Imagine mtu anaomba 300,000 halafu ukimtazama mkavu. Unatest zari unamwambia hebu chukua 50,000 kwanza wakati tunatafuta kwingine, utashangaa hatafuti ila anakukazia wewe utafute umpe.... Sasa unajiuliza mtu kama huyu hana vyanzo vingine, anatoboa vipi mishe zake mjini....?!Nimeishuhudia mara kadhaa sana. Ili mradi anakufahamu tu, hata kama hujawahi kuleta story za mahusiano kwake.
Wanatamani sana kujikweza.
Vizinga vyao na kuomba kuazima hela ambazo ukitazama uwezekano mkubwa ni ku'risk hela tu, maana haviendani na maisha wanayoishi.
Tuwavumilie na kiwasaidia tunapoweza.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Wanafanana wasome uone, tofauti yao ni mtoa mada anakuwa serious Sana kwenye mwandiko, huyo mpare yeye anakauli laini kiasi huwezi kushtuka hata akikutukana
Shekh kama kuna mtu alidanganya 2020/21 basi ni mimiHabarini wadau. Naandika hii kitu hapa baada ya kukerwa na tabia za baadhi ya mabinti especially hawa wamjini ambao wameanza kurithi tabia zile walizokuwa nazo wanaume za "kuna hela na isikilizia" halafu baada ya dakika kumi utasikia "una elfu tano au kumi ya karibu hapo".
Ipo hivi, kuna wadada kadhaa nimenotice wanahii tabia katika mazungumzo kukuaminisha wao ni watu wa mipango mikubwa. Na hata wanavyojiweka ni as if ni watu muhimu sana hapa mjini but ukweli wa mambo ni wabangaizaji wasio na mbele wala nyuma.
Kuna m'moja ameshakuwa na tabia ya kunicheki kuniomba kuniazima gari akisema ana wageni sijui wanakuja kutoka nje wanahitaji usafiri watakaotumia wakiwa hapa mjini.
Nikamkata nikamwambia twende nitakupeleka safari yako. Nimekwenda mchukua yupo na wenzake wawili, wanasema wanaenda serena kufika hapo serena wanaangaliana yale macho ya tumeumbuka, mimi nikaona wananipotezea muda maana waliniweka zaidi ya nusu saa hapo kwenye kiti sehemu ya kusubiria kisha mwenzake nisie mjua anakuja niomba ufunguo kuwa anaomba aende pale posta ATM mara moja kisha aniletee, nikamwambia ngoja twende sote na mimi nilikuwa naenda huko, tukaenda kufika pale CRDB anatoa toa macho (sidhani kama hata alitoa hela alipoingia kwenye ATM mule). Nikamrejesha serena kisha nikampigia mwenzake nikawaaga nikawaambia nina dharula nitawareje, sikurudi tena.
Mwingine kila nikichekiana nae story zake ni "kuna jamaa tuna contract nae katika ile kampuni yangu, hapa ndio naangalia contract inakaribia kuisha ili nionane nae tukasaini mkataba mwingine" ukimuuliza mnadeal na nini katika kampuni yako, ooooh apartments kwa foreigners, tuna import na kuexport bidhaa etc, halafu hapo hapo anakupiga kibomu cha msosi. Au anaomba umnunulie soda tena anachagua yeye anataka soda gani.
Mwingine nilishapiga hadi mashine, shida ikaja baada ya kumleta maskani. Ni mwanamke ambaye hana impact ndani ya nyumba ukiachia kukuomba hela ndogo ndogo bila utaratibu as if mission yake ni kuhakikisha hauna hata mia mfukoni.
Ukiachia kulala hadi saa nne asubuhi kulala tu kitandani anachat na kupiga simu za kuongea na mashost zake na hakuna la maana wanaongea zaidi ya kupeana umbea wa juzi waliposafiri au bata sijui kumuongelea mtu gani, hawana mazungumzo ya maana.
Ila mtu huyu huyu ukiongea nae anaongelea kuhusu kufanya kazi katika NGO iliyomlipa milioni 2. 7 take home na imefungwa kipindi cha magufuri.
Mara akwambie anasomesha wadogo zake international schools, na anamhudumia mama yake mwenyewe. Mara akwambie sijui anataka ajiajiri anataka kufungua kampuni ya beauty and cosmetic ambayo ataiweka kule masaki au oysterbay na inalipa sana. Mara aseme yeye ni CEO haoni haja ya kuajiriwa.
