SoC03 Mabilioni ya pesa yanayotafunwa na wachache yangetumika kundeleza wabunifu tungekuwa mbali sana

SoC03 Mabilioni ya pesa yanayotafunwa na wachache yangetumika kundeleza wabunifu tungekuwa mbali sana

Stories of Change - 2023 Competition

Fannjosh

Member
Joined
May 28, 2016
Posts
35
Reaction score
46
Utangulizi
Katika kukua kwangu, nimebahatika kusikia na kushuhudia wabunifu wengi katika nchi yetu. Mfano: Kuna mtu alitengeneza umeme wa kinyesi, mwingine gari, mwingine ndege inayoruka kwa injini ya piki piki, mwingine stesheni ya redio na wengine kibao.

Imekuwa ni historia katika nchi yetu kuona baadhi ya viongozi wakitafuna fedha za umma bila wasi wasi kabisa. Hivi karibuni ripoti ya CAG imeonyesha upotevi wa fedha nyingi sana ambazo kama zingeelekezwa katika kutatua changamoto basi zingefanya kazi kubwa sana.

Hivi! hawa wabunifu huwa wanaishia wapi mara tu baada ya kuonekana kwenye vyombo vya habari?
Ni hali ya kawaida kuona wabunifu wakionyeshwa kwenye runinga hasa kuonyesha kazi zao walizofanya. Lakini swali ni kwamba, baada ya ubunifu wao kuonekana, mbona hawaonekani tena? na mbona hatusikii wamefikia wapi? kazi zao zimesapotiwa kwa kiasi gani? kuna viwanda vimeanzishwa ili kuendeleza ubunifu huo?

Haya maswali yananipa picha kwamba, yawezekana ubunifu wao haupewi sapoti na wala hauendelezwi. Na huwenda pia baadhi wanawekewa masharti mengi sana kiasi kwamba inakuwa vikwazo kwao wanashindwa kuendeleza ubunifu wao.

Ukweli ni kwamba, sekta binafsi duniani kote ndiyo inayoinua uchumi wa nchi husika. Makampuni, viwanda na taasisi nyingi binafsi zimeonekana kuchangia uchumi wa nchi husika kwa wastani wa 80%. Wabunifu wanaoanzisha kazi zao wangeweza kuleta matokeo makubwa sana katika ukuaji wa uchumi wetu. Cha ajabu sasa! Wakiibuka siku moja Hatuwasikii tena.

Nikafikiria tena... Hivi pesa zinazopigwa na watu wachache kama zingewekezwa kwenye bunifu hizi, Nchi yangu ingekuwa wapi? Nikajaribu kufikiria juu ya watu mashuhuri kama akima Elon Musk, Jeff Bosses, Jack ma jinsi walivyokuwa wabunifu na leo tunatumia bidhaa zao.

Kama bunifu hizi zingepewa vipaumbele, basi leo nchi yangu ingekuwa inatengeneza magari mazuri, ndege zinazoruka angani, mifumo imara ya simu na compyuta, umeme bora NK. Nchi yangu nchi yangu.. Tunatamani kuwa na viongozi wenye weredi, uaminifu na uadilifu ili pesa zinazotumika vibaya, basi zikatumike kuinua kazi za wananchi.

Mamlaka na sekta zinazohusika na sanaa zijikite katika kutoa sapoti kwa wabunifu hawa kwa kuendeleza pale walipoishia, kwa kutoa mitaji, kwa kutangaza bidhaa zao, na pia kuwapeleka katika vyuo vya sanaa na ufundi ili wakafundishe wengine.

Tunatamani kuona viongozi wakisimama majukwaani na kunadi viwanda vilivyoanzishwa kutokana na ubunifu wa mtu fulani. Tunatamani kuona msamaha wa kodi kwa vijana wabunifu wanaoanza kuingia sokoni. Tunatamani kuona michango iliyotolewa kuinua bunifu za watu ili na sisi kama nchi tujivunie kuwa na teknolojia yetu wenyewe badala ya kunyenyekea vilivyotengenezwa na mataifa mengine.

Wale wanaopiga pesa nyingi kwa rushwa, ufisadi na wizi, hebu kuweni na utu. Pelekeni fedha hizo kwa wabunifu ili kusapoti kazi zao na hatimaye nchi yetu ionekane ina watu wanaopenda maendeleo ya Umma na sio maendeleo ya tumbo la mtu.

Hitimisho
SAPOTI WABUNIFU, EPUKA WIZI NA RUSHWA ILI KUKUZA UCHUMI WA TAIFA.

VOTE kama umependa makala hii. Asante
 
Upvote 2
Back
Top Bottom