Mabinti wa kisasa hebu acheni uongo usio na maana

Mabinti wa kisasa hebu acheni uongo usio na maana

Wapo wengi
Ma slay queens[emoji28][emoji28]
Ngoja nisimulie kisa kimoja kuna dada nilikutana nae vowet kulikuwa na maonyesho ya bidhaa na Mimi nilipeleka bidhaa zangu yeye tulijuana alikuwa ni jirani kwangu kwenye meza yake picha linaanza ameweka bidhaa sio zake ni brand name ya mtu mwingine ambae mimi namjua akanidanganya ni bidhaa yake mwenyewe nikaguna ila nikapotezea,tuka exchange number tukawa close alinizoea haraka sana akajua ninapo ishi nika mu introduce kwa circle yangu tena marafiki zangu wa maana kabisa,sad alikuja kutuvurugaa duh mpaka leo tumesambaratika
Aliwakopa hela alikuwa muongo ana project nyingiii za kufikirika
Mpaka leo sijui hata alikuwa anaishi wapi najua sinza madukani ila mtaa upi sijui nilikuwa naonana nae kituoni
Alikuwa na baba wawili kwa mtoto mmoja yani maisha yake mvurugiko mpaka huruma sijui alikuwa anapata nini kwa uongo uongo
So mleta mada nakuelewa
Nadhani huwa ni namna ya kuvutia watu waonekane ni high profile people kumbe hamna kitu
Wanaume wanao penda mtelezo ukijichanganya kwa wadada kama hawa you’re finished
Unaanzaje kumtambulisha mtu kwa watu wa circle yako wakati mwanzo tu kaanza kukudanganya!?
 
Habarini wadau. Naandika hii kitu hapa baada ya kukerwa na tabia za baadhi ya mabinti especially hawa wamjini ambao wameanza kurithi tabia zile walizokuwa nazo wanaume za "kuna hela na isikilizia" halafu baada ya dakika kumi utasikia "una elfu tano au kumi ya karibu hapo".

Ipo hivi, kuna wadada kadhaa nimenotice wanahii tabia katika mazungumzo kukuaminisha wao ni watu wa mipango mikubwa. Na hata wanavyojiweka ni as if ni watu muhimu sana hapa mjini but ukweli wa mambo ni wabangaizaji wasio na mbele wala nyuma.

Kuna m'moja ameshakuwa na tabia ya kunicheki kuniomba kuniazima gari akisema ana wageni sijui wanakuja kutoka nje wanahitaji usafiri watakaotumia wakiwa hapa mjini.

Nikamkata nikamwambia twende nitakupeleka safari yako. Nimekwenda mchukua yupo na wenzake wawili, wanasema wanaenda serena kufika hapo serena wanaangaliana yale macho ya tumeumbuka, mimi nikaona wananipotezea muda maana waliniweka zaidi ya nusu saa hapo kwenye kiti sehemu ya kusubiria kisha mwenzake nisie mjua anakuja niomba ufunguo kuwa anaomba aende pale posta ATM mara moja kisha aniletee, nikamwambia ngoja twende sote na mimi nilikuwa naenda huko, tukaenda kufika pale CRDB anatoa toa macho (sidhani kama hata alitoa hela alipoingia kwenye ATM mule). Nikamrejesha serena kisha nikampigia mwenzake nikawaaga nikawaambia nina dharula nitawareje, sikurudi tena.

Mwingine kila nikichekiana nae story zake ni "kuna jamaa tuna contract nae katika ile kampuni yangu, hapa ndio naangalia contract inakaribia kuisha ili nionane nae tukasaini mkataba mwingine" ukimuuliza mnadeal na nini katika kampuni yako, ooooh apartments kwa foreigners, tuna import na kuexport bidhaa etc, halafu hapo hapo anakupiga kibomu cha msosi. Au anaomba umnunulie soda tena anachagua yeye anataka soda gani.

Mwingine nilishapiga hadi mashine, shida ikaja baada ya kumleta maskani. Ni mwanamke ambaye hana impact ndani ya nyumba ukiachia kukuomba hela ndogo ndogo bila utaratibu as if mission yake ni kuhakikisha hauna hata mia mfukoni.

Ukiachia kulala hadi saa nne asubuhi kulala tu kitandani anachat na kupiga simu za kuongea na mashost zake na hakuna la maana wanaongea zaidi ya kupeana umbea wa juzi waliposafiri au bata sijui kumuongelea mtu gani, hawana mazungumzo ya maana.

Ila mtu huyu huyu ukiongea nae anaongelea kuhusu kufanya kazi katika NGO iliyomlipa milioni 2. 7 take home na imefungwa kipindi cha magufuri.

Mara akwambie anasomesha wadogo zake international schools, na anamhudumia mama yake mwenyewe. Mara akwambie sijui anataka ajiajiri anataka kufungua kampuni ya beauty and cosmetic ambayo ataiweka kule masaki au oysterbay na inalipa sana. Mara aseme yeye ni CEO haoni haja ya kuajiriwa.

Ila ukitoka kwenda dukani nje, utaona text kutoka kwake imeingia beib, ukirudi niletee Cadbury bars mbili na maziwa ya asas au utasikia niletee sausages na apple juice ya ceres kubwa. Anaagiza hivi kwa confidence kabisa utadhani mimi ni babake.

