Kumekuwako na hali ya kujitokeza kwa matukio ya ukatili wa kijinsia na watoto, upotofu wa maadili pamoja na vifo vya wanafamilia, mke, mume, Watoto ama wanandugu wakati mwingine bila sababu zinazofahamika na ama pia kwa sababu zilizo wazi jambo linalopelekea kuibuka kwa tafrani, simanzi na hata kuacha hasara kwa ndugu, jamaa na Taifa kwa ujumla. Mojawapo ya sababu kuu za uwepo wa matukio haya ni pamoja na:
Kutokana na maelezo machache yaliyotangulia hapo juu, lakini pia kwa kuzingatia hatua mbalimbali zinazoendelea kutekelezwa na wadau pamoja na Serikali kwa ujumla wake katika kukabiliana na changangamoto hizi, ufuatao ni ushauri ama mkakati wa namna ya kukabiliana nazo kupitia idara za Ustawi na Maendeleo ya Jamii.
Ni pamoja na:
Ikumbukwe kuwa familia ndiyo msingi mkuu wa awali wakimalezi kwa jamii yoyote na hivyo kukiwa na mkakati wa kitaifa unaolenga kuimarisha maadili, malezi na usalama wa familia niwazi kwamba kutakuwa na mambo chanya:
Njia hii ya kujumuisha ustawi na maendeleo ya jamii katika kukabiliana na changamoto tajwa inalenga kutumia huduma za kifamilia kama njia kuu itakayosaidia kuzifikia familia ambazo zina matatizo. Familia zinaweza kupangiwa ratiba namna ya kuzifikia ili kupatiwa huduma mbalimbali.
Muhimu katika mkakati huu ni kuhakikisha kwamba maafisa hawa wanapata mafunzo mengi na endelevu katika kuutekeleza ili kuzirejesha familia katika misingi inayokubalika.
Njia hii itasaidia kung’amua aina nyingi za migogoro ambayo inaweza kuwa hatarishi kabla ya kuleta madhara miongoni mwa wanafamilia. Pia ikumbukwe kuwa baadhi ya wanafamilia walio wengi hasa wahanga huwa na siri za mambo mbalimbali ambayo pia huwa ni viashiria vya kutokea kwa madhara lakini hawajui wachukue hatua gani.
Idara hizi zipewe kipaumbele cha kufika katika ngazi za familia kwani zinatambulika na wanakaya walio wengi, nani idara zihusuzo maendeleo na ustawi wa kaya. Maafisa hawa endapo wakipewa jukumu hili litakuwa ni jukumu la kimfumo linaloeleweka na lenye utaratibu na miongozo. Kuna taasisi nyingine za kijamii ambazo zinashiriki katika kurekebisha, kukemea, kulea kimwili na kiroho kama dini lakini zinakosa misingi na mamlaka ya kimuongozo na kimuundo katika kuzisimamia na kuziongoza familia na pia si wanafamilia na kaya zote huweza kuhudhuria ibada ili kupata mafunzo ya malezi. Pia si kaya zote zinaamini katika dini, nyingine ni wapagani wasiofika katika nyumba za ibada wanamifumo mingine ya imani inayowaongoza. Vivyohivyo kwa viongozi wa kimila, wanayo nafasi ya kushiriki katika mpango huu na baadhi wameendelea kufanya vyema katika uondoshwaji wa baadhi ya mila zinazoonekana kuwa vyanzo vya ukatili na usababishaji vifo. Kwa Taifa letu la Tanzania, idara zinazoweza kulibeba jukumu hili ni mbili, Ustawi na Maendeleo ya jamii huku taasisi kama za dini, wazee wakimila na Wizara nyinginezo zikilibeba jukumu hili pale watakapoweza kuliweweka katika mipango na mikakati yao.
- Uwepo wa hali ya vitendo vya ukatili wa kijinsia
- Misongo ya mawazo na magojwa ya kiakili
- Uwepo wa migogoro na wivu kimahusiano
- Hali duni za kiuchumi
- Kukosa mazingira ya kiushauri nasihi kwa baadhi ya changamoto
- Baadhi ya mamlaka nyinginezo kutotimiza wajibu na majukumu yao
- Uchukuaji wa sheria mikononi na sababu nyinginezo.
