CCM MKAMBARANI
JF-Expert Member
- Mar 15, 2017
- 2,031
- 1,514
Sahihi,Nyaucho ni pandikizi,sukrani.Hapana, NCCR haikuanza kama chama cha bandia. NCCR ulikuwa mkutano tu wa wanasheria kudai mfumo wa vyama vingi. Baada ya vyama vingi kukubaliwa ndipo chama cha NCCR-Mageuzi kikaanzishwa na wale waliokuwa wahuhudhuriaji wa makomngamano hayo ya NCCR. Watu kama Masumbuko Lamwai, Profesa Baregu, Kasanga Tumbo,James Maparara na Chief Fundikira, hawakuwa mapandikizi wa CCM
"karba" ndiyo nini?Huyu ni mmoja ya Miamba ya siasa kakamavu. Ni jasusi , ni msomi, ni mtu karba ya Tundu Lissu.
Inasikitisha hatupo naye tena kwenye Siasa. Najiuliza alipatwa na nini? Amechoka? Yu mgonjwa? Ni hasara sana kwa Taifa kupoteza watu kama hawa halafu kuwa na akina Nape, Januari na .... .
Aliyetokea Tukuyu?Mbona mbowe ndio snitch no 1
Siku mlikua ukweli mtajiona mlivyo pumbu za mbwa
Hii nchi mpinzani wa kweli alishakufa kwenye Premio
Nam namAliyetokea Tukuyu?
Nccr ilianzishwa na makchero na wakamuweka kachero wao kuwa mgombea urais,mrema,na Hilo siyo la mwisho,endeleeni kupoteza muda kupambania upinzaniKwa kuwa wananchi wengi wamejiweka mbali na siasa imekuwa rahisi kwa ccm kuanzisha vyama na kupandikiza watu wao ndani ya vingine!
UMD ilishughulikiwa haraka Sana,sidhani hata ilifika kwenye uchaguzi 1995,maana mapalala Alianza kuwazungukia machifu wenzie wa kinyamwezi na kisukuma,hayo makabila mawili yenye lugha moja Yana watu nyomiUpo sahihi sana juu ya uanzaji wa NCCR bila neno mageuzi isipokuwa kirefu halisi kilikuwa ni National Convention for CONSTITUTION Reform- Mkutano wa Kitaifa Kwa ajili ya Mabadiliko ya Katiba. Wakitaka Katiba Ibadilike ili tuingie kwenye mfumo wa Vyama Vingi.
Baadaye vuguvugu hilo likawa maarufu ijapokuwa along the way Mzee Mapalala akajitoa kwenda kuanzisha CCW ( Chama Cha Wananchi), Mzee Fundikira akaenda kuanzisha UMD ( Union for Multiparty Democracy) huku Kina Maalim Seif wakiwa na Taasisi Yao waiitayo KAMAHURU. Nadhani UMD ndio kilikuwa Chama Cha kwanza kusajiliwa nchini. NCCR ni baadaye walipokuja kuamua kubadili lile vuguvugu la kudai Katiba na kulifanya Chama Cha Siasa na Sasa wakaitwa National Convention for Construction and Reform ambapo Reform ni MAGEUZI.
Kivipi?!MKUTANO MKUU, 1997 RASKAZONE HOTEL TANGA
UMEME KUZIMIKA
MREMA vs. MARANDO
MWENYEKITI vs. KATIBU MKUU
(Kwahiyo sikushangaa sana issue ya MBATIA na SELASINI)