Getrude Mollel
JF-Expert Member
- Apr 26, 2022
- 270
- 362
Serikali ya Rais Samia Suluhu iliwekeza kiasi cha TZS 157.8bn/- mnamo mwaka 2021 kwa lengo la kuboresha uwezo wa bandari ya Mtwara ikiwamo kuongeza kina cha bahari ili iweze kupokea meli zinazoweza kubeba shehena kubwa zaidi za mizigo.
Baada ya ujenzi huo kukamilika mapema mwaka huu, bandari hiyo imeanza kuzaa matunda. Uwezo kwa kusafirisha mizigo kutoka nje umeimarika mara mbili zaidi ya uwezo wa awali. Takwimu za kati ya Januari 2022 hadi Juni 2022 zinaonesha kwamba tani 592,365 za mizigo zimesafirishwa kupitia bandari hiyo ambapo ni sawa na ongezeko la 56.83%
Takwimu zinaoesha kwamba kwa mwaka 2020/21, kabla ya maboresho yaliyofanyika, bandari hiyo ilisafirisha tani 177,388.
Meneje anayekaimu bandari ya Mtwara kwa sasa, Bw. Narbeth Kalembwe amesema kwamba makisio ya usafirishaji wa bandari hiyo ilikuwa ni tani 377,770 kwa mwaka, lakini ndani ya muda mfupi tangu kukamilika kwa bandari hiyo, tayari bandari hiyo imeonesha uwezo mkubwa sana katika kusafirisha mizigo.
Ongezeko hilo kubwa la usafirishwaji wa shehena kubwa wa mizigo limechangiwa na ongezeko la usafirishwaji wa makaa ya mawe kwa wingi kwenda nchi za India, Ghana, Senegal na Misri.
Kabla ya matengenezo, bandari hiyo ilikusanya mapato ya kiasi cha TZS 11bn/- kwa mwaka 2020/21, huku kati ya Januari - June 2022, bandari hiyo tayari imeshakufanya TZS 23bn/-.
Hapo awali kabla ya matengenezo bandari hiyo iliweza kuhimili tani 400,000 tu za miziog kwa mwaka. Hivi sasa, bandari hiyo itaweza kuhudumia mizigo tani 1,000,000 kwa mwaka.