Mabinti wa kisasa hebu acheni uongo usio na maana

Mabinti wa kisasa hebu acheni uongo usio na maana

Huo kimsingi ni utoto tu na kuji “kukuz” kuna limoja nilikutana nalo humu humu jeiefu nikasema hiiiiiii!~ in hayatiz voice

Tabia hizo hizo za kujikweza unaweza dhania ni mtu wa maana kumbe jau tu [emoji23][emoji23][emoji23] !!! Mambo ya kishamba hayo kama unazo zitakutangaza wala huna haja ya maigizo na upambe!
Kabisa mwana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umejuaje?! [emoji15][emoji15][emoji15]

Wazuri mbona wapo wengi ni vile tu sijawahi leta story zao hapa mazuri yao. Ila wapo wengi tu mbona. Anyways, huwa siongelei kwa nia mbaya (u sound like u took it personal), naongelea kwa namna ya kujenga.

Kwa mfano wewe ukisha soma hapa sidhani kama utaanza kusema uongo na umeona wanaume hapa wanakerekwa na hiyo tabia.....

So ni part ya kujifunza. Wanaume tunajua zaidi bad sides za wanawake. By the way, wanaume huwa hatukosei..... [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwamba wewe unanifundisha vile natakiwa kubehave mbele ya mwanaume wa kiafrika anaenitongoza😂😂😂 nalijua hilo kabla hujabalehe we dogo

Mazuri yao labda uyaandike leo sijawahi kuona popote humu jf kwa ID yako hii labda uwe na nyingine
 
Hahahahah na mademu wa hivyo ndio ma Mogul wa kudanga! Kuna mtu humu namuonaga ana Taizi hizo ila namchuniaga tu [emoji75][emoji75][emoji75] but what i know atakuwa hewa tu ila mtu wa mipango kweri kweri!!!
Itikadi za kusema kuna mzigo wangu upo china nasubiria paperwork...... "Mzigo gani mama si useme tu umefua unalinda heshima kwa uongo"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habarini wadau. Naandika hii kitu hapa baada ya kukerwa na tabia za baadhi ya mabinti especially hawa wamjini ambao wameanza kurithi tabia zile walizokuwa nazo wanaume za "kuna hela na isikilizia" halafu baada ya dakika kumi utasikia "una elfu tano au kumi ya karibu hapo".

Ipo hivi, kuna wadada kadhaa nimenotice wanahii tabia katika mazungumzo kukuaminisha wao ni watu wa mipango mikubwa. Na hata wanavyojiweka ni as if ni watu muhimu sana hapa mjini but ukweli wa mambo ni wabangaizaji wasio na mbele wala nyuma.

Kuna m'moja ameshakuwa na tabia ya kunicheki kuniomba kuniazima gari akisema ana wageni sijui wanakuja kutoka nje wanahitaji usafiri watakaotumia wakiwa hapa mjini.

Nikamkata nikamwambia twende nitakupeleka safari yako. Nimekwenda mchukua yupo na wenzake wawili, wanasema wanaenda serena kufika hapo serena wanaangaliana yale macho ya tumeumbuka, mimi nikaona wananipotezea muda maana waliniweka zaidi ya nusu saa hapo kwenye kiti sehemu ya kusubiria kisha mwenzake nisie mjua anakuja niomba ufunguo kuwa anaomba aende pale posta ATM mara moja kisha aniletee, nikamwambia ngoja twende sote na mimi nilikuwa naenda huko, tukaenda kufika pale CRDB anatoa toa macho (sidhani kama hata alitoa hela alipoingia kwenye ATM mule). Nikamrejesha serena kisha nikampigia mwenzake nikawaaga nikawaambia nina dharula nitawareje, sikurudi tena.

Mwingine kila nikichekiana nae story zake ni "kuna jamaa tuna contract nae katika ile kampuni yangu, hapa ndio naangalia contract inakaribia kuisha ili nionane nae tukasaini mkataba mwingine" ukimuuliza mnadeal na nini katika kampuni yako, ooooh apartments kwa foreigners, tuna import na kuexport bidhaa etc, halafu hapo hapo anakupiga kibomu cha msosi. Au anaomba umnunulie soda tena anachagua yeye anataka soda gani.

Mwingine nilishapiga hadi mashine, shida ikaja baada ya kumleta maskani. Ni mwanamke ambaye hana impact ndani ya nyumba ukiachia kukuomba hela ndogo ndogo bila utaratibu as if mission yake ni kuhakikisha hauna hata mia mfukoni.

Ukiachia kulala hadi saa nne asubuhi kulala tu kitandani anachat na kupiga simu za kuongea na mashost zake na hakuna la maana wanaongea zaidi ya kupeana umbea wa juzi waliposafiri au bata sijui kumuongelea mtu gani, hawana mazungumzo ya maana.

