Mabinti wa Kiislamu kuvaa bukta katika mafunzo JKT ni kwenda kinyume na Katiba

Mm sipo kwenye ugalatia wa ufarisayo
Mzee mimi ni Mgalatia...tukubali tu vile vibukta vinatweza utu wa watoto wetu wa kike.
Nalizungumzia jeshi na taratibu zake. Hivi unafikili kwenye mafunzo ya jeshi Kuna mda wa kuwaza uzinzi Kama mnavyofikili?. Mleta mada kajaa uzinzi tu. Na anawaza kila mtu ni mzinzi Kama yeye kaona vibukta kapagawa analeta visheria vya kipuuzi. Mkuu watu wa Aina hiyo hata akiniona mtoto aliyemzaa anamtamani sababu ya kujaa uzinzi kwenye mwili wake.
 
Ndugu yangu, labda jeahi la siku hizi liwe hivyo. Mimi ni mehenga kidogo. Dada zetu na kaka zetu kabla lile jeshi lenyewe halijafutwa miaka ya tisini mwanzoni, walikuwa wanatupa taarifa za ngono hatari....hali ilikuwa mbaya na ni ukweli...sasa labda hilo jeshi la sasa hivi liwe lomeboreshwa sana...pia urahisi wa kupata na kusambaza taarifa unaweza ukawa umechangia mambo ya ngono kupungua...ila wadada wa enzi zile wadinywa sana
 
Sikukatalii unachosema kiongozi. Lakini uzinzi na ngono Kama zipo hata wavae nguo za Aina gani mzinzi atatamani tu. Nilichokiona siku hizi Kuna mambo yameboreshwa na kuepusha na kukataza kila Jambo ambalo linaondoa nidhamu za kijeshi
 
Kwa hiyo stara ni Hako kakitambaa kichwani ka kufunika kichwa anachovaa Mwanamke wa kiislamu Wakati kavaa kasuruari ka jeshi kanakobaba na tumatako twake tulikobinuka tunaonekana
Yote ni ktk stara.

Lkn stara kubwa kabisa ni kuwa na kambi tofauti. Kama ilivyo boarding za wanawake na wanaume
 
Kuwalisha vibukta na kuwachanganya na wavulana ni kichocheo cha kuandaa vijana hana na ufuska.

Jambo hili si dogo tunakwenda mahakama kutaka tafsiri ya mahakama kama ni lazima kwa wasichana kuzuiwa kuabudu kupitia uniform zao. Lkn pia kama ni sharti la jeshi kuwachanganya wasichana na wavulana kambi moja
 
yaonesha wewe asili yako ni lile tabaka ambalo umemaliza wakati wazazi hawakufunga ndoa.

Nawe huenda una mtoto nje ya ndoa.

kwa hiyo ukiona dada yako anaziniwa au anaishi kinyume hushtuki.

Ktk tabaka letu zinaa ni jambo baya sana kiasi kwamba sio tu tunakatazwa tusizini, bali tusikaribie zinaa.

Kambi za jkt hata kama mtoto anatokea nyumbani kama malaika watarudi akiwa shetani.

Huwezi kuwalisha vikaptura ukawachanganya na wavulana ukategemea wata kusimama na uadilifu.

Na msikurubie zinaa.
 
Mohamed Abubakar navyojua jeshi siyo lazima kwenda. Kama unakwazika kwa mwanao kuvalishwa hayo mavazi mkataze asiende jeshini.
Tuishi kwa kuacha athari chanya kwa jamii. Kwa kukumbushana juu ya yale tuliyokubaliana kama taifa.

Mkataba wetu kama taifa KATIBA sio mbaya. Bali wasimamizi eitha hawana maarifa au wanafanya kazi kwa mazoezi, kueleweka vibaya wa dhana na kwako huenda ni fikra mpya. Mara nyingi fikra mpya hupingwa mpaka izoeleke.

1. Serikali isiyo na dini ina maana gani.

Kulinda wenye dini au kuwadhibiti? Ktk mataifa yanayoishi kwa kusimamia misingi ya haki za binadamu taifa lisilo na dini ina maana serikali italinda haki ya wenye imani na dini. Kinyume na tz ambapo baadhi ya watu wa imani wanadhibitiwa. Jkt no mfano halisi.

Uhuru wa kuabudu ulio ndani ya katiba huishia ktk geti za kambi zao. Kinachofanywa na serikali ni The Clash of civilizations.

Kwa hiyo suluhisho si kumuondoa mwanangu bali kufata matakwa ya katiba hii hii tuliyonayo yatosha
 
Mbona Waislamu wengi tu wanatoza ushure biashara za pombe na kitomoto na wengine wako benki maafisa mikopo wana process mikopo ya riba,
Mbona wasanii wengi tu Waislamu wanafanya matangazo ya pombe na pia Waislamu wengi wanafanya biashara ya betting?!
 
Tuanzie hapa,
Katika dini ya Kiislamu wanawake wanaruhusiwa kuwa viongozi wa siasa watawala, wanajeshi au majaji??
 
Tuanzie hapa,
Katika dini ya Kiislamu wanawake wanaruhusiwa kuwa viongozi wa siasa watawala, wanajeshi au majaji??
Why Not.

Kwa mujibu wa wanachuoni wa karne hii. Mwanamke yyt aliyepitiliza miaka 45 anaruhusiwa kuongoza taasisi yyt.

Mke wa mtume (s) bi Aisha aliwahi kuongoza jeshi ktk historia ya uislam.

Hata hivyo hiyo ni mada mpya, fungua threat yako.
 
Mbona Waislamu wengi tu wanatoza ushure biashara za pombe na kitomoto na wengine wako benki maafisa mikopo wana process mikopo ya riba,
Mbona wasanii wengi tu Waislamu wanafanya matangazo ya pombe na pia Waislamu wengi wanafanya biashara ya betting?!
Suhulisho ni utawala wa majimbo yenye uhuru zaidi au uhuru kamili wa kujiamulia mambo yao wenyewe.

Uzuri wa aina hii ya utawala kila jimbo litaamua iwapo pombe, kamari, mfumo wa riba uwe ndio msingi wa uchumi au laa.

Tuhamasishane kuutawalisha mfumo huo wa utawala
 
Hata katika mfumo wa majimbo jeshi haliwezi kuwa suala la kimajimbo, jeshi litabakia kuwa federal tu, la kitaifa.
Ni ujuha kutamani majimbo ili mwanao tu asivae bukta jeshini.
 
Lazima kuwe na sheria na taratibu za pamoja kama nchi ambazo ziko juu ya dini zote, haiwezekani kila mtu akataka kuingiza mambo ya dini yake katika mifumo ya serikali. Yani wa Niqab atake niqab jeshini, rastafarian atake kusuka rasta jeshini, msabato akatae kulinda nchi Jumamosi hilo litakuwa jeshi au uwanja wa vurugu.
 
Lilikuwa ni kosa kubwa kuruhusu mavazi yanayowatambulisha wanafunzi kwa dini zao mashuleni, hayo makosa hayapaswi kurudiwa.
 
Ungejua hizo sera za woke, DEI na political correctness zilivyoleta mtafaruku mkubwa huko Magharibi hadi kusababisha watu wa hovyo hovyo kuchaguliwa kwa sababu ya hasira za raia usingekuwa unazirejea rejea hizo nchi katika haya masuala.
 
Bila kusahau pia mashoga wanaruhusiwa katika jeshi la Marekani na Africa Kusini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…