Kuna m'moja huyo, nilikutana nae kwenye stationary naona anasaidia kazi. Nikamuomba namba akanijibu mapema sana (ila usoni nikamuona tu huyu anajihami). Sikubembeleza nikakausha.
Kuna siku tukakutana nipo na gari ya rafiki yangu (harrier makalio ya nyani) nimekwenda nayo sokoni. Kuniona macho yakamtoka. Muda naondoka baada ya kununua vitu namuona ananipungia mkono. Nikampungia back kawaida tu nikaendelea na ratiba zangu.
Baada ya siku kadhaa at the same stationary, akaniona akaja haraka sana. Kufika akachukua simu yangu (kama utani hivi) kuishika inadai password. Akaniomba niweke password. Nikaweka akaweka namba zake akajipigia akanirejeshea simu yangu.
Picha ndio likaanza, akanitext usiku ule ule. Tukaanza kuchat. Huku na kule akaanza sasa story za kuonekana yeye yupo vema. Mara ananiambia ile stationary ni ya kwake yule ni mfanya kazi wake.
Mara ananiambia sijui hapa nasoma report ya biashara zangu, namuuliza biashara gani anahamisha magoli taratibu utasikia, "acha tu yaani biashara ni nyingi kwakweli, anyways leta story".
Hapo hapo mara aseme ana mambo mengi sana kichwani hadi anatamani kulewa ili apoteze mawazo, nimtoe out..... [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Namuuliza mambo gani yanakuzonga. Oooh wazazi wangu unajua wamefariki, sisi kwetu tupo watatu tu, sasa tumeachiwa nyumba zipo huko mbezi Beach, kijitonyama na tabata, mimi ndio nasimamia. Sasa sijazunguka kufanya ukaguzi.
Namuuliza wewe unaishi wapi kwan kwa sasa, ooooh nakaa tegeta. Kuna siku namtext upo wapi, anasema nipo tegeta, namuuliza upo home, anajibu ndio, nikamwambia nielekeze nakuja kukusalimia nipite njia gani, anaanza kuhamisha magoli, aaaah upo njiani unakuja tegeta au upo tegeta kabisa,namjibu nipo tegeta hapa wewe upo wapi, aaaah sawa ngoja basi nikupigie baada ya dakika 1 maana simu yangu inazima chaji ipo betry low, ngoja niichomeke kwenye chaji isizime...... kisha nikuelekeze.
Kubabake kwan alipiga tena.... Nikapiga simu kimya haiiti..... Nilicheka balaa siku ile.... [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sent using
Jamii Forums mobile app