Unapoliongelea Jeshi basi hakikisha kwanza umeelewa misingi ya uendeshaji wake.
Kuna kitu unasahau mkuu. Katika Social status kuna baadhi ya mambo hayatathiminiwi kwa hali ya kawaida.
Mfano; Kijamii Mwanamme kumpiga mwanamke sio jambo linalokubalika na wengi, haijalishi kosa gani kalifanya kwani kufanya hivyo jamii huona ni ukatili. Ndio maana utasikia watu wakisema
"Haikuwa na haja ya kumpiga angemwacha tu aende kwao"
Walakini akitokea jambazi wa kike basi hata akatokea mwanamume akapambana naye na kumuua basi sifa huenda kwa mwanaume kuwa amefanya kitendo cha kishujaa licha ya kuwa mwanamke yule ameuawa.
Namaanisha kuwa Ipo misingi ya kijeshi ambayo ukiitathimini kwa maisha ya kawaida kwenye jamii utakuta ni Ukatili, Udharirishaji, Unyanyasaji, Upotofu wa mila na desturi au Kutoheshimiwa kwa misingi ya dini. Lakini kumbe misingi hiyo ndiyo yenye kuongeza utendaji bora wa majeshi pamoja na usalama
Najua unaweza waza ina maana gani kwa wanafunzi wanaoenda kuchukua mafunzo kwa mda mfupi?
Kikubwa katika mafunzo haya sio mda bali yale wanayoenda kujifunza. Haitakuwa bora kubadirisha taratibu za jeshi eti kwa sababu ni mambo ya mda kwani kwa kufanya hivyo itakuwa haina thamani kuwepo kwa mafunzo hayo.
MUHIMU ZAIDI NI KUWA yote hayo yanafanyika kwasababu kadha wa kadha, miongoni mwao ni
1. Usalama na Usafi
2. Kutokuwepo kwa Upendeleo wa Kidini
3. Ufanisi wa Mafunzo
4. Kushirikiana na Kujenga Udugu
Wazazi na walezi wanapaswa kutambua jeshi halifanyi hivyo kwa kukinzana na misingi ya kitamaduni au dini bali inatokana na sababu mbalimbali za kiutendaji na kijeshi ambazo zinalenga kuhakikisha usalama, utendaji bora, na umoja wa kikosi.
Ndio maan baadhi ya sheria hazizingatiwi.