Ila mtu huyu huyu ukiongea nae anaongelea kuhusu kufanya kazi katika NGO iliyomlipa milioni 2. 7 take home na imefungwa kipindi cha magufuri.

Mara akwambie anasomesha wadogo zake international schools, na anamhudumia mama yake mwenyewe. Mara akwambie sijui anataka ajiajiri anataka kufungua kampuni ya beauty and cosmetic ambayo ataiweka kule masaki au oysterbay na inalipa sana. Mara aseme yeye ni CEO haoni haja ya kuajiriwa.

Ila ukitoka kwenda dukani nje, utaona text kutoka kwake imeingia beib, ukirudi niletee Cadbury bars mbili na maziwa ya asas au utasikia niletee sausages na apple juice ya ceres kubwa. Anaagiza hivi kwa confidence kabisa utadhani mimi ni babake.

Unakuta mpo kwenye foleni barabarani inapita vogue utasikia one day lazima nita own hii gari...... Nina rafiki yangu ana jaguar hii ya 2018 and she's only 25, yaani i must get there....

Sasa huwa nawatazama nasema hivi hawa ni kwamba hawaoni uhalisia wa maisha yao au ni vipi. Watu wana maisha ya kubangaiza, wanatoka katika very common families za kitanzania ambazo wazazi ni wastaafu na hawana hela.

Why mtu usiwe humble na kuishi according to your level requirements wakati unaplan kuwa mkubwa baadae....?!

Why uishi maisha ya kufake fake na uongo mwingi ile hali hauna uwezo na ni tegemezi by 150%?!

Kuna haja gani ya kunidanganya kuwa kuna report naandika mara sijui kuna email muhimu nataka nijibu hapa.... Au unanipigia simu au kunitext whatsapp baada ya kuniona online saa saba usiku halafu unanifix kuwa Atm imemeza card na hauna balance muda huo unaomba nikuazime 50,000 utanirejeshea asubuhi, halafu asubuhi ikifika unapiga kimya naona tu upo online unapost status unakaa kimya wiki, hatimae mwezi na miezi?!

Au unaniazima laptop unasema kuna a very serious work unahitaji kutype (hata haujulikani unajishughulisha na biashara gani mjini). Kisha nakupa tu bila ya kukuuliza swali lolote zaidi ya utaniletea lini, cha ajabu dakika chache baadae baada ya kukupa laptop unanitext kuniuliza file ya movies ipo upande gani?! Unakaa na laptop yangu zaidi ya wiki hadi naanza kuiulizia na hapo bado utanambia sijui kuna mgeni kaja anacheki movie, anamalizia utaniletea!

Why mnakuwa waongo waongo watoto wa kike?!

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Bro.. thank you soo much for making my evening. Nimechekaa. Unawapata wapi hao watu? Umekutana nao wapi haswa?
Pole sana aisee... hata na kulala na mtu wa hivyo nayo yataka ujasiri. Hukuogopa? Hoping ulitumia protection...

Nilichojifunzaa ninkwamfano maybe basi huyu dada ni mdangaji alitakiwa hata kuonyesha efforts za kuwa a good girl hata kuamka na kuweka mazingira mapema asubuhi maybe hata ungemfikiria. Kitendo cha kuwa mvivu na kutofanya lolote na kuagiz vitu ndo lililokukera zaidi. Unamwaminije hata kumuacha mwenyewe ndani kwako.? Dont bwana. Nyumbani kwako ni pahali patakatifu sana. Wengine wana mikosi. Palinde sana. Bora mkamalizane mahotelini huko..

Ila kuwa halisia sisi imekua tatizo sana. Sijui tunaamini tukijiweka matawi sana ndo tutathaminika kwenye jamii hata sijui. Hivi ni huu utandawazi unatuharibu hv ama
 
Inategemea na ninae mpa sio kwamba sijawahi au huwa siazimishi. Kuna siku nilimuachia mtu gari ikarudi imevunjwa taa ya nyuma na alikuwa anaendesha sijui ni dogo gani, muhusika akapotea na simu alikuwa haupokei.

Nilikuja kukutana nae mwaka na baade kwa bahati mbaya sana Moshi, akaishia kunambia tuyazungumze anaomba msamaha hakujua atanambia nini hadi akaamua tu kuondoka....

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo nayo ni changamoto kiukweli.
 
Kuna rafiki yangu aliniambia, yeye anasoma Arusha Technical College (ATC).
course ya kuingiza nyimbo kwenye simu na flash. 😂😂😂. It is a very true story. Nilimhurumia sana kwa fix aliyonipiga.
 
Back
Top Bottom