Mabraza wa Kariakoo na dili zao

Hatari na nusu.
 
Hapana niko bongo tu hapa hapa,, lakini Mungu kanijaalia kupata michongo na connection nikiwa hapa hapa though nina mabest wengi nje ya nchi na baadhi ulaya.... Ntakufatilia nikishakuelewa na kujua wewe ni nani na sio hatari mbona east yote utatamba .
 
ITAENDELEA......!!!!
Nilikua KAZIMBE napambania kombe......afu huko hakuna network........nitamalizia simulizi yangu......ila nimetoka salama south kivu......nipo njiani narudi Kigoma kwa njia za panya kama nilivyokuja......kama nilivyowaambia nilikuja huku kwa njia za panya.
Braza NDAGARA yupo Burundi anamalizia kibanda chake......japokua dili hazikukamilika kwa kiasi cha 100% lakini Mungu ni mwema hatujatoka haba.
Sikuendelea na simulizi sababu nilikua natafuta mkate wa kila siku na ilibidi nikimbilie KAZIMBE kukwepa vita vya wenyewe kwa wenyewe""I mean vikundi vya waasi""!!!Na vile vile kuke KAZIMBE kulikua na fursa za kucheki kuhusu mawe.
Unajua maisha ya Kivu kusini na Kivu kaskazini ni mpera mpera mda wote.....WATU WAMEVURUGWA.
MUNGU NI MWEMA CHA MUHIMU UHAI.
PAMOJA NA YOOOTE TUNAPUMUA,TUNA AFYA NA HATUNA MADENI.
NARUDIA TENA MUNGU NI MWEMA.
 
😂🤣🤣🤣🤣 umenifurahisha ukishanielewa mimi ni nani 🤣🤣🤣🤣🤣 Watoto wa mjini hatueleweki.....maana hata sisi wenyewe hatujielewi 🤣🤣🤣🤣
Mm raia mwema wa kawaida hapa hapa TANZANIA na ninapambana kujitafutia mkate wa kila siku.
SISI NDIO WALE WATOTO TULIOKULIA MTAANI ILA JAMII HAIKUTUTUPA.....!!!
MUNGU AWABARIKI SANA WATU WOOTE WALIOTUSAIDIA MPAKA HAPA TULIPOFIKA......!!!
 
