Mabraza wa Kariakoo na dili zao

Mabraza wa Kariakoo na dili zao

Miaka hiyo sina hela afu ujana mwingi......kidogo nipagawe.

Nikamcheki braza yangu MUBA MUBANDA....mzee wa kazi zote pale kariakoo.

MIMI: Kaka mdogo wako sina kitu afu unavyojua lazima avensis iingie barabarani siwezi kukaa kinyonge, madogo wa maghorofani wananitambia kinoma.

MUBANDA: Dogo sikia mimi nakupa dili sikupi hela, Kwanza wewe mtoto wa down town...nakuelewa hutoniangusha. Sasa ni hivi nakufundisha kupiga watu ""KIJERUMANI"

MIMI: Kupiga watu MUBA?

MUBANDA: Ndiyo kupiga watu namaanisha kuwaibia dogo. Sio kuiba kwa kutumia nguvu ila kwa kutumia akili, leo jioni twende ukajifunze kwa vitendo ili uive.

Braza Muba mubanda akaninanga sana mda huo"""WEWE MTOTO WA MJINI UNAKOSA HELA UNALIALIAWAKATI WAJINGA KIBAO WA KUWAPIGA KWA KUTUMIA AKILI? ACHA UJINGA TUTAKUFUKUZA DAR SALAAM URUDI NACHINGWEA ......Madai yake ukizaliwa dasilamu jiji la makamba enzi hizo hutakiwi kukosa hela.

JIONI IKAFIKA: Sasa jioni imefika braza MUBA MUBANDA na braza yangu mwingine MUDI MUZUNGU wakanichukua mpaka kkoo kule wanapouza vitu vilivyotumika.....wakaniambia kua kuna pasta ataleta computer zilizotumika ili kuziuza sasa anatakiwa kupigwa...nikae mkao wa kula nijifunze mchezo...wao walishaupanga wiki mbili nyuma leo wanakamilisha tu...mm nitulie nijifunze.

Baada ya saa lizima yule mchungaji kafika na gari aina ya dastun pick up enzi hizo ndio gari za kubebea mzigo ya kishua kafika na mzigo wa computer umejaa nyuma na kawakabidhi mabraza zangu kama madalali wa kumuuzia.

Kumbe ule mzigo mchungaji kaupiga sehemu huko kanisani na inatakiwa wahusika wamdake pale akishauzabna wahusika wenyewe ni wazee wa kanisa wamepewa habari na mabraza zangu ambao wanajifanya madalali kitambo tu..ina maana mabraza wamemzunguka pasta bila yeye kujua wapo sehemu wanasubiria wamkamate ns vidhibiti.

Ila mpango wa mabraza lazima mzigo uuzwe kwanza wachukue hela afu ndio wawastue wazee wa kanisa ili pasta akamatwe.

Na vile vile anayeuziwa tayari alikua ameshatoa cha juu kwa kuwashukuru mabraza kwa kumletea dili tamu...na pia mchungaji alikua ameshatoa cha juu kuwashukuru mabraza kwa kumtafutia mteja wa mali.

Na vilevile wazee wa kanisa walikua wameshatoa cha juu kuwashukuru mabraza kwa kuwaonyesha mwizi wao.
Na mabraza walikua na mpango wa kumzunguka muuzaji na mnunuzi hela ikiwekwa mezani.

Makubaliano yalikua hivi...kwa kua mali ni za wizi...basi hela watachukua mabraza na kumletea mchungaji....yeye hatakiwi kuonekana pale sehemu ya makabidhiano.

Na mnunuzi yeye atatoa hela afu mzigo ataufuata kule ambapo leo ndio ipo stendi ya mwendokasi gerezani.
Mpango wa mabraza ni kumdakisha muuzaji na mnunuzi kwa wakati mmoja wote.

Yaani wakipewa hela wampelekee mchungaji wanamdakisha kabla ya kumpa hela na jamaa anaechukua mzigo wanamdakisha kabla hajaondoka na mzigo...afu hela zote wanakunja wao...na kujifanya dili limeshitukiwa.

Mimi nipo pale kuangalia mchezo na kujifunza ili huko mbele nicheze madili mengine.

Saa mbili ucku mchungaji kaja...kabana sehemu mbali na gari ya mzigo ilipopaki anasubiri hela.

Mnunuzi kakutana na mabraza pale kidongo chekundu kawapa hela nusu nyingine atamalizia mzigo akiuweka katika himaya yake.......afu wao wanampelekea mchungaji hela sababu enzi hizo hakukua na haya mambo ya kutumiana hela kwenye simu...hasa hizi dili chafu.

