Mabinti wa Kiislamu kuvaa bukta katika mafunzo JKT ni kwenda kinyume na Katiba

Ostaz umepuyanga hapa. Mabuibui na ukakamavu wapi na wapi sheikh.
 
Kaeni nao huko huko mkiwaleta huku lazima watii kilichopo huku.
Hujui hata ni kwanini hasa wanavaa hizi pitshorts Haina haja ya kuleta matakwa Yako.

Jeshini siyo msikitini, we train people to become combat and fighting tools not to decorate suitors!

Jeshi ni idara ya kitaifa ya kiulinzi na siyo sehemu ya kudhihirisha Imani, itikadi au mirengo ya aina yoyote.

Unataka kuruta apande kwenye IVECO na gauni la kufunika vidole vya miguu??? Jinga sana boss!
 
Kuwa mpole; Acha Serikali ifanye kazi yake. Akirudi nyumbani after.....months atavaa anavyotaka na ww (esp. ukiwa Baba i.e Me) wala huwezi kamwe kumzuia - mbona utakuwa unakaribisha maswali ya "Mbaba mzima anamfuatilia Binti yake vipi huyo?"
Bukta za Ke ni tofauti na bukta wanazovaa Me. Halafu yale masuala ya "kibaiolojia" wapo ma-Afande wa kike na wanayashughulikia.
 
Askari dini na yeye tofauti kaulize Somalia na sudani kwenye uislami mtupu wanatwangana Hadi mwezi wa Ramadan wako kazini hakuna Cha Leo idd Wala Nini

Raisi mfano akiwa mapumziko walinzi hawawi mapumziko iwe msabato mlinzi au Mkristo au Muislamu

Kama waislamu hutaki mwanao aende jeshi sio kesi mwambie asiende Jeshini
 
Kwanza naunga hoja ikiwa mimi sio muislamu.

Bila mihemuko yoyote ya kidini. Kule jeshini wanavalishwa vibukta vidogo viko juu ya magoti.

Pili imani ya mtu ni ya kuheshimu sana kuepuka migongano ya kiimani. Waislamu wanalazimishwa kusafisha mabanda ya nguruwe, kitu ambacho sio sawa
 
Huu uzi bila picha unakosa ladha. Weka picha ili tupate ushahidi
 
Hii nchi ina watu walalamishi sanaa! Dini gani inakubali mavazi ya ovyo? Ubinafsi tu
 

Kwahiyo unataka kusema dini ya kiislamu pekee ndio inakataza kula nguruwe? Kwann usingewaongelea wasabato?

Je kwa mimi mkristo ni sahihi kuingia ulinzi mpaka jumapili, mbona makamu wa raisi anapumzika jumapili? Vipi kuhusu wasabato na Waislamu wanaosali na kuswali Ijumaa je nisahihi kwenda kulinda siku za ibada?

Mwanamke wa kiislamu hatakiwi kuacha kichwa wazi hadharani je ni sahihi kuvaa hijab juu ya kombati ya jeshi?

Je ni sahihi kuruti kupiga course kudandia maAshok na Abaya?

Niliingia jeshini nikiwa mlokole safi, lakini wanajeshi wakanitoa ulokole wakauingiza Uaskari, Mbona hukemei kwamba wanajeshi wanabadilisha tabia za imani ya watu?
 
Unapenda ligi kila mtu mawazo yake yaheshimiwe

Hawajakataa kwenda jeshini na hakuna sehemu wanesema wanakimbia na abaya

Wanaweza kuvaa track mabwanga zisizoshika miili yao
 
Ni Africa pekee ndio tunapenda kufanya jambo bila kuhoji. Ukihoji unashambuliwa vibaya sana.

Kwanza swalI langu la msingi kwa nini watu wanyoe mapara? For what reason

Nchi zote kubwa dunuani, zinatambua heshima za dini husika ndio maana unqona jeshini wanawake wa kiislam wanapewa uhuru wa kujisitiri


 
Unapenda ligi kila mtu mawazo yake yaheshimiwe

Hawajakataa kwenda jeshini na hakuna sehemu wanesema wanakimbia na abaya

Wanaweza kuvaa track mabwanga zisizoshika miili yao
Umewahi kujiuliza kwanini ukiwa Mzalendo jeshini unavaa Track na ukiwa kuruti unavaa pitshort?

Acha kupelekwa pelekwa na midini dini utachelewa. Acha jeshi lijiendeshe kama linavojiendesha.

Waislam mnajikutaga imani mnazijua sana.
 
Hao waliovaa kidini nguo za jeshi ni askari wa dini nchi za kiislamu

Nchi za kiislamu Mwanamke haendi vitani ni askari tu wa mitaani wa kusimamia sharia za dini ya kiislamu kusimamia uvaaji hijabu mitaani
 
Weka japo kapicha tuione na sisi kina Tomaso
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…