Ila ukitoka kwenda dukani nje, utaona text kutoka kwake imeingia beib, ukirudi niletee Cadbury bars mbili na maziwa ya asas au utasikia niletee sausages na apple juice ya ceres kubwa. Anaagiza hivi kwa confidence kabisa utadhani mimi ni babake.
Unakuta mpo kwenye foleni barabarani inapita vogue utasikia one day lazima nita own hii gari...... Nina rafiki yangu ana jaguar hii ya 2018 and she's only 25, yaani i must get there....
Sasa huwa nawatazama nasema hivi hawa ni kwamba hawaoni uhalisia wa maisha yao au ni vipi. Watu wana maisha ya kubangaiza, wanatoka katika very common families za kitanzania ambazo wazazi ni wastaafu na hawana hela.
Why mtu usiwe humble na kuishi according to your level requirements wakati unaplan kuwa mkubwa baadae....?!
Why uishi maisha ya kufake fake na uongo mwingi ile hali hauna uwezo na ni tegemezi by 150%?!
Kuna haja gani ya kunidanganya kuwa kuna report naandika mara sijui kuna email muhimu nataka nijibu hapa.... Au unanipigia simu au kunitext whatsapp baada ya kuniona online saa saba usiku halafu unanifix kuwa Atm imemeza card na hauna balance muda huo unaomba nikuazime 50,000 utanirejeshea asubuhi, halafu asubuhi ikifika unapiga kimya naona tu upo online unapost status unakaa kimya wiki, hatimae mwezi na miezi?!
Au unaniazima laptop unasema kuna a very serious work unahitaji kutype (hata haujulikani unajishughulisha na biashara gani mjini). Kisha nakupa tu bila ya kukuuliza swali lolote zaidi ya utaniletea lini, cha ajabu dakika chache baadae baada ya kukupa laptop unanitext kuniuliza file ya movies ipo upande gani?! Unakaa na laptop yangu zaidi ya wiki hadi naanza kuiulizia na hapo bado utanambia sijui kuna mgeni kaja anacheki movie, anamalizia utaniletea!
Why mnakuwa waongo waongo watoto wa kike?!
Sent using Jamii Forums mobile app
Yani tuogope miandiko yenu😂😂😂 Unachekesha Sana we mtoto,[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sasa mbona mnakuwa waoga tukiwapa makavu.... Eti?!
Sent using Jamii Forums mobile app
Kabisa mkuu naanza kuwa kauzu now nawachana live...Tatizo lipo KWAKO mkuu. Ur a very nice guy
And to the slay queens, a nice a guy is a foolish guy.
Anza kuwa rude and they will respect you big time
Ha ha ha ha ha [emoji23][emoji23][emoji23] sio tu mwanaume hata mzungu, mtu yoyote hatakiwi kuwa muongo muongo.....Hata Mwanaume akiwa muongo muongo ni kitu kibaya sana halafu haipendezi kabisa.
But huwa hatuna hizo swagga za kurequest wawe hivyo. Ni tofauti na mwanaume, unaweza kuwa na mwanamke anakwambia kabisa, me napenda mwanaume ambaye anaendesha gari bei fulani, anavaa suti anapesa benki.Wanajiupdate according to status mnazozitaka vijana wa kileo kwaiyo usiogope maana njia ya muongo ni fupi
Kingsmann
Ha ha ha ha ha ha [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] love of my life..... Ndio maana nadate na wewe tu.... Chuma changu cha nguvu....., [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]We unatoka wapi na hao wadada??wanakudanganya kwa jinsi wanavyokuona....huenda na ww ni muongo muongo so wananata na biti lako...[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Umbea huo kaone...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Si umeona watu wanavyofunguka...Wallah huu uzi hapana lol, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ama uongo brother [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Aisee [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Wengine wanakuwa wapo vizuri kweli ila hawana discipline ya pesa.Hii nilikutana nayo mwaka juzi, demu kanipeleka hadi kwao[emoji16][emoji16] pako vizuri saana, wanaishi ndani ya bonge la jumba huko kinyerezi.
Tulipozoeana akaanza vizinga vya kijinga.. mara baba yake anaumwa, mara baba yake kasafiri, pesa ya matumizi imeisha, mara mdogo wake alipiwe ada arudi shule ili baba yake akirudi atanirudishia [emoji3][emoji3][emoji3].
Mwanzoni nilisaidia pale nilipoweza ila nikagundua napigwa changa la macho.