Wazee wa kanisa nao wamekuja na wamebana sehemu wanamsikilizia mnunuzi wamtie red handed na vifaa.....afu watamalizana na kijana wao mchungaji pale tu atakapokua na hela za mauzo mkononi...hivyo wamejigawa makundi mawili ya vikosi kazi.

Wakati huo mabraza nao wamejipanga wakichukua ile hela nusu toka kwa mnunuzi wataiacha kwangu....pembeni ya barabarani afu mm nitakua kama naokota mfuko...na kutokomea.

NB:Kumbuka hapo wameshakula hela za watu wote watatu ...kwa kujifanya waleta dili kwa mnunuzi na muuzaji na kujifanya watu wema kwa aliyeibiwa.

Mpango ulikua hv...wakimkamatisha pasta wao wanakula kona....tutakutana magomeni mikumi.....Na mm nikichukua lile fuko pale barabarani nipotee tutakutana magomeni.....tujipongeze kwa utapeli wetu uliofanikiwa!

Mda huo kkooo kila mtu yupo bize hata hawajui kama watu tupo kazini.

BAS MUDA UKAFIKA:
Pasta kaja na dastun yake imejaa macomputer used ya kanisa...mzee kasalimiana na mabraza afu kaelekea sehemu kujibanza kusubiri hela.

Dereva wa dastun kaelekea kule relini kupaki gari kusubiri wanunuzi.

Mnunuzi kakutana na mabraza wakampanga mzigo tayari kawapa hela nusu afu kaelekea kule relini lilipopaki dastun kuchukua mzigo.

Wazee wa kanisa wakajigawa makundi mawili na vijana wao, moja kwenda kule relini kuzuia gari.....lisitoke mpaka polisi waje na jingine la kumtaiti pasta mpaka polisi waje.

Mabraza wamechukua hela wakaitia kwenye mfuko wakaja wakaudondosha mbele yangu nilikua nimekaa barabarani nje ya kibaraza cha duka ambalo limeshafungwa tayari na nikaubeba mimi huyo kwenye daladala za kimara zinapopaki naitafuta magomeni mikumi hakuna kugeuka nyuma full uoga 🤣🤣🤣😂😂.

Msala wa nyuma niliadithiwa baadae na mabraza wapigaji watoto wa Kariakoo na Ilala.

ITAENDELEA.........!!!!!

Muendelezo Soma Mabraza wa Kariakoo na dili zao
Hatari na nusu.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] bas sista....nilidhani ww ndio yule dada wa kitanzania 2006 niliekutana nae Beirut.....nimevurugwa afu nina pasi ya kusafiria ya Burundi......wajanja wamenitapeli......Alinisaidia sana yule sista.....mpaka nafika nililotakiwa kufika.
[emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23]Mm nishawahi kukaa na madini ya tanzanite ya thamani ya 460 Tz shilling ila sikua najua miaka mitatu na nusu wakati mwenye nayo yupo kifungoni.....baada ya yeye kupata msala huko singida.
Mpaka leo wale mabroo,,,,,huwambiii kitu kuhusu mm.
Hapana niko bongo tu hapa hapa,, lakini Mungu kanijaalia kupata michongo na connection nikiwa hapa hapa though nina mabest wengi nje ya nchi na baadhi ulaya.... Ntakufatilia nikishakuelewa na kujua wewe ni nani na sio hatari mbona east yote utatamba .
 
ITAENDELEA......!!!!
Nilikua KAZIMBE napambania kombe......afu huko hakuna network........nitamalizia simulizi yangu......ila nimetoka salama south kivu......nipo njiani narudi Kigoma kwa njia za panya kama nilivyokuja......kama nilivyowaambia nilikuja huku kwa njia za panya.
Braza NDAGARA yupo Burundi anamalizia kibanda chake......japokua dili hazikukamilika kwa kiasi cha 100% lakini Mungu ni mwema hatujatoka haba.
Sikuendelea na simulizi sababu nilikua natafuta mkate wa kila siku na ilibidi nikimbilie KAZIMBE kukwepa vita vya wenyewe kwa wenyewe""I mean vikundi vya waasi""!!!Na vile vile kuke KAZIMBE kulikua na fursa za kucheki kuhusu mawe.
Unajua maisha ya Kivu kusini na Kivu kaskazini ni mpera mpera mda wote.....WATU WAMEVURUGWA.
MUNGU NI MWEMA CHA MUHIMU UHAI.
PAMOJA NA YOOOTE TUNAPUMUA,TUNA AFYA NA HATUNA MADENI.
NARUDIA TENA MUNGU NI MWEMA.
 
