Imeshawatokea wengi. Unaitikia hodi kisha kimya ukitoka nje huoni mtuπHii ya kutoitikia hodi Kwa mara ya Kwanza hata wazazi walikuwa wakitukumbusha sana.
Kuna kipindi nilikuwa nadaiwa ,siwezi kufungua geti kama sikujui wewe ni naniπ
Mkuu Mshana Jr hiyo namba 1 naomba maelezo kidogo1.Usiende moja kwa moja nyumbani unapotoka makaburini.. Simama kidogo mahali zuga kwa muda kidogo then nenda kwako
2. Usiweke alama ya KARIBU nyumbani kwako si kila mtu ni wa kukaribisha na hapo sio eneo la biashara
3. Usilale na kioo kinakutazama.. Ukiwa usingizini utaonwa na wengi
4. Usipige mluzi baada ya saa 12 jioni..kuna mtu atakujibu
5. Usiitikie hodi ya kwanza si kila apigaye hodi ni binadamu.. !
Niwatakie Ijumaa kuu yenye baraka na fanaka tele.
Ijumaa khareem kwa wengine pia!
Kupoteza "Mizimu" au Gundu: Inaaminika kuwa ukitoka makaburini, kunaweza kuwa na "vitu" au nishati hasi (vifungo/mizimu) inayoweza kukufuata nyuma. Kwa kusimama sehemu nyingine (kama gengeni au kwa rafiki), unakata hiyo njia ili usiipeleke nyumbani kwako .Mkuu Mshana Jr hiyo namba 1 naomba maelezo kidogo
Ilikuwaje?3 Hiyo lilishawahi nikuta jambo ambalo mpaka leo hii sijawahi kulielewa
Picha likaanza nimelala usiku na siku hiyo sikuzima taa, nikaota ndoto Kuna mtu ananiangalia pasipo kupepesa macho .. Sasa ile kushtuka usingizini Kuna kioo nilikuwa nimekiweka dirishani.... Ghafla naona taswira yangu ikiniangalia kwa kunikazia macho pasipo kujitingisha huku nakisogelea kioo... Baada ya hapo ikapotea ikabaki taswira yangu ya kawaida halisi... Hili tukio naliwazaga sana sijawahi kupata majibuIlikuwaje?
Hii ni imani nyingine nzito ya kishirikina au kishirikina-jamii ambayo imekuwepo kwa muda mrefu. Inahusisha kioo na ulimwengu wa roho au "vitu visivyoonekana."
Sababu zinazotolewa kwa imani hii ni pamoja na:
Lango la Kiroho: unajua kioo ni kama "dirisha" au lango. Ukilala kinakutazama, roho yako (ambayo huaminika kuwa safarini unapolala) inaweza "kunaswa" au kuonekana na viumbe wa ulimwengu mwingine.
Wizi wa Nishati: Wengine huamini kioo kinaweza kunyonya nishati yako ukiwa umelala, jambo linaloweza kukufanya uamke ukiwa umechoka sana au mwenye maumivu ya mwili.
Ndoto za Kutisha: Kisaikolojia, ukishtuka usiku na kuona kivuli chako mwenyewe kwenye kioo, unaweza kupata hofu kubwa inayopelekea ndoto mbaya au kiharusi cha usingizi (sleep paralysis).
Hata kwenye misingi ya Feng Shui (sanaa ya mpangilio ya Kichina), kioo kinachotazama kitanda kinahesabiwa kama nishati mbaya inayoweza kuleta vurugu kwenye mahusiano au usingizi.
Bahati Mbaya na Imani Potofungoja nisubiri visa na ushuhuda ππ
hiyo no 2 sasa wale watu wa naksh nakshi mbona inatukata
hiyo no 3 kuna mahali niliona wanasema kioo kilicho pasuka ndo kibaya zaidi