Mabinti wa Kiislamu kuvaa bukta katika mafunzo JKT ni kwenda kinyume na Katiba

Nikiandika kama muislamu mwanaume na niliyepitia mafunzo ya jkt kwa mujibu miaka kadhaa nyuma .

1. Niseme tu jkt/jeshi/ polisi ni kazi ambazo hazifai kwa muislamu awe wa kike au wa kiume na hii ni kiimani zaidi maana hata wanaume tulivaa pitshort kibukta ambacho hakifuniki magoti hivyo kuacha mwili uchi
maana uchi wa mwanaume ni kitovuni mpaka kwenye magoti hii ni kwa mujibu wa kidini (uislamu).

2. Muda wa ibada huwa unakosekana kutokana na ratiba zilivyo kule na pia mavazi hayaruhusu kuswalia hivyo ni ngumu kwa kijana wa kiislamu kutimiza swala zote tano kwa wakati , japo kuna watu watatumia mlango wa udhuru ila jibu langu ni kuwa udhuru haupo maana haukulazimishwa kwenda kule.

3. Kama umeona kuvuliwa nguo kwa wasichana wa kiislamu ni jambo kubwa mkuu kuna kitu inaitwa KUPIGWA TOCHI sitozama ndani zaidi ila wengi mnafahamu na kwa wale ambao hamfahamu basi jaribuni kuuliza uliza sitolielezea kiundani ila ni ukaguzi wa mwili mzima na hii ni kwa wanaume na wanawake no exception MEANING KAMA DAKTARI NI MWANAMKE ATAHUDUMIA WOTE NA KWA MWANAUME PIA HIVYO HIVYO.

4. Jeshi huwa halazimishwi mtu kwenda na hata usipokwenda hakuna atakayekufuatilia na haito affect chochote kwenye maisha yako ya kila siku hivyo sioni kama kuna ulazima wa binti au kijana wa kiislamu kwenda jeshi.

5. Ukifika kule kuna mkataba utasainishwa na kuna wiki mbili za uzalendo na kama haujiskii kubaki upo huru kuuvunja mkataba na kuondoka ndani ya hizo wiki mbili hakuna wa kukulazimisha.
 
Kulikuwa hakuna ulazima wa kutumia lugha kali mkuu ungemjibu kwa ustaarabu ingetosha tu.
 
Walivaa.....kabla na hatukuona madhara yake. Hao mabinti zenu wakiingia disco na kutembelea Beach wanapigilia kaptura eti JKT Ni kinyume. Acheni udini kwenye Mambo ya kiserikali

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ndugu hii nchi zinaendeshwa kwa katiba. Iwapo kuna sheria yyt zinazopingana na katiba, sheria hiyo ni batili.

Pili kama waislam tuna mapungufu ya kuelewa elimu Sosholojia na uraia na matokeo yake tunaona uislam hauko compatible kwa baadhi ya mazingira. Hili haliwezi kuondoka hadi mtaala wetu wa elimu uongeze somo la Sosholojia.

Miaka ya 80 watoto wa kiislam hawakuruhusiwa kuvaa uniform zenye kukidhi na kuwatumikia waislam uhuru wao wa kuabudu. Waisla. Wa wakati huo walisema haifai kuwapeleka watoto wa kike mashuleni.

Lkn walipoibuka wenye maarifa wakasimama na kushinikiza ruhusa ikatolewa.

Hali hiyo iko ktk vikosi vyetu. Yaonyesha ktk vikosi vyetu zinafanya mambo kimazoea.

Katika utawala wa kidemokrasia na serikali isiyo na dini, inayozingatia utawala bora, haki za binadamu na uhuru wa kuabudu. Kutokuwa na dini manake ni kulinda wenye dini hata kwenye idara za serikali na si kuwadhibiti.

Google hii

GUIDE ON RELIGION AND BELIEF
IN THE ARMED FORCES

uone nchi nyingine kama malawi, sa, uk, us wanavyoweka utaratibu huu kwa wenye dini zote kupewa haki zao za kiibada kama kuvaa kilemba kwa masingasinga wa kiume, msalaba kwa wakristo na hijab kwa mabinti wa kiislam.

Hatuwezi kuharamisha jambo kwa sababu kuna watumishi hawajui katiba inasemaji.

katiba ya nchi inawapa askari unapotifa muda wa swala wenye mahitaji hayo waende wakati shughuli nyingine zinafanywa na wengine.