SIMULIZI ITAENDELEA NIPO NJIANI NARUDI KIGOMA........!!!!!
UNAJUA WADOGO ZANGU NIWAMBIE KITU KIMOJA.
VIJANA WA KITANZANIA TULIOTOKEA MAISHA YA KAWAIDA TUNAPAMBANA SANA NA HAMUWEZI KUELEWA.
TULIFIWA NA WAZAZI TUKIWA WADOGO..... NA BAADHI YA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WALITUTENGA KIMAKUSUDI AU LABDA WALICHOKA KUTUSAIDIA.....HATUWALAUMU SABABU NA WAO WALIKUA NA MAISHA MAGUMU KAMA MNAVYOJUA MAISHA YA KITANZANIA.
MUNGU NI MWEMA MTAANI MABRAZA HAWAKUTUTENGA HIVYO HIVYO WALITUPA SUPPORT HATUWEZI KUWASAHAU JAPO WALITUFUNDISHA MEMA NA MABAYA.
*USHAURI USIO RASMI NO 1
VIJANA WA KISHUA HAMWEZI KUELEWA.
VIJANA MLIOPATA AJIRA ZA SERIKALINI SEHEMU NYETI HAMUWEZI KUELEWA,WENYEWE MNAJIITA WATU WA KWENYE SYSTEM.
VIJANA MLIOPEWA URITHI NA WAZAZI WENU HAMUWEZI ELEWA JINSI MLIVYO NA BAHATI.
PUNGUZENI KUWAHUKUMU SANA VIJANA AMBAO BADO WANAJITAFUTA
*USHAURI USIO RASMI NO 2
VIJANA AMBAO MLIPATA BAHATI YA KUPATA WATU WA KUWASHIKA MKONO HAMUWEZI KUELEWA.
MSIWASEME VIBAYA VIJANA AMBAO BADO HAWAJAFANIKIWA.
WASAIDIENI PALE MNAPOWEZA HAMUWEZI KUJUA KESHO.
**********************************
VIJANA WA KITANZANIA ACHENI KUWAAMINI SANA MOTIVATION SPEAKER KWENYE MITANDAO....97% WANAONGEA VITU VYA KUFIKIRIKA... . TAFUTENI MABRAZA WA KITAANI WAWAPE MIPANGO HALISIA.
VIJANA WA KITANZANIA WANAHITAJI KUPATA WATU WA KUWASHIKA MKONO NA KUWAONYESHA FURSA....ILA KIZAZI CHA SASA NI CHA WATU WABINAFSI...TOFAUTI NA SISI KIZAZI CHA MIAKA YA NYUMA.
ILA MSIFE MOYO WADOGO ZANGU......CHA MSINGI JIFUNZENI KUISHI NA WATU VIZURI SABABU.......WATU NDIO KILA KITU!!!!
ANGALIZO*
KUNA WATU WAKIWAADITHIA WALIPOTOKEA HAMUWEZI KUAMINI.....!!!
KWAHIYO USIWAHUKUMU
UKIONA WAMEKUA MATEJA
UKIONA WAMEFUNGWA JELA
UKIONA WAMEFIA UGHAIBUNI
UKIONA HAWAJAFANIKIWA.
USIPENDE KUWAHUKUMU VIJANA WA KITANZANIA WANAPITIA MENGI.
VILE VILE USISHOBOKEE SANA HELA ZAO....MAANA WANAJUA WALIPOZITOA.
TANZANIA NGUMU KAMA HAUNA CONNECTION.
TANZANIA NGUMU KAMA HAUNA WATU WA KUKUSAIDIA.....NA NI MUNGU PEKEE ANAYELETA BAHATI NA FURSA KWA VIJANA WA MTAANI.
**JAMII HAITUELEWI
JAMII HAITUELEWI SABABU HATUELEWEKI KUTOKANA NA HISTORIA YA NYUMA....!!!
KUSEMA KWELI TUSHAKUAGA VIBAKA.
TUSHAKUAGA WAHUNI WASIO NA AKILI.
TUSHATAPELI.
TUSHADANGANYA SANA.
TUSHADHULUMU SANA.
TUSHAWAINGIZA MJINI SANA WAZEE WA MIGODINI MPAKA TUNAJISIKIA HATIA NA AIBU KWENYE NAFSI ZETU.
JAMII INAYO HAKI YA KUTOTUELEWA VIJANA WA MTAANI NA WALA HATUILAUMU KWA HILO...TUNAOMBA MSAMAHA JAMII ITUSAMEHE
SABABU TULIANZIA NEGATIVE KWENDA POSITIVE.
MIMI NAHADITHIA HARAKATI ZANGU KUWATIA MOYO WADOGO ZANGU KUA MTAFUTAJI HACHOKI NA AKICHOKA BASI HUYO UJUE AMESHAPATA.
HAKUNA KUKATA TAMAA MUNGU YUPO.
KAMA WAO WAMEPATA UKWASI...BASI HATA SISI TUNAWEZA KUUPATA PIA HUO UKWASI.
MUNGU NI MWEMA.
 
NILIPOZUNGUMZIA KUHUSU WAHINDI WALIONIKOPA HELA AKINA PATEL......WATU WALIDHANI NIMETUNGA.....ILA ANDIKO LAKO UMEWADHIBITISHIA KUA HIZI SIO STORY BALI REAL LIFE
Humu wengi hawajakutana na misoto na maisha haina haja ya kufanya wakuamini achana nao ndio maana wengi wao wanapitwa hata na madili ya kawaida tu kwa ubishi wao... Jamaa nimefaidi sana mema yao
 
broh hizo connection msipeane wenyewe 😥😥😥
 
sister usinisahau mdogo wako kwenye ufalme wako...!
 
sister usinisahau mdogo wako kwenye ufalme wako...!
Connection hazianzii kama hizi hazianzii uzeeni, zinaanzia shule!!!!! Kaa ukijua kuna watu wanakusoma na kuelewa uthubutu wako, roho ngumu, kutunza Siri. Sasa hapo ulipo anza kuishi maisha usidharau hata muuza karanga huwezi jua chini ya karanga kuna nn?
 
ACHANA NA USHAURI NASAHA. LETE STORY
 
Mi nina vitabu vyangu kuandika hapa mpk nihakikishiwe ulinzi.. Hongera kwa kujipambania ulipopita hizo ni harakati tu zilizofanya leo uwe hapa!! Maisha ni fumbo kubwa sana shukuru kwa yote.
weka japo code. ila tuandikie tukusome pengine kupitia sauti za muandiko wako wengi akili zetu zitafunguka....!

kuna dada mmoja wa magomeni mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi😭😭😭

yule dada alifanya dili jeusi akapiga pesa dili la mwisho lika ondoka na uhai wake. siku niliyo gundua kuwa mwanamke amethubutu harafu mimi na mikaptura yangu mikubwa mikubwa sina lolote 😭😭😭 haki vile chozi lili nitoka. sister ukipata muda tuhadithie tujifunze...!​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…