JPM alifanya trip kadhaa pale bandarini mara baada tu ya kuingia madarakani. Haikuwa kazi rahisi kuikata ile mirija pale.
Huyu mama ameingia madarakani akaanza kuwachekea hao wezi akidhani JPM alikuwa kichaa kuwanyoosha.
Sasa anadhani DPW watafanya nini?? Shida ni yeye, amekuta mifumo imara kaamua kuibomoa kwa ushauri mbovu aliopewa na hao wezi waliotega mirija yao hapo.
As long as anaongoza nchi kwa kulipa fadhila kwa maswahiba asahau kuhusu ufanisi. Kwanini alimwondoa Kakoko pale? Nani alimshauri? Arejee hatua zake nyuma atawajua wabaya wake.
Tatizo ni mama Mwenyewe Wala SIO watanzania.
Hii nchi kamwe haiataacha kutafunwa kama tutakua na watu wabinafsi na wanaosimamia Mila na itikadi zao Badala za Katiba.
Yani akiingia mmanyema anaangalia Mila za kimanyema, akiingia Mzaramo anaangalia Mila za kizaramo Badala ya Katiba. Akiingia Mzanzibari au mtanganyika akataka ajikite kwenye ukanda wake Badala ya Katiba ya nchi. Mbaya zaidí CCM Imekua ikicheza mchezo mbaya zaudi Wa Udini Kila Wanapoona Wizi wao unaanza kuwachosha Wananchi.
Mfano karata anayetaka kuitumia Kikwete ni kuwachanginisha Wakristo kupitia madhahebu anayojua miaka yote hawalipendi kanisa la Roma ,Mfano Wasabato,na makanisa ya Mabepari na wakaloni Mambo Leo ya kimarekani yanayoendeshwa kifamilia na kukusanya Sadaka Kwa ajili ya kujilimbikizia Mali bila kutoa Mchango Wowote au huduma yoyote kwenye jamii.
Magufuli alikua na akili kubwa na Maono.
Chuki kubwa ya watu wachache sana ndiyo inayoliumiza taifa hili.
Kuelekea 2025 wapinzani walikua na nafasi kubwa sana ya kuchukua nchi Kwa asilimia kubwa sana.
Tatizo litakalowasumbua ni Kuwa na Vyama visivyo na Mrengo Wa kisiasa.
CCM ni Chama Cha kijamaa na katiba Yetu na Mila zetu na utamaduni WETU ni utamadunia unayoendana sana na ujamaa na kujitegemea .
Mwalimu alitumia nguvu kubwa sana kulinda Mila zetu ,umoja WETU na utamaduni WETU na hulka Yetu ya Ujamaa.
Tatizo wamejitokeza watawala wanaoendekeza ama Udini au biashara Zao na uroho Wa Mali . Yani kuanzia kipindi Fulani walijitokeza watawala wakaanza kuwagawa wanafunzi mashuleni kulingana na Dini zao Kwa kuvaa mavazi Tofauti. Mara zikaanza Taasisi za kudhaminiwa na Matajiri Wenye Dini Fulani kuanzisha benki zisizo na Riba Kwa watu Wa Dini Fulani,mara wakaanza kufadhili Taasisi za kuficha watoto misituni na kuwafundisha mambo ya kupigana na kupigania Dini. Mabiloni ya pesa yakaelekezwa mifukoni mwa watu. Baadae wakajitokeza watu wakapiga Kelele Kuwa hatuelekei kuzuri. Watawala wakakaa kimya na chama tawala. Watu wakaanza kumwagiwa Tindikali kule Zanzibar watawala wakakaa kimya . Zanzibar ni kaeneo kadogo watu wanajuana lakini hakuna aliyekamatwa. Kwa kuchoma makanisa moto Wala kumwagia mapadri Tindikali.
Kikwete akemee Dini zinazokaa kimya wakati watawala wanapokiuka Sheria na kuwaonea wanyonge kwenye utajiri aliouumba Mwenyezi MUNGU.