Unakuta mpo kwenye foleni barabarani inapita vogue utasikia one day lazima nita own hii gari...... Nina rafiki yangu ana jaguar hii ya 2018 and she's only 25, yaani i must get there....

Sasa huwa nawatazama nasema hivi hawa ni kwamba hawaoni uhalisia wa maisha yao au ni vipi. Watu wana maisha ya kubangaiza, wanatoka katika very common families za kitanzania ambazo wazazi ni wastaafu na hawana hela.

Why mtu usiwe humble na kuishi according to your level requirements wakati unaplan kuwa mkubwa baadae....?!

Why uishi maisha ya kufake fake na uongo mwingi ile hali hauna uwezo na ni tegemezi by 150%?!

Kuna haja gani ya kunidanganya kuwa kuna report naandika mara sijui kuna email muhimu nataka nijibu hapa.... Au unanipigia simu au kunitext whatsapp baada ya kuniona online saa saba usiku halafu unanifix kuwa Atm imemeza card na hauna balance muda huo unaomba nikuazime 50,000 utanirejeshea asubuhi, halafu asubuhi ikifika unapiga kimya naona tu upo online unapost status unakaa kimya wiki, hatimae mwezi na miezi?!

Au unaniazima laptop unasema kuna a very serious work unahitaji kutype (hata haujulikani unajishughulisha na biashara gani mjini). Kisha nakupa tu bila ya kukuuliza swali lolote zaidi ya utaniletea lini, cha ajabu dakika chache baadae baada ya kukupa laptop unanitext kuniuliza file ya movies ipo upande gani?! Unakaa na laptop yangu zaidi ya wiki hadi naanza kuiulizia na hapo bado utanambia sijui kuna mgeni kaja anacheki movie, anamalizia utaniletea!

Why mnakuwa waongo waongo watoto wa kike?!

Sent using Jamii Forums mobile
Kweli JPM aliwatia adabu watanzania, kipindi cha JK wengi wadada walikuwa wanategemea waume za watu wenye pesa, wengi walikuwa nyumba ndogo , mzee baba alivyoingia michongo na wizi wote kwishinei, wadada wakawa Kama kuku waliofunguliwa kwenye Banda lao, nyumba ndogo zote zikaisha. Mambo ya uongo uongo yakaanza hili kusogeza maisha.
 
Ila mbona mimi toka primary napiga boarding mpaka chuo naishi hostel na sijawahi kuwa influenced na yeyote?
Nadhani ni ulimbukeni wao plus malezi... maisha ya kuigiza ni ujinga sana. Siku za sikukuu mf. Nilikua nalala zangu room hostel kimyaa hata christmas[emoji28] yaan sishtuki. Club tukienda sitaki kibambiwa. Simple. Ninprincipals tu

Naomba nafasi mrembo tufanye maisha
 
Hahahahaja kuna jamaa hapo juu kasema ndege wafananao?!,kwanin yy tuu ila teseme mabinti wenye tabia za hivyo wapo baadhi hata ww unaweza kukutana nae,umdhaniaye kumbe sio man

sijakataa kukutana nae ila ntakavyomchenga hataamini me sipendag usanii inapokuja swala la maisha
 
Nilimpa mtu gari ameniaga anaenda mchukua demu wake airport kisha ananiletea. Kuja akaja na mdada ila hawana muonekano kama mtu aliyetoka safari inaonekana alikwenda mzoa mtaa wa pili.

Mimi sikuwa na pressure akaniomba kuwa anampeleka kwao kisha atakuja. Nikamwambia poa haina shida.

Akaenda akapotea anakuja nitafuta saa kumi na mbili asubuhi. Na hapo amefanya kunitumia text kuwa eti jana alipoenda alichelewa kutoka so akaona asinisumbue usiku akaenda kulala na gari ili aniletee asubuhi mapema.

Nikamwambia haina noma kama vipi we utanicheki tu ukishafika me nipo macho. Akaja mida ya saa mbili kasoro story nyingi nikaona vijana uhuni mnajifunza kwa kuchelewa sana halafu kwa wandewa. Nikamuitia bodaboda akasepa.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app

aisee ashawah mtu chukua chuma akasema anaenda kibaha akaenda tabora akapiga nayo mbanga mbaya sana alafu gari nilijibana kweli harrier tako la nyani nikauza nikanunua kialteza siji kusahau maisha yangu yote na urafiki tuliuua
 
Bibie pls njoo pm tuyajenge
Jaribuni kuwaepuka mademu wanaovaa hivi viatu,hakika mtakuja kunikumbuka
JamiiForums-1132086857.jpg
 
Mimi nina shughuli na ina eleweka hata mtu akitaka jua ofisi yangu nampeleka na ananiona kabisa ni muajiriwa na nina shughuli zangu.

Ila hapa kuna agenda ya tabia ya kuongea uongo uongo ili uonekane wewe upo vizuri ile hali uwezo hauna. Why sasa udanganye na kupiga sound?!

Me watu wa hivi akiniomba hata buku simpatii maana nahisi ananichora.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu umeeleweka kabisa, sema watu wanataka kuwatetea tabia mbaya maana nao ni mumo humo
 
Back
Top Bottom