Kutokana na maelezo machache yaliyotangulia hapo juu, lakini pia kwa kuzingatia hatua mbalimbali zinazoendelea kutekelezwa na wadau pamoja na Serikali kwa ujumla wake katika kukabiliana na changangamoto hizi, ufuatao ni ushauri ama mkakati wa namna ya kukabiliana nazo kupitia idara za Ustawi na Maendeleo ya Jamii.
- Kuanzisha kazi za familia kwa maafisa Ustawi na afisa maendeleo. Pamoja na majukumu yao yakimsingi, maafisa hawa wanaweza kuongezewa majukumu ili kuwaleta jirani na familia. Chini ya mpango huu watafanya yafuatayo:
- Wataweza kutoa elimu, kufanya vipindi na kupata taarifa ngazi ya familia, vitongoji, mitaa na kata na kuzibadili familia zilizo na changamoto za kimalezi, migogoro, upotofu wa maadili, watoto mitaani, utoro mashuleni, kutowajibika kwa wazazi, utelekezaji wa watoto, ukatili wakijinsia n.k.
- Wataweza kuwaongezea wazazi maarifa ya kimalezi.
- Watakuwa na utaratibu wa kuzitembelea na kukagua baadhi ya familia hizi zitakazo kuwa zimeainishwa ili kujua maendeleo yao na kukazia makubaliano waliyoafikiana kupitia mpango kazi kati yao.
- Watatoa huduma za ushauri nasihi, elekezi na saikolojia katika familia husika hali itakayosaidia kupunguza na kuondoa migogoro iliyopo ndani ya familia na inayoweza kusababisha madhara.
- Wataweza kuainisha aina ya huduma inayohitajika katika familia na wapi zielekezwe kulingana na hitaji la kaya (referral).
Ni pamoja na:
- Uwepo wa vifo vinavyoweza kuzuilika miongoni mwa wanafamilia kama mama, baba, watoto, ndugu, walio katika mahusiano n.k.
- Ndoa kuvunjika na kuparaganyika.
- Unyanyasaji.
- Kutelekeza watoto ama familia.
- Ongezeko la Watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani.
- Watoto kusitisha masomo katika shule zote.
- Upotofu wa maadili na utumiaji wa dawa za kulevya.
Ikumbukwe kuwa familia ndiyo msingi mkuu wa awali wakimalezi kwa jamii yoyote na hivyo kukiwa na mkakati wa kitaifa unaolenga kuimarisha maadili, malezi na usalama wa familia niwazi kwamba kutakuwa na mambo chanya:
- Usalama wa familia zetu utaimarika.
- Tutaondoa migogoro iliyopo ngazi ya familia na hivyo kuondoa vihatarishi vya mauaji, ukatili na ukatili wa kijinsia, upotofu wa maadili na changamoto nyinginezo.
- Itaongeza mshikamano ndani ya familia.
- Itasaidia kuhuisha mfumo wa kimaadili yaliyokuwepo kwa jamii nyingi za kitanzania kabla ya mabadiliko ya miaka ya hivi karibuni.
- Uzalishaji wakipato ngazi ya familia utaongezeka na kukuza pato la Taifa kwa ujumla.
- Ushirikishwaji na usawa ngazi ya familia utaongezeka.
- Itaimarisha mfumo wa kimalezi katika familia nyingi zilizo na mapungufu na kusaidia kurejesha maadili ndani ya familia.
- Huduma hii itakuwa niya ngazi ya chini kabisa inayozifikia familia ikiwa ni juhudi za Serikali kuwajibika na kutoa huduma kwa wananchi, hivyo itaongeza furaha, imani na upendo kwa Serikali.
- Mpango huu utaweza kusaidia katika uainishaji wa kaya na familia stahiki katika kupatiwa huduma za kimkakati kama TASAF, n.k.
- Itasaidia wanafamilia kuwa na uwezo wakuzifikia huduma za kiustawi na maendeleo ya kijamii kwa ukaribu zaidi na ni suluhu kwa masuala mengi yakifamilia ambayo yamekuwa yakileta mazingira hatarishi aidha kwa kuvunjika kwa familia, mauaji kutokea, ukatili wakijinsia, kutelekeza familia, upotofu wa maadili n.k.

Upvote
3