Hapana niko bongo tu hapa hapa,, lakini Mungu kanijaalia kupata michongo na connection nikiwa hapa hapa though nina mabest wengi nje ya nchi na baadhi ulaya.... Ntakufatilia nikishakuelewa na kujua wewe ni nani na sio hatari mbona east yote utatamba .
😂🤣🤣🤣🤣 umenifurahisha ukishanielewa mimi ni nani 🤣🤣🤣🤣🤣 Watoto wa mjini hatueleweki.....maana hata sisi wenyewe hatujielewi 🤣🤣🤣🤣
Mm raia mwema wa kawaida hapa hapa TANZANIA na ninapambana kujitafutia mkate wa kila siku.
SISI NDIO WALE WATOTO TULIOKULIA MTAANI ILA JAMII HAIKUTUTUPA.....!!!
MUNGU AWABARIKI SANA WATU WOOTE WALIOTUSAIDIA MPAKA HAPA TULIPOFIKA......!!!
 
SIMULIZI ITAENDELEA NIPO NJIANI NARUDI KIGOMA........!!!!!
UNAJUA WADOGO ZANGU NIWAMBIE KITU KIMOJA.
VIJANA WA KITANZANIA TULIOTOKEA MAISHA YA KAWAIDA TUNAPAMBANA SANA NA HAMUWEZI KUELEWA.
TULIFIWA NA WAZAZI TUKIWA WADOGO..... NA BAADHI YA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WALITUTENGA KIMAKUSUDI AU LABDA WALICHOKA KUTUSAIDIA.....HATUWALAUMU SABABU NA WAO WALIKUA NA MAISHA MAGUMU KAMA MNAVYOJUA MAISHA YA KITANZANIA.
MUNGU NI MWEMA MTAANI MABRAZA HAWAKUTUTENGA HIVYO HIVYO WALITUPA SUPPORT HATUWEZI KUWASAHAU JAPO WALITUFUNDISHA MEMA NA MABAYA.
*USHAURI USIO RASMI NO 1
VIJANA WA KISHUA HAMWEZI KUELEWA.
VIJANA MLIOPATA AJIRA ZA SERIKALINI SEHEMU NYETI HAMUWEZI KUELEWA,WENYEWE MNAJIITA WATU WA KWENYE SYSTEM.
VIJANA MLIOPEWA URITHI NA WAZAZI WENU HAMUWEZI ELEWA JINSI MLIVYO NA BAHATI.
PUNGUZENI KUWAHUKUMU SANA VIJANA AMBAO BADO WANAJITAFUTA
*USHAURI USIO RASMI NO 2
VIJANA AMBAO MLIPATA BAHATI YA KUPATA WATU WA KUWASHIKA MKONO HAMUWEZI KUELEWA.
MSIWASEME VIBAYA VIJANA AMBAO BADO HAWAJAFANIKIWA.
WASAIDIENI PALE MNAPOWEZA HAMUWEZI KUJUA KESHO.
**********************************
VIJANA WA KITANZANIA ACHENI KUWAAMINI SANA MOTIVATION SPEAKER KWENYE MITANDAO....97% WANAONGEA VITU VYA KUFIKIRIKA... . TAFUTENI MABRAZA WA KITAANI WAWAPE MIPANGO HALISIA.
VIJANA WA KITANZANIA WANAHITAJI KUPATA WATU WA KUWASHIKA MKONO NA KUWAONYESHA FURSA....ILA KIZAZI CHA SASA NI CHA WATU WABINAFSI...TOFAUTI NA SISI KIZAZI CHA MIAKA YA NYUMA.
ILA MSIFE MOYO WADOGO ZANGU......CHA MSINGI JIFUNZENI KUISHI NA WATU VIZURI SABABU.......WATU NDIO KILA KITU!!!!
ANGALIZO*
KUNA WATU WAKIWAADITHIA WALIPOTOKEA HAMUWEZI KUAMINI.....!!!
KWAHIYO USIWAHUKUMU
UKIONA WAMEKUA MATEJA
UKIONA WAMEFUNGWA JELA
UKIONA WAMEFIA UGHAIBUNI
UKIONA HAWAJAFANIKIWA.
USIPENDE KUWAHUKUMU VIJANA WA KITANZANIA WANAPITIA MENGI.
VILE VILE USISHOBOKEE SANA HELA ZAO....MAANA WANAJUA WALIPOZITOA.
TANZANIA NGUMU KAMA HAUNA CONNECTION.
TANZANIA NGUMU KAMA HAUNA WATU WA KUKUSAIDIA.....NA NI MUNGU PEKEE ANAYELETA BAHATI NA FURSA KWA VIJANA WA MTAANI.
**JAMII HAITUELEWI
JAMII HAITUELEWI SABABU HATUELEWEKI KUTOKANA NA HISTORIA YA NYUMA....!!!
KUSEMA KWELI TUSHAKUAGA VIBAKA.
TUSHAKUAGA WAHUNI WASIO NA AKILI.
TUSHATAPELI.
TUSHADANGANYA SANA.
TUSHADHULUMU SANA.
TUSHAWAINGIZA MJINI SANA WAZEE WA MIGODINI MPAKA TUNAJISIKIA HATIA NA AIBU KWENYE NAFSI ZETU.
JAMII INAYO HAKI YA KUTOTUELEWA VIJANA WA MTAANI NA WALA HATUILAUMU KWA HILO...TUNAOMBA MSAMAHA JAMII ITUSAMEHE
SABABU TULIANZIA NEGATIVE KWENDA POSITIVE.
MIMI NAHADITHIA HARAKATI ZANGU KUWATIA MOYO WADOGO ZANGU KUA MTAFUTAJI HACHOKI NA AKICHOKA BASI HUYO UJUE AMESHAPATA.
HAKUNA KUKATA TAMAA MUNGU YUPO.
KAMA WAO WAMEPATA UKWASI...BASI HATA SISI TUNAWEZA KUUPATA PIA HUO UKWASI.
MUNGU NI MWEMA.
 
