Mabondia wa Zanzibar wakataa pambano la kimataifa la Mwakinyo kufanyika Zanzibar, watia msisitizo mapambano ya Zanzibar yawe fursa kwa wazanzibari tu

Mabondia wa Zanzibar wakataa pambano la kimataifa la Mwakinyo kufanyika Zanzibar, watia msisitizo mapambano ya Zanzibar yawe fursa kwa wazanzibari tu

Ni kwa mara nyingine tena watanzania bara tunaotumia nguvu kubwa kulazimisha undugu kwa Wazanzibari tumeangukia pua 😂😂

Mabondia wa Zanzibar wakataa pambano la kimataifa la Mwakinyo kufanyika Zanzibar, watia msisitizo mapambano ya Zanzibar yawe fursa kwa wazanzibari tu na sio ya Watanzania Bara,

Bondia Hassan Mwakinyo (27) ambaye anajiandaa na pambano lake dhidi ya Bondia Mmarekani Peter Dobson (32) ambalo limepangwa kufanyika December 30,2022 katika Uwanja wa Mao Tse Tung, Zanzibar, ameelezea masikitiko yake kwa kile alichodai Mabondia wa Zanzibar wameandika barua wakidai hiyo ni fursa ya Wazanzibar na sio ya Watanzania Bara.

Pambano hilo la Mwakinyo vs Mmarekani Dobson ni la kugombania mkanda wa WBC International Super Welter.

Mwakinyo amesema “Baada ya miaka mingi kupita nimekuwa mstari wa mbele sana kuipambania Boxing ya Zanzibar mpaka kufanikiwa kupata ridhaa kupitia Mh. Rais wa Zanzibar na Baraza lake kupata kibali cha kufanya fight ajabu ni kwamba Boxer wa Zanzibar wasioona ukubwa wa hili jambo wameandika barua wakidai ile ni fursa yao Wazanzibar na sio ya Watu wa Tanzania Bara so hawataki tujihusishe nao”

“Na sasa sijui ikisemwa kuwa kuna Muungano uliopo kati yetu Muungano huo unaunganisha kitu gani anyway kila la kheri Mabingwa”
Hata ningekuwa Mimi ningekasirika,
Ukiangalia timu ya Taifa ya mpira,wamejaa wa bara,timu ya Taifa ya riadha,imejaa wa bara,ya uogeleaji,wabara watupu,viongozi wote wa vyama vya michezo,ni wabara!Zenj hawasikiki kabisa!!
Kipindi kile Cha big brother Africa,wazenj hio fulsa huwa hawapati!!!
Huu Muungano umekaa vibaya sana
 
Muungano unasaidia kuongeza idadi ya watu. Watu ni soko. Watu wengi maana yake soko kubwa la bidhaa
nina haja kweli ya kujibu hiki ki hoja?

vita vyetu si dhidi ya damu na nyama... let me move on
 
Wanzanzibar ni watu wabaguzi sana nimeishi NAo mazingira ya Bata huku kwanza ata ki.mahusiano wabaguzi utasikia uyu mbara kumbe hawajui nature Yao nikutoka huku Bara slave trade wanyamwezi wengi asili Yao na wasukuma wanzanzibar weusi ma waliozaliana na waarabu Cha ajabu awajui nature Yao ni wapi kumbe vizazi vyao vilianzia huku vikasafirishwa na mwarabau utasikia.mi mpemba ....nature yake hajui KWAIYO sio watu wakiwashangaa sana
 
Msimu wa sikukuu huu Zanzibar wageni kama wote so mwakinyo akaona aitumie Fursa ila sasa ndo hivyoo Wazanzibar choyooo imewakabaaa...!! Aje tu kupigania Daslaaaa.
 
Hapa wa kwanza kuona aibu ni waziri wa michezo zanzibar na ilitakiwa baada ya kuipokea hiyo barua hata asiijibu
Ngoja nimtafute huyo muhusika na watu wa baraza la sanaa niwape neno la kuwqfungua akili
 
Hata ningekuwa Mimi ningekasirika,
Ukiangalia timu ya Taifa ya mpira,wamejaa wa bara,timu ya Taifa ya riadha,imejaa wa bara,ya uogeleaji,wabara watupu,viongozi wote wa vyama vya michezo,ni wabara!Zenj hawasikiki kabisa!!
Kipindi kile Cha big brother Africa,wazenj hio fulsa huwa hawapati!!!
Huu Muungano umekaa vibaya sana
Unaweza kuwa na hoja lakini ni nyepesi. Huko visiwani kuna matatizo mengi na la msingi ni uislam wa kimya kimya ni mwingi. Kama Mwalimu Nyerere asingeitumia nguvu kuikataa hoja ya OIC ya kuigeuza Zanzibar kuwa nchi ya kiislam leo hii Nchi nzima ingekuwa imetumbukia katika matatizo yale yale yanayoitesa Nigeria.

Kuna mbegu ya kibaguzi huwa inapandwa na kusimamiwa na wanasiasa na inasumbua sana wananchi. Suala la michezo kudumaa ni hayo hayo masuala ya kukataa udhamini wa kampuni za pombe (kigezo ni kile kile cha uislam uliojificha), vipaji vipo vingi sana mfano Fei Toto na yule kiungo mmoja alicheza timu ya vijana ya Unguja miaka ile ya copa coca cola lakini pesa za udhamini ndio hizi zinasusiwa.

Mkwamo wa visiwa hivyo unaanzia huko huko.
 
Kuna mambo yanachekesha sana...wazanzibar sidhani kama wengi wanajitambua
 
1 Ikiwa unafikiria Wazanzibari wamejaa Bara nakushauri upande boti uende Zanzibar halafu uje uandike tena.

2. Nashangaa watu wanatoka povu sababu tu Mwakinyo kaandika alivyoandika bila ya watu kujaribu kutafuta ukweli uko wapi? Who the fck is Mwakinyo? Huko UK na kwengineko alikokwenda kupigana kwani tumeungana nao. You dont need to be united to fight in a country. Its strictly business.

Wacheni kubweka jaribuni kutafuta undani wa sababu ya yeye kukataliwa ku fight in Zanzibar if ever thats the case!
Nyie huku mnazaaana kama nguruwe na mnamiliki Hadi aridhi na mashamba.

Watanganyika wangapi wanaomiliki aridhi Zanzibar . ?

Acheni roho mbaya

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Cha ajabu wahusika ni boxers unashangaa hawajui faida ya pambano kufanyika zanzibar.
1. Kuitangaza zanzibar
2. Kuifungua zanzibar boxing
3. Kiuchumi-wageni watashuka zenj kushuhudia pambano.
4. Ongea mengine
Mwakinyo asipopigana hiyo nafasi haiendi kwa mwingine itapotea.
Mola alijalie pambano hilo wajifinze kutafuta fursa.
Zanzibar hiyo michezo ya kitwana haikuwahi kuwepo na ilikatazwa na serikali. Niliwahi kusema na ntaendelea kusema Watanganyika msiokua na kazi maalumu kule Zanzibar mtaendelea kunyooshwa mpaka museme nini hiki. Na kama huamini nenda kule Zanzibar alafu angalia mtanganyika akifanya kosa hata kwa bahati mbaya wanavyomfakamia 😂😂
 
Back
Top Bottom