Mabere Nyaucho Marando yupo wapi?

Mabere Nyaucho Marando yupo wapi?

Hapana, NCCR haikuanza kama chama cha bandia. NCCR ulikuwa mkutano tu wa wanasheria kudai mfumo wa vyama vingi. Baada ya vyama vingi kukubaliwa ndipo chama cha NCCR-Mageuzi kikaanzishwa na wale waliokuwa wahuhudhuriaji wa makomngamano hayo ya NCCR. Watu kama Masumbuko Lamwai, Profesa Baregu, Kasanga Tumbo,James Maparara na Chief Fundikira, hawakuwa mapandikizi wa CCM
Sahihi,Nyaucho ni pandikizi,sukrani.
 
Huyu ni mmoja ya Miamba ya siasa kakamavu. Ni jasusi , ni msomi, ni mtu karba ya Tundu Lissu.

Inasikitisha hatupo naye tena kwenye Siasa. Najiuliza alipatwa na nini? Amechoka? Yu mgonjwa? Ni hasara sana kwa Taifa kupoteza watu kama hawa halafu kuwa na akina Nape, Januari na .... .
"karba" ndiyo nini?

Au ulitaka kuandika Kingereza "caliber"?
 
Upo sahihi sana juu ya uanzaji wa NCCR bila neno mageuzi isipokuwa kirefu halisi kilikuwa ni National Convention for CONSTITUTION Reform- Mkutano wa Kitaifa Kwa ajili ya Mabadiliko ya Katiba. Wakitaka Katiba Ibadilike ili tuingie kwenye mfumo wa Vyama Vingi.

Baadaye vuguvugu hilo likawa maarufu ijapokuwa along the way Mzee Mapalala akajitoa kwenda kuanzisha CCW ( Chama Cha Wananchi), Mzee Fundikira akaenda kuanzisha UMD ( Union for Multiparty Democracy) huku Kina Maalim Seif wakiwa na Taasisi Yao waiitayo KAMAHURU. Nadhani UMD ndio kilikuwa Chama Cha kwanza kusajiliwa nchini. NCCR ni baadaye walipokuja kuamua kubadili lile vuguvugu la kudai Katiba na kulifanya Chama Cha Siasa na Sasa wakaitwa National Convention for Construction and Reform ambapo Reform ni MAGEUZI.
UMD ilishughulikiwa haraka Sana,sidhani hata ilifika kwenye uchaguzi 1995,maana mapalala Alianza kuwazungukia machifu wenzie wa kinyamwezi na kisukuma,hayo makabila mawili yenye lugha moja Yana watu nyomi
 
aliugua ndio sababu hakuwa ameonekana kwa muda mrefu. Sifahamu kwa sasa anaendeleaje. Mzee Marando muda wote alikuwa anatabasamu ukimuona kwenye media.
 
Back
Top Bottom