NILIPOZUNGUMZIA KUHUSU WAHINDI WALIONIKOPA HELA AKINA PATEL......WATU WALIDHANI NIMETUNGA.....ILA ANDIKO LAKO UMEWADHIBITISHIA KUA HIZI SIO STORY BALI REAL LIFE
Humu wengi hawajakutana na misoto na maisha haina haja ya kufanya wakuamini achana nao ndio maana wengi wao wanapitwa hata na madili ya kawaida tu kwa ubishi wao... Jamaa nimefaidi sana mema yao
 
NILICHUKUA HELA NDOGO KWA SABABU SIPENDI.....KUKAAA NA HELA NYINGI ZA WATU NI HATARI.....
MATAJIRI WATU WAZURI ILA SIO KWENYE HELA ZAO ZA BIASHARA......MNAWEZA KUUANA KISA HELA.
Nitakuchek DM sista usijali nikupe michongo.......
Bro wako nilikua chimbomoja linaitwa KAZIMBE......🤣🤣🤣🤣nimefirisika now.....dili zimekataa
broh hizo connection msipeane wenyewe 😥😥😥
 
Hapana niko bongo tu hapa hapa,, lakini Mungu kanijaalia kupata michongo na connection nikiwa hapa hapa though nina mabest wengi nje ya nchi na baadhi ulaya.... Ntakufatilia nikishakuelewa na kujua wewe ni nani na sio hatari mbona east yote utatamba .
sister usinisahau mdogo wako kwenye ufalme wako...!
 
sister usinisahau mdogo wako kwenye ufalme wako...!
Connection hazianzii kama hizi hazianzii uzeeni, zinaanzia shule!!!!! Kaa ukijua kuna watu wanakusoma na kuelewa uthubutu wako, roho ngumu, kutunza Siri. Sasa hapo ulipo anza kuishi maisha usidharau hata muuza karanga huwezi jua chini ya karanga kuna nn?
 
