Machache yaliyoonekana Yanga ikiibuka na ushindi mnono dhidi ya Dodoma jiji

kalisheshe

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2020
Posts
2,064
Reaction score
4,056
1. Inawezekana kabisa Yanga imejipata, wachezaji wanacheza kwa nguvu na kujituma kama ilivyokua mwanzo, gari limewaka.

2. Kibwana Shomari ameendelea kuproove kwanini mashabiki walipiga kelele apewe nafasi ya kucheza. Aziz k amerudi.

3. Clement mzize ni winga hatari sana kwa sasa, ana kasi, nguvu na uwezo wa kufunga ni kipaji tu ndio amekosa ila vingine vyote anavyo.

4. Dodoma jiji wameiga kila kitu kutoka kwa Kagera walipocheza na Simba, huwezi kupishana na wachezaji wenye quality halafu wasikuadhibu.

5. Naiona Yanga ikitinga robo fainali club bingwa kama itapata ushindi dhidi ya Tp mazembe tar 4.

6. Makosa madogo ya refarii kuhusu penati hayaondoi ukweli kwamba Yanga wamecheza vizuri.

Hongereni watani

Karibuni kwenye ubaya ubwela
 
Hapo umenena kiufundi na kikubwaπŸ‘πŸ‘
 
Nimebidi nipekue mafaili kwanza ili nijue kama kweli ni mwana Simba ama lah. Aisee hongera huwezi kuona Scars akaandika vitu vyenye uhalisia kama wewe. Wewe ni shabiki haswa wa mpira
 
Nimevumilia nimeshindwa, uchambuzi murua kabisa.
Tukutane Robo fainali.
 
Umenena vyema,
 
🀣🀣🀣usiwape moyo mkuu hapo hyo nafasi ya robo fainali haipo yanga walijiharibia wenyewe walipotoa suluhu na tp mazembe km wangeshinda mechi hizo 2 wangekuwa na nafasi ya kutinga hatua nyingine
 
Wewe ni kolo usie na umbumbumbu.
 
Kuna kitu Dube inabidii aboleshe zaidi anakua na pressure sana akiwa kwenye 18, imagine alipo anguka bilaa kuguswa Leo refa makosa kibinadam akatenga penalty. Kii piaa amepotezaa pasiii sana! Wakikutana na Timu Boraa kama Mazembee hawafurukutiiiiiii.
 
Haya ni maigizo tu mkuu sema soka la bongo usichulkulie serious sana hawa Dodoma juzi wamecheza na simba wakapewa ahadi nzito ili waifunge simba bahati mbaya wakafungwa wakalia hadi wakatoa makamasi ila leo unaona kabsa ni maigizo mwanzo mwisho
Nimeona wakipongezana mwishoni

Ila tusiache kuwapa credit Yanga, wamelitumia vyema kila nafasi waliyoipata
 
Point no.4 ni ukweli mtupu (naked truth)

Point no.5 ni sawa sawa na MENDE KUANGUSHA KABATI..NI SAWA NA MAJI KUUPANDA MLIMA AU TUSEME NI NDOTO YA ALINACHA.
 
Point no.4 ni ukweli mtupu (naked truth)

Point no.5 ni sawa sawa na MENDE KUANGUSHA KABATI..NI SAWA NA MAJI KUUPANDA MLIMA AU TUSEME NI NDOTO YA ALINACHA.
Kama yanga wataibuka na ushindi dhidi ya Tp mazembe watarudisha ali na morali iliyokua imepotea kwahiyo itakua rahisi kwa wao kuforce matokeo watakapokutana na MC Algers, hapo watafikisha point 7 kumbuka mechi zote zitachezwa Tanzania baada ya hapo watawafata Al Hilal ambao sina shaka watakua wamefuzu tayali kwa hiyo hakutakua na ugumu wa yanga kuforce matokeo.
 
Mzee Yanga na Simba bado hazijapata vipimo halisi kwa levels zao,Huku ni kusherehekea point 3 sababu tuko kwenye mbio za kukusanya point lakini team yakuifunga mazembe pale sijaona
Hivo vipimo halisi ni vipi? Maana Simba ina point 6 kwa group lake mpaka muda huu.
 
Haaahaa 😊 ☺️ yaani ULICHO KIELEZEA UMENIKUMBUSHA KILIMO CHA WATERMELON πŸ‰ πŸ‰ πŸ‰ πŸ‰ KWENYE MAKARATASI πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£πŸ˜…

Ngoja tuonee.
Yanga haendi popote na hata engineer hersi analijua Hilo na ndio maana siku hizi Hana furaha..
 
Hivo vipimo halisi ni vipi? Maana Simba ina point 6 kwa group lake mpaka muda huu.
Utalinganisha mbingu na ardhi...kaa ukijua SIMBA NDIO WAKALI WA HIZI KAZI na nitimu inayo ogopwa na kuitangaza vyema Tanzania

Whatcha & see Jan 5 🦁 🦁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…