Na bado ukasoma.... Mtizame kwanza ulivyo katili nyau wewe... [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kuna watu mnakuaga na muda mchafu wa kuandika jamani, yaan kabisa umelala kwenye kigodoro chako cha futi 2 na kuanza kuandika upupu,
Niandae ftari mie nisijewapandisha watu Muhaho.
Hiyo gari inakuwa gari kweli uliyonunua kwa jasho na kujinyima au inakuwa gari ya urithi.We jamaa inaonekana ni mtu wa kushikilia vitu vidogo vidogo pia una asili ya ubinafsi ndani yako. Be fair, mie mtu akihitaji gari yangu wala simuulizi unaenda wap wala nn.
Babu.... Kuna watu ukiongea nae ana kwa ana anaona kama unamuattack ila akisikia wengine wanazungumzia hiyo tabia ndio ubongo wake unaanza kufiriki sawa sawa. [emoji23][emoji23][emoji23]Umeandika kwa uchungu sana ila ni vizuri ukae naye na umwambie haya yote kuliko kuleta huku jukwaani maana wengine mazingira tunayoishi hakuna watu wa hivyo mkuu.
Bora mtu mtu anaetoa sumu kuliko anaevunga ni mstaarabu ile hali hapendi kinachotokea.Ana gubu pia,ana moyo flani ivi mdogo
Ha ha ha ha ha [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]hutaamini utakae kutana nae sio?!kuna hawa masistaduu wana unapicha makali kinoma kule insta na uko fesibuk hata apa jeief unachat na mdada adi akili inakukaa swsw, nenda sasa muonane uso kwa macho...salalleh
Hata mm huwa siwaelewagi kabisa,unajiuliza mtu kama huyo alikuwa anakudanganya kwa mantiki ipi labda au apate nin?,hakika unakosa majibu unabaki kucheka tuuKuna m'moja huyo, nilikutana nae kwenye stationary naona anasaidia kazi. Nikamuomba namba akanijibu mapema sana (ila usoni nikamuona tu huyu anajihami). Sikubembeleza nikakausha.
Kuna siku tukakutana nipo na gari ya rafiki yangu (harrier makalio ya nyani) nimekwenda nayo sokoni. Kuniona macho yakamtoka. Muda naondoka baada ya kununua vitu namuona ananipungia mkono. Nikampungia back kawaida tu nikaendelea na ratiba zangu.
Baada ya siku kadhaa at the same stationary, akaniona akaja haraka sana. Kufika akachukua simu yangu (kama utani hivi) kuishika inadai password. Akaniomba niweke password. Nikaweka akaweka namba zake akajipigia akanirejeshea simu yangu.
Picha ndio likaanza, akanitext usiku ule ule. Tukaanza kuchat. Huku na kule akaanza sasa story za kuonekana yeye yupo vema. Mara ananiambia ile stationary ni ya kwake yule ni mfanya kazi wake.
Mara ananiambia sijui hapa nasoma report ya biashara zangu, namuuliza biashara gani anahamisha magoli taratibu utasikia, "acha tu yaani biashara ni nyingi kwakweli, anyways leta story".
Hapo hapo mara aseme ana mambo mengi sana kichwani hadi anatamani kulewa ili apoteze mawazo, nimtoe out..... [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Namuuliza mambo gani yanakuzonga. Oooh wazazi wangu unajua wamefariki, sisi kwetu tupo watatu tu, sasa tumeachiwa nyumba zipo huko mbezi Beach, kijitonyama na tabata, mimi ndio nasimamia. Sasa sijazunguka kufanya ukaguzi.
Namuuliza wewe unaishi wapi kwan kwa sasa, ooooh nakaa tegeta. Kuna siku namtext upo wapi, anasema nipo tegeta, namuuliza upo home, anajibu ndio, nikamwambia nielekeze nakuja kukusalimia nipite njia gani, anaanza kuhamisha magoli, aaaah upo njiani unakuja tegeta au upo tegeta kabisa,namjibu nipo tegeta hapa wewe upo wapi, aaaah sawa ngoja basi nikupigie baada ya dakika 1 maana simu yangu inazima chaji ipo betry low, ngoja niichomeke kwenye chaji isizime...... kisha nikuelekeze.
Kubabake kwan alipiga tena.... Nikapiga simu kimya haiiti..... Nilicheka balaa siku ile.... [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app
Chawa kabisa mwamba chawa kama chawa.hawa ni wanawake machawa hawa hawana inshu ya maana mkuu,