SIMULIZI ITAENDELEA NIPO NJIANI NARUDI KIGOMA........!!!!!
UNAJUA WADOGO ZANGU NIWAMBIE KITU KIMOJA.
VIJANA WA KITANZANIA TULIOTOKEA MAISHA YA KAWAIDA TUNAPAMBANA SANA NA HAMUWEZI KUELEWA.
TULIFIWA NA WAZAZI TUKIWA WADOGO..... NA BAADHI YA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WALITUTENGA KIMAKUSUDI AU LABDA WALICHOKA KUTUSAIDIA.....HATUWALAUMU SABABU NA WAO WALIKUA NA MAISHA MAGUMU KAMA MNAVYOJUA MAISHA YA KITANZANIA.
MUNGU NI MWEMA MTAANI MABRAZA HAWAKUTUTENGA HIVYO HIVYO WALITUPA SUPPORT HATUWEZI KUWASAHAU JAPO WALITUFUNDISHA MEMA NA MABAYA.
*USHAURI USIO RASMI NO 1
VIJANA WA KISHUA HAMWEZI KUELEWA.
VIJANA MLIOPATA AJIRA ZA SERIKALINI SEHEMU NYETI HAMUWEZI KUELEWA,WENYEWE MNAJIITA WATU WA KWENYE SYSTEM.
VIJANA MLIOPEWA URITHI NA WAZAZI WENU HAMUWEZI ELEWA JINSI MLIVYO NA BAHATI.
PUNGUZENI KUWAHUKUMU SANA VIJANA AMBAO BADO WANAJITAFUTA
*USHAURI USIO RASMI NO 2
VIJANA AMBAO MLIPATA BAHATI YA KUPATA WATU WA KUWASHIKA MKONO HAMUWEZI KUELEWA.
MSIWASEME VIBAYA VIJANA AMBAO BADO HAWAJAFANIKIWA.
WASAIDIENI PALE MNAPOWEZA HAMUWEZI KUJUA KESHO.
**********************************
VIJANA WA KITANZANIA ACHENI KUWAAMINI SANA MOTIVATION SPEAKER KWENYE MITANDAO....97% WANAONGEA VITU VYA KUFIKIRIKA... . TAFUTENI MABRAZA WA KITAANI WAWAPE MIPANGO HALISIA.
VIJANA WA KITANZANIA WANAHITAJI KUPATA WATU WA KUWASHIKA MKONO NA KUWAONYESHA FURSA....ILA KIZAZI CHA SASA NI CHA WATU WABINAFSI...TOFAUTI NA SISI KIZAZI CHA MIAKA YA NYUMA.
ILA MSIFE MOYO WADOGO ZANGU......CHA MSINGI JIFUNZENI KUISHI NA WATU VIZURI SABABU.......WATU NDIO KILA KITU!!!!
ANGALIZO*
KUNA WATU WAKIWAADITHIA WALIPOTOKEA HAMUWEZI KUAMINI.....!!!
KWAHIYO USIWAHUKUMU
UKIONA WAMEKUA MATEJA
UKIONA WAMEFUNGWA JELA
UKIONA WAMEFIA UGHAIBUNI
UKIONA HAWAJAFANIKIWA.
USIPENDE KUWAHUKUMU VIJANA WA KITANZANIA WANAPITIA MENGI.
VILE VILE USISHOBOKEE SANA HELA ZAO....MAANA WANAJUA WALIPOZITOA.
TANZANIA NGUMU KAMA HAUNA CONNECTION.
TANZANIA NGUMU KAMA HAUNA WATU WA KUKUSAIDIA.....NA NI MUNGU PEKEE ANAYELETA BAHATI NA FURSA KWA VIJANA WA MTAANI.
**JAMII HAITUELEWI
JAMII HAITUELEWI SABABU HATUELEWEKI KUTOKANA NA HISTORIA YA NYUMA....!!!
KUSEMA KWELI TUSHAKUAGA VIBAKA.
TUSHAKUAGA WAHUNI WASIO NA AKILI.
TUSHATAPELI.
TUSHADANGANYA SANA.
TUSHADHULUMU SANA.
TUSHAWAINGIZA MJINI SANA WAZEE WA MIGODINI MPAKA TUNAJISIKIA HATIA NA AIBU KWENYE NAFSI ZETU.
JAMII INAYO HAKI YA KUTOTUELEWA VIJANA WA MTAANI NA WALA HATUILAUMU KWA HILO...TUNAOMBA MSAMAHA JAMII ITUSAMEHE
SABABU TULIANZIA NEGATIVE KWENDA POSITIVE.
MIMI NAHADITHIA HARAKATI ZANGU KUWATIA MOYO WADOGO ZANGU KUA MTAFUTAJI HACHOKI NA AKICHOKA BASI HUYO UJUE AMESHAPATA.
HAKUNA KUKATA TAMAA MUNGU YUPO.
KAMA WAO WAMEPATA UKWASI...BASI HATA SISI TUNAWEZA KUUPATA PIA HUO UKWASI.
MUNGU NI MWEMA.
ACHANA NA USHAURI NASAHA. LETE STORY
 
Mi nina vitabu vyangu kuandika hapa mpk nihakikishiwe ulinzi.. Hongera kwa kujipambania ulipopita hizo ni harakati tu zilizofanya leo uwe hapa!! Maisha ni fumbo kubwa sana shukuru kwa yote.
weka japo code. ila tuandikie tukusome pengine kupitia sauti za muandiko wako wengi akili zetu zitafunguka....!

kuna dada mmoja wa magomeni mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi😭😭😭

yule dada alifanya dili jeusi akapiga pesa dili la mwisho lika ondoka na uhai wake. siku niliyo gundua kuwa mwanamke amethubutu harafu mimi na mikaptura yangu mikubwa mikubwa sina lolote 😭😭😭 haki vile chozi lili nitoka. sister ukipata muda tuhadithie tujifunze...!​
 
Back
Top Bottom