Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Vurugu zimezuka katika Tamasha la Kitaifa la maigizo huko Nakuru nchini Kenya, baada ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Butere kukataa kucheza tamthilia yao ya kutatanisha "Echoes of War’’, mchezo ambao unaangazia mapambano ya Vijana kuhusu uhuru wa kiraia, utawala na haki ya kijamii.
Polisi walitumia Mabomu ya kutoa machozi, kuwaondoa Wanafunzi wa Shule hiyo, kutoka kwenye eneo la Tamasha la Muziki, Sanaa na maigizo awamu ya Kitaifa, linaloendelea katika ukumbi wa Melvin Jones, kaunti ya Nakuru.
Machafuko yalizuka Alhamisi, Aprili 10, tukio hilo lilisababisha taharuki kubwa huku wanafunzi wakionekana wakilia na kuondoka kwa huzuni baada ya kunyimwa fursa ya kutumbuiza.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa, Raymond Omollo, ametetea hatua hiyo ya serikali kuzuia igizo hilo, akieleza kuwa taifa linakumbwa na "Utamaduni unaopenya wa ukosefu wa maadili." Akiwa kwenye mkutano mkuu wa Chama cha Maafisa wa Utawala (ANGAK), Omollo aliwataka viongozi wa serikali kuwa mstari wa mbele katika kurejesha nidhamu mashuleni, maofisini na katika maisha ya kila siku.
Machafuko haya yameibuka siku chache baada ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Marekani barani Afrika (USIU–Africa) kuandaa tukio la Culture Day, ambapo wanafunzi wa mataifa mbalimbali walionyesha tamaduni za nchi zao. Wanafunzi kutoka Tanzania walionekana wakiwa wamevaa vijora na kucheza Baikoko, jambo lililotikisa mitandaoni kuhusu maadili na uhuru wa kuonesha utamaduni.
Machafuko yalitokea saa chache baada ya wanahabari sita kujeruhiwa walipokuwa wakiripoti tamasha katika Shule ya Wasichana ya Kirobon, hali iliyozua wasiwasi kuhusu usalama na uhuru wa habari. Polisi walifunga milango ya ukumbi mara baada ya basi la Butere Girls kuwasili, na kuwaacha watazamaji na wanahabari nje. Igizo lenye utata, Echoes of War, lililotungwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa UDA, Cleophas Malala, na kuzua mjadala mkali Kenya, likitajwa kugusa masuala nyeti ya kijamii na kisiasa. Huku wengi wakihoji uhuru wa kujieleza na nafasi ya sanaa katika jamii.
Chanzo: capitalfm.co.ke
===
Butere Girls High School students on Thursday, April 10, opted not to perform their highly anticipated play Echoes of War at the Kenya National Drama and Film Festivals, citing a string of frustrations and alleged intimidation.
In a veiled refrence to developments at the National Drama and Film Festival in Nakuru, Omollo argued that the country faces a “creeping culture of disorder” he said required an intervention.
Speaking at the 9th Annual General Meeting of the Association of National Government Administrators of Kenya (ANGAK) in Machakos, Omollo urged government administrators to lead efforts in restoring discipline in public institutions and daily life.
“There is a culture currently creeping across the country where order is lacking — in schools, offices, and leadership,” Omollo said.
Polisi walitumia Mabomu ya kutoa machozi, kuwaondoa Wanafunzi wa Shule hiyo, kutoka kwenye eneo la Tamasha la Muziki, Sanaa na maigizo awamu ya Kitaifa, linaloendelea katika ukumbi wa Melvin Jones, kaunti ya Nakuru.
Machafuko yalizuka Alhamisi, Aprili 10, tukio hilo lilisababisha taharuki kubwa huku wanafunzi wakionekana wakilia na kuondoka kwa huzuni baada ya kunyimwa fursa ya kutumbuiza.
Chanzo: capitalfm.co.ke
===
Butere Girls High School students on Thursday, April 10, opted not to perform their highly anticipated play Echoes of War at the Kenya National Drama and Film Festivals, citing a string of frustrations and alleged intimidation.
Interior and National Administration Principal Secretary Raymond Omollo has defended the government’s move to restrict the performance of Echoes of War by Butere Girls High School.In a veiled refrence to developments at the National Drama and Film Festival in Nakuru, Omollo argued that the country faces a “creeping culture of disorder” he said required an intervention.