Uchaguzi 2020 Mabomu ya machozi yarindima Iramba Magharibi

Uchaguzi 2020 Mabomu ya machozi yarindima Iramba Magharibi

Ahaaaa ahaaaa nimecheka ile mbaya. Huwa unaleta post ndefu hapa jukwaani na kiingereza cha English course, niliwahi kukuambia kila kitu kina wakati wake. Ccm ni chama cha kizazi kilichopita, sio kwamba ccm haijafanya kitu, bali hiki sio kizazi cha ccm bali ni kizazi tofauti. Namna pekee ya kuifanya ccm iendelee kukaa madarakani sio kuleta maendeleo, bali ni kutumia vyombo vya dola kushurutisha kukaa madarakani.

Ccm naifananisha na mwanamke mzee anayejipamba ili kuvutia wanaume. Kimsingi hawezi kuvutia wanaume, bali itabidi atumie, pesa, ushirikina na mbinu nyingine chafu ili akubalike. Na kimsingi hatukubalika bali ataliwa pesa zake, na bado wanaume watapenda wanawake wenye umri mdogo. Hali ya ccm kupambana na ukweli inazidi kuwa wazi, na kudhibitisha kuwa wakati ni ukuta.
Katibu wao alithibitisha hilo

Ova
 
Mabomu ya machozi yanarindima wakati huu jimbo La Iramba Magharibi mkoani Singida ambapo Mgombea ubunge jimbo hilo kupitia CHADEMA Bi Jesca Kishoa inasemekana amekamatwa na kufungiwa ofisi za msimamizi wa uchaguzi.

Chanzo cha mabomu hayo kinadaiwa kuwa ni vurugu zilizotokea baada ya kutokea mabishano makali kati ya mgombea huyo na Msimamizi wa Uchaguzi, Inadaiwa kuwa JESCA KISHOA alimwekea pingamizi mgombea mwenzake kupitia CCM, Dkt Mwigulu Nchemba na mpaka sasa msimamizi amekataa kutoa majibu yake. Hali ya kukataa kutoa majibu ya pingamizi imepelekea hasira kwa mgombea huyo pamoja na wafuasi wake na ndiyo chanzo cha kuzuka kwa vurugu.

Mwingulu mwenyewe hilo siyo jina lake ni jina la vyeti vya kununua kisha akaendelea kusomea Elimu ya juu mmiliki wa vyeti ni Msukuma na huko singida hawana ukoo wala jina hilo
 
Bomu huwa halivunji kiu ya mtu,ila linamrudisha tu nyuma kwa hatua fulani na kumfanya kuwaza mbinu bora ya kutumia mbadala wa mdomo.
Mbinu bora ni kuwasomea Albadiri wakurugenziccm wale wote wenye kuendekeza figisu figisu uonevu kwa wapinzani
 
Vurugu zinaletwa na Tume sio Chadema kuwa muelewa,,,WANAKATWA BILA ISSUE ZA MSINGI,,,UNATAKA WAKUBALI HUJUMA KAMA KONDOO MKUU KAMA WEWE NI MWOGA WAOMBE TUME WATENDE HAKI NDO SULUHISHO WANAVYO IFANYIA CCM WAIFANYIE NA CHADEMA HIVYO HIVYO,,,VINGINEVYO AWAMU HII KINANUKA NA HUTA AMINI UVUMILIVU SASA BASII
Uonevu unyanyasaji wa CCM ndiyo chanzo kikuu cha vurugu
 
Mbinu bora ni kuwasomea Albadiri wakurugenziccm wale wote wenye kuendekeza figisu figisu uonevu kwa wapinzani
😁😁😁 Mkuu Shehe Sharrifu Majini Ameongea Leo kuwa ana ANTIDOTE ya Kuzuia ALBADR umemsikia akiongelea Kabla Clouds FM haijaanza Yale matangazo ya kuomba msamaha kwa Kosa walilofanya.....
 
Tanzania siyo kisiwa cha Amani tena bali ni Nchi ya wavumilivu wa vurugu za CCM inayofanya kazi kwa kukariri zidumu fikra zisizo sahihi za mwenyekiti wa CCM
 
Kwa jinsi nchi hii ilivyo kubwa,sidhani kama kuna Polisi wa kutosha kudhibiti maelfu ya wapinzani wa nchi hii.

Wacheni tufike wanakotaka kutufikisha labda ndio heshima itafuata.

