Machache ya kuzingatia - Maalumu kwa tamaduni za kitanzania

Ghafla naona taswira yangu ikiniangalia kwa kunikazia macho pasipo kujitingisha huku nakisogelea kioo... Baada ya hapo ikapotea ikabaki taswira yangu ya kawaida halisi..🥺🥺🥺
 
nimekupata mkuu🙏
 
Mkuu Mshana Jr naomba kujua kuhusu mambo ya kiroho yanayotokana na nishati ya asili, Nilikua na Biashara mbili zilikjya zinaniingizia pesa lakini hakuna kitu cha Maana unafanya kazi nikufanya biashara ila nilishindwa kununua ata kiwanja japo biashara inanipa faida,Mimi nilikua nafanya biashara X nikapata ushindani na mtu ambaye alizungumza maneno ya kuroga biashara alafu baada ya miezi kadhaa vitu vinaanza kuharibika n.k, hadi biashara ilikufa. Pia kuwa nilikuwa na mali kama kiwanja, biashara alafu zikatokea changamoto zikasababisha kila kitu kufa, hiyo hali imenikuta miaka miwili iliyopita kwasasa sina kitu yani nimeanza moja..
Napambana kurud kwenye mstari hii kiroho nawezaje kuvuka? Kwa namna ivi narudi kwenye mstari?
 
Mkuu soma hii kisha nitakurudia

 
Sawa ngoja nisome
 
Mateka na watumwa kwenye ulimwengu wa roho | JamiiForums Mateka na watumwa kwenye ulimwengu wa roho
 
Yeah you are right, Shangazi yangu alinifundisha kwamba nguo ulizotoka nazo kuzika hutakiwi kuingia nazo ndani. Zivulie nje zifuliwe zikikauka ndio ziingie ndani. Sasa hizi nyumba za ku share compound ndio kimbembe kuvulia nguo nje🤣🤣🤣
 
Mshana Jr unaweza kutoa ufafanuzi kidogo kuhusu mlango mtu anapokufungulia au kufunga hasa unapoingia katika nyumba ya mtu.

Nimewahi kuambiwa kuna manuizi hatari mtu anaweza kukufanyia kwa namna hii.
 
Asante mkuu, nipo kusoma kwenye Tiba ya chumvi, nikipata jambo sijaelewa nitakuuliza mkuu 🙏
 
Huu sasa ni ushirikina.
 
Sjaelewa mzee mshana hii ya kutoka makaburini, una maanisha mfano msiba umetokea kwa jirani huyo jirani sehemu ya makaburi yao ni 3km kutoka nyumbani kwake,ina maana tukitoka kuzika, narudi sasa nyumbani kwa jirani ina maana NIZUGE njiani ama mpaka natoka makaburini naenda nyumbani kwangu ndo nizuge njiani?
 
Msiba wowote ule ukitoka makaburini usinyooshe nyumbani weka kituo mahali kwa dakika chache kuvunja mnyororo wa nishati ya makaburini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…