JUAN MANUEL
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 7,808
- 16,972
Hata ningekuwa Mimi ningekasirika,Ni kwa mara nyingine tena watanzania bara tunaotumia nguvu kubwa kulazimisha undugu kwa Wazanzibari tumeangukia pua ππ
Mabondia wa Zanzibar wakataa pambano la kimataifa la Mwakinyo kufanyika Zanzibar, watia msisitizo mapambano ya Zanzibar yawe fursa kwa wazanzibari tu na sio ya Watanzania Bara,
Bondia Hassan Mwakinyo (27) ambaye anajiandaa na pambano lake dhidi ya Bondia Mmarekani Peter Dobson (32) ambalo limepangwa kufanyika December 30,2022 katika Uwanja wa Mao Tse Tung, Zanzibar, ameelezea masikitiko yake kwa kile alichodai Mabondia wa Zanzibar wameandika barua wakidai hiyo ni fursa ya Wazanzibar na sio ya Watanzania Bara.
Pambano hilo la Mwakinyo vs Mmarekani Dobson ni la kugombania mkanda wa WBC International Super Welter.
Mwakinyo amesema βBaada ya miaka mingi kupita nimekuwa mstari wa mbele sana kuipambania Boxing ya Zanzibar mpaka kufanikiwa kupata ridhaa kupitia Mh. Rais wa Zanzibar na Baraza lake kupata kibali cha kufanya fight ajabu ni kwamba Boxer wa Zanzibar wasioona ukubwa wa hili jambo wameandika barua wakidai ile ni fursa yao Wazanzibar na sio ya Watu wa Tanzania Bara so hawataki tujihusishe naoβ
βNa sasa sijui ikisemwa kuwa kuna Muungano uliopo kati yetu Muungano huo unaunganisha kitu gani anyway kila la kheri Mabingwaβ
Ukiangalia timu ya Taifa ya mpira,wamejaa wa bara,timu ya Taifa ya riadha,imejaa wa bara,ya uogeleaji,wabara watupu,viongozi wote wa vyama vya michezo,ni wabara!Zenj hawasikiki kabisa!!
Kipindi kile Cha big brother Africa,wazenj hio fulsa huwa hawapati!!!
Huu Muungano umekaa vibaya sana