Bwani fulani Jumapili huyo kanisani anasahau Mungu hadhihakiwi.
Sababu ya madaraka ndio maana unaombea nchi yako mabaya? Ndio ulafi wa wapi huo??
Madai ya mtu wako au mapenzi wako , haimaanishi kama ni kweli, hivyo vita subiri tusikie taarifa za pande zote.
Au as mtu wa Kati
 
Tanzania siyo kisiwa cha Amani tena bali ni Nchi ya wavumilivu wa vurugu za CCM inayofanya kazi kwa kukariri zidumu fikra zisizo sahihi za mwenyekiti wa CCM
Yaani vurugu zote hizi kisa fisi kanyimwa mifupa.au anaelekea kuukosa mifupa
 
Mabom hayajawahi kuwa suluhu ya aman, bali haki ndio nguzo kuu ya Iman, ccm wanaotetea amani hawatetei haki, sisi tunaotetea haki tunambiwa tunafanya uchochezi wa kuvuruga amani, msingi au ngozo ya amani ni haki nasivinginevyo.
Tume nao kimya kama hawapo
 
Wananchi wakiji-organise usiku huu, tunaweza ongea mengine.
Mlikosea sana kumwekea pingamizi JPM na Lipumba wakati nyie hampendi mapingamizi na mnajua kabisa mapingamizi na mchezo mchafu halafu mnatumia mbinu hizo hizo za kidhalimu.

Hata hivyo bado Wakurugenzi madhalimu wanafurahia udhalimu wao huku wanaopinga udhalimu wakikamatwa na kuziacha familia zao zikiteseka.
Hapo kila mkurugenzi lazima awe udhalimu mana udhalimu umeonekana kuwa unalipa.

Kuna siku nilimsikia Siro akisema kuwa uhalifu haulipi mana atakayejaribu tu watamshughulikia ipasavyo.
Sasa Wakurugenzi wamegeuka kuvunja sheria kwa maslahi yao binafsi na hawajashughulikiwa ipasavyo ndio maana wanapeana mbinu za kihalifu zaidi kila kukicha ili wapate vyeo na pesa toka kwa wagombea wa CCM. Hapo bado suala la kuwaengua wapiga kura linakuja na kugeuza matokeo na hata kuyafuta.
Kama watazidi kuachwa na kuendelea kunafaika na udhalimu wao hakika hata 2025 wataendelea na utaratibu huo huo na wapinzani watakua hoi.

Wajerumani walikimbia mashamba ya Pamba Kusini baada ya Wamatumbi kupambana na udhalimu wa wakoloni Wajerumani kwa kutia moto mashamba yao ya pamba na kung'oa miche ya pamba.

Tume ya Taifa na mahakama ya Rufaa imewakosea sana watanzania kwa kupuuza Kesi ya kikatiba iliyofunguliwa kupinga Wakurugenzi kusimamia uchaguzi. Hii nchi lolote litakalotokea lakini kuna watu wa kulaumiwa moja kwa moja ambao wanasimamia sheria kwa kufuata matakwa ya nafsi zao na maslahi yao bila kujali umoja na mshikamano wetu.

Tunaiomba Tume iwarejeshe Wagombea wote ili wananchi wampige kura wachague viongozi wao wanaowapenda.
Tume itupilie mbali mapingamizi yote kama ilivyotupa ya wagombea urais.
 
Hii mabomu kila soku kuja kufika siku ya uchaguzi si police watakuwa wameishiwa mabomu?
 
Mabomu ya machozi yanarindima wakati huu jimbo La Iramba Magharibi mkoani Singida ambapo Mgombea ubunge jimbo hilo kupitia CHADEMA Bi Jesca Kishoa inasemekana amekamatwa na kufungiwa ofisi za msimamizi wa uchaguzi.

Chanzo cha mabomu hayo kinadaiwa kuwa ni vurugu zilizotokea baada ya kutokea mabishano makali kati ya mgombea huyo na Msimamizi wa Uchaguzi, Inadaiwa kuwa JESCA KISHOA alimwekea pingamizi mgombea mwenzake kupitia CCM, Dkt Mwigulu Nchemba na mpaka sasa msimamizi amekataa kutoa majibu yake. Hali ya kukataa kutoa majibu ya pingamizi imepelekea hasira kwa mgombea huyo pamoja na wafuasi wake na ndiyo chanzo cha kuzuka kwa vurugu.

View attachment 1550284

View attachment 1550159
Mwigullu anaogopa mama tumbili?
 
Hii ndiyo Serikali inayodai kuwa ni ya wanyonge na eti uchaguzi Mkuu utakuwa huru na haki. Hovyooo.
 
Nadhani vurugu zinatokana na kukosa haki. Moja kwa moja unafahamu ni wakina nani waanzilishi wa vurugu
 
Back
Top Bottom