Nchi ni ya MUNGU,rasilimali ameziumba Mungu sio chama Cha Mapinduzi Wala Watawala na tamaa Zao. MUNGU ananungunikiwa na wanyonge kwenye nchi aliyoiumba na kuiwekea rasilimali nyingi Kwa sababu ya Wanasiasa waovu halafu eti viongozi Wa Dini wakae kimya.!!
Lakini walipoanza kusema CCM isichaguliwe kule Zanzibar ndipo walipokamatwa mashekhe na kupewa kesi ya ugaidi. Waliona CCM ikiondoka madarakani maslahi ya wale wanaotumika kupokea Mapesa machafu kupitia mipango Yao ya hovyo yatapotea.
Hii nchi Kuna watu wachache wanajilimbikizia Mali kutokana na harakati chafu sana na Kwa sababu wamejificha ndani ya Chama Cha Mapinduzi hawaguswi.
Haiwezekani bandari kubwa kama ya Dar es Salaam wapewe Waarabu kuja kuiendesha Chini ya Serikali ya wezi waliojawa na Udini ,uchama na ubinafsi mkubwa halafu ifanye Vizuri . Ni ndoto ya alinacha . Kinachofanyika ni Wezi waliochota pesa za umma kuungana na DPW kujiuzia bandari Kwa mgongo Wa Nyuma.
Hivi kama Mwarabu Chini ya mkataba huo mbovu na utawala mbovu Chini ya Chama kibovu na TRA yenye utendaji mbovu na TPA mbovu akishindwa kuleta tija atafanywaje.?
Yaani Waarabu wanaotuibia wanyama na kufanya njama kumiliki nchi ya Loliondo ndani ya Tanganyika Leo wamegeuka na Kuwa na Huruma ya kutukuaanyia pesa za bandari yetu Kisha watupe tupate maendeleo tusomeshe watoto WETU wapate utaalamu mkubwa na tuwe na jeshi kubwa na imara ,na teknolojia kubwa na maendeleo makubwa ,tuchimbe mafuta Yetu na gesi yetu na urenium Yetu Kisha tuchukue bandari Yetu tuimiliki na wao warudi Dubai Jangwani . Ni kichaa pekee aliyechanganyikiwa na kubaki kama Nabii Tito anaxeweza kuamini Kuwa DPW watatuletea maendeleo.
Kwanza hawatamuogopa MTU yeyote Kwa sababu Hana Cha kuwafanya na Hana mamlaka ya kuwafanya Chochote.
Magufuli aliogopwa mana alikua anaweza kumfanya MTU Chochote.
Hawa Hata Wakiiba hakuna MTU atawakamata Wala Kufunga Akaunti zao Wala kuwafungulia kesi za uhujumu uchumi Wala kuwanyanganya Mali zao Wala kutengua uteuzi wao.
Kifupi Kwa Serikali ya chama Cha Mapinduzi ni Bora tuendelee kuendesha bandari Yetu mana angalau akijakutokea Magufuli Mwingine basi atawatumbua Wezi na kuwaweka gerezani au Hata kutaigisha Mali za wale wasiotaka kubadilika . Angalau watu watakua waoga pale bandarini. Watanzania ni waoga lakini wakiona wenzao wanaiba na hawasemeshi Wala kutumbuliwa basi na wao Wanaiba. Na wakiona Kuwa kibali Cha kuiba ni shati la kijani basi wanavaa.
Bandari zetu wapewe watanzania Wenzetu . Wapewe Kwa mikataba inayobana wizi kuliko kupewa waarabu ambao hatutaweza kuwabana Kwa sababu mkataba umewapa heshima kubwa Kama miungu. Mbaya zaidí kuna watu wanawaona kama vile ni wakombozi Wa kidini na kiroho.
Bodi ya bandari iundwe na Majenerali Wa Jeshi la Wananchi Badala ya makada Wa CCM waliotumikia wizi Kwa miaka mingi na wanaendelea kuwaza pesa za Rushwa zipatikane wapate Mgao .
Ukimsikiliza Zito kabwa huwezi kuamini Kuwa Ana Miliki chama Cha kijamaa kifalisafa na kiimani Bali ni Muungano Wa fursa ya kuiba pamoja na CCM.