katika kunyanyua viwango vya maisha ya wengi na pia kusaidia kuinua uchumi ulioanguka.