Kutofata ibada zako kwasababu kuna mpagani inayoongoza vikosi kakuta utaratibu kama huo hatupaswi kuharamisha waislam wasishiri mafunzo ya jeshi.

Angalia wenzetu tena marekani.

Kwann waznz, wadanganyika wakubali ratiba iliyoandaliwa na mkurya ionekane ndio sheria ya nchi.

 
SEMA mkuu leo umeongea pumba point yaani we unataka kuileta dini ya waarabu kwenye jeshi la waafrika dah hembu funguka akili bas

Kama jeshi la Marekani wameweza kupeleka dini ya waarabu ktk jeshi lao.

Marekani yenye 5% ya waislam. Tanzania yenye zaidi ya 30% ishindikane.

Tatizo ni pumzi ya kutoweza vumilia values za makundi mengine, tatizo ni fikra ngeni kwako, katiba inakataza uhuru wa kuabudu ktk kambi za jeshi, tatizo ni mfumo wa serikali kuu na kuwa tunahitaji mfumo wa serikali za majimbo yenye uhuru zaidi wa kujiamulia mambo yao wenyewe, tatizo ni itikadi ya nchi kwa mujibu wa waanzilishi wa itikadi hiyo, tatizo ni somo la Sosholojia na uraia au tatizo ni utz.


 

Attachments

  • IMG_2hiiht.jpg
    81.8 KB · Views: 3

Mtoto wako asiende basi JKT ili kumlinda. Maana ukiona vizuri ni kama unataka mambo ya uarabuni yaende jeshini. Hizo ni culture zao. Tuna culture zetu.

Col. Ghadhafi alikuwa analindwa na mademu watupu. Unataka na sisi tuige? Halafu wote wakipata ujauzito muda mmoja itakuwaje?
 
wa ghadafi walikuwa wanapimwa bikra kila siku, ukikutwa haipo fasta unaondolewa, walikuwa hawaruhusiwi hata kuwa na mahusiano au kunyanduana licha kuolewa.
 
Ujinga mzigo. Lkn hii ni kazi ya chama, kazi ya mwalimu.

Amebrainshawed vijana na kuona all disinformation is a true way of live.

Hii ni haki ya kikatiba ndugu

Walivaa.....kabla na hatukuona madhara yake. Hao mabinti zenu wakiingia disco na kutembelea Beach wanapigilia kaptura eti JKT Ni kinyume. Acheni udini kwenye Mambo ya kiserikali

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app

Utaondoka kwenye mada.

Hoja hapa ni katiba inatoa uhuru wa kuabudu kwa kila raia. Ktk uislam kuvaa hijab ni ibada (kuabudu). Kwanini haki hii inaminywa kwa wasichana jeshini.

Kwanini wanafunzi wa shule warehusiwe lkn wanafunzi wa jkt/jku wadhibitiwe.

Nadhani tatizo ni jambo jipya kwa tz. Lkn kwa Malawi, sa waruhusu kupitia guide.

GUIDE ON RELIGION AND BELIEF
IN THE ARMED FORCES


Bahati mbaya taasisi mama bakwata wao wako usingizini.
 

Attachments

  • Screenshot_20220114-215050.jpg
    288.9 KB · Views: 2
Nikubali kwanza sikuwahi kulifuatilia hili kiundani hivyo meengi uliyoandika hapo nilikuwa siyafahamu ila nimejifunza kitu na nimekuwa interested kujifunza zaidi inshaallah nitachimba zaidi ili niwezw kuwa familiar na sheria hizi hasa kwenye nchi ambazo ni za ki demokrasia kama ya kwetu na waliwezaje kufanya mabadiliko na kama Kuna lolote limebadilika baada ya kupitishwa sheria hiyo.

Itanichukia muda ila inshallah kwa kdiri nitakavyoafikishwa nitakuwa nachangia uzi huu as long as utakavyokuwepo hewani.

Jazakallahu khairan akhi .
 
Wanavuliwa nguo zote ili kukaguliwa pia haswa watoto wa kiume.
 
Kwa hiyo stara ni Hako kakitambaa kichwani ka kufunika kichwa anachovaa Mwanamke wa kiislamu Wakati kavaa kasuruari ka jeshi kanakobana na tumatako twake tulikobinuka tunaonekana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…