Machache ya kuzingatia - Maalumu kwa tamaduni za kitanzania

Tawire tawire mkuu
 
Hahaha huwa mambo mengi sana nataka nione , kuna nyumba niliambiwa kuna majini yanapiga watu niliishi sikuoana nikipigwa😃
Ulikaa siku ngapi? Mimi Tanga kuna nyumba niliwahi kusimuliwa vituko vyake SIKUAMINI KABISA
Shida yake kubwa usilale pekeyako
Likizo moja nikaenda kukaa na wenyeji ambao baada ya Kama siku 4 hivi wakasafiri nikabaki peke yangu
Nilikaa bila shida kwa siku kumi mwisho nikaamini ni story tuu
Bado siku moja warudi wale wenyeji nikakipata usiku mzima ulikuwa mauzauza tupu😂
Kokoto zinamwagwa kwenye paa la nyumba
Mara mwanga unamulika chumba chote
Mara unahisi kabida chumbani huko pekeyako nknk😂
 
Kuna kiwango cha uoga kikifika akili inakuletea mauza uza😀
 
Kuna kiwango cha uoga kikifika akili unakuletea mauza uza😀
Hapana mimi sio muoga na ile show ilidumu almost saa nzima.. Nina shuhuda nyingi sana za Tanga nilizoshuhudia live mwenyewe😀
 
Bora lawama, kuanzia leo hii dressing table ya ma mtu, kabla ya kulala nitakuwa naifunika na gunia aisee maana ina face kitanda directly.
 
Mkuu Mshana Jr ,nakuomba nielezee hii namba 3 vizuri kwa mapana yake.
 
Mkuu Mshana Jr ,nakuomba nielezee hii namba 3 vizuri kwa mapana yake.
Usilale na kioo kinakutazama.. Ukiwa usingizini utaonwa na wengi

Hii ni imani nyingine nzito ya kishirikina au kishirikina-jamii ambayo imekuwepo kwa muda mrefu. Inahusisha kioo na ulimwengu wa roho au "vitu visivyoonekana."

Sababu zinazotolewa kwa imani hii ni pamoja na:
Lango la Kiroho: unajua kioo ni kama "dirisha" au lango. Ukilala kinakutazama, roho yako (ambayo huaminika kuwa safarini unapolala) inaweza "kunaswa" au kuonekana na viumbe wa ulimwengu mwingine.
Wizi wa Nishati: Wengine huamini kioo kinaweza kunyonya nishati yako ukiwa umelala, jambo linaloweza kukufanya uamke ukiwa umechoka sana au mwenye maumivu ya mwili.

Ndoto za Kutisha: Kisaikolojia, ukishtuka usiku na kuona kivuli chako mwenyewe kwenye kioo, unaweza kupata hofu kubwa inayopelekea ndoto mbaya au kiharusi cha usingizi (sleep paralysis).
 
aisee
 
Nyumba ikifagiliwa usiku, usitupe taka nje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…