Pre GE2025 Machi 8 tunaadhimisha Siku ya Wanawake au Siku ya Samia? Picha zake kutapakaa kwenye vitenge vya maadhimisho ni ili iwe nini?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Yaani hawa Marais wa Awamu ya 5 na 6 wameleta mambo ya AJABU na AIBU kabisa nchini

Sijui nani aliwaambia ukiwa Rais wa nchi hii basi wewe ndio ALPHA na OMEGA..una haki ya kusifiwa na kupambwa asubuhi, mchana na hadi usiku..AIBU
Mbunge akiwa Bungeni anamuomba Rais barabara; Diwani kule Nyamanoro anamuomba Rais barabara; Mwananchi hapo Naberera anamuomba Rais barabara. Sasa viongozi wanashindana kuomba!
 
Wakuu,

Hii ni kali. Yaani kila kitu sasa hivi ni Samia, Samia, Samia! Kwani kampeni zimeanza wengine hatuna taarifa?

Msajili wa Vyama vya Siasa ni zaidi ya 0. Kuna maana gani ya kuwa hapo ofisini kama msumeno wako unakata sehemu moja tu wengine haufiki?

Yaani utafikiri ndio tunasherekea birthday ya Samia, kujaza sura Samia halafu mseme ni Siku ya Wanawake huo ni uzindiki. Yaani mnafosi mtu akubalike mpaka mnaboa. Hata haistui zaidi ya kuonekana wajinga tu.

Halafu ikifika muda wa kutoa tathimi za uchaguzi utaona wale chuchunge wakisema uchaguzi ulikuwa wa huru na haki. Unakuaje wa haki wakati rafu zimeanza mapema hivi?

Sasa hiki ni nini?🤦‍♀️🤮🚮🚮

Tutakuwa kwenye kariakoo derby hiyo cku watajua wenyewe
 
Mbunge akiwa Bungeni anamuomba Rais barabara; Diwani kule Nyamanoro anamuomba Rais barabara; Mwananchi hapo Naberera anamuomba Rais barabara. Sasa viongozi wanashindana kuomba!
Hakika ni mambo ya kijinga Sana bunge limesahau wajibu wake CCM ni vipofu
 
Dkt. Gwajima D kila mtu ana mama yake awe hai au amefariki , hii ni siku ya kidunia kila mtu amkumbuke mama yake huyu sio mama wa watanzania huyu ni mama yake Abdul & Wanu.

Diversionary tactics kama hizi wala hatuwezi kuzikubali lengo la hili adhimisho lipotoshwe you're more than that.

Hivyo kila mtu akumbushwe tu kumkumbuka mama yake jinsi atakavyowiwa.
2699115_90876541.jpg
 
View attachment 3225885
Nadhani sijaelewa, tutakapoanza elimu kwa umma kuhusu malengo ya mkutano wa Beijing mwaka 1995 ambapo pia liko lengo la wanawake na uongozi, hapo ndiyo hata wewe utaelewa zaidi kuhusu mafanikio eneo hilo. Iwapo wewe hapo hutaelewa na wengine wakaelewa, basi tutakubaliana kutofautiana. Haya usiku mwema, ahsante kwa kumbukumbu ya picha 💁
 
Nadhani sijaelewa, tutakapoanza elimu kwa umma kuhusu malengo ya mkutano wa Beijing mwaka 1995 ambapo pia liko lengo la wanawake na uongozi
Itapendeza mkitoa elimu hiyo na pia dhima kuu ya siku hiyo ikabaki ilivyo na sio kumpromote Samia.

Kuna wanawake wengi walikuwepo kwenye harakati za uhuru kama kina Bibi Titi Mohamed hii ni siku yao ingepaswa waenziwe sio kuifanya siku ionekane imemezwa na Samia kama mlivyoweka vitenge hivyo.

Kwani Tanzania hamna "Iron ladies"?

Mfanye adhimisho kuna wanawake wamefanya makubwa katika afya ,siasa mazingira, habari, sheria, haki za binadamu na kadhalika.
, hapo ndiyo hata wewe utaelewa zaidi kuhusu mafanikio eneo hilo. Iwapo wewe hapo hutaelewa na wengine wakaelewa, basi tutakubaliana kutofautiana.
Niko tayari kama kuna kipya cha kuelimishwa kuhusu hii siku ila msiitumie kumfanyia Samia promotion na sifa asizostahili.
Haya usiku mwema, ahsante kwa kumbukumbu ya picha 💁
Ahsante usiku mwema kwako, hapa nilipo ni mchana .
 
Nimeamini ukiwa ccm akili zako lazima uzitoe hata huyu Dokta gwajima kawa chawa pro pamoja na elimu yake?
Ndugu yangu kwanza salaam. Halafu ujue ni hivi, kama jambo ni la msingi, na Lina hoja ya msingi kwenye ajenda ya msingi, hata kama hutalipenda, mimi huwa nalifanya kwa uhuru.

Fuatilia elimu kwa umma kuhusu historia ya mkutano wa Wanawake Beijing mwaka 1995 uone maazimio na mafanikio ya Tanzania kwenye wanawake na uongozi. Hatuko kiitikadi, tuko Kitaifa zaidi, tunaongea na Dunia kama Taifa kuwa, Tanzania kwenye eneo la wanawake na uongozi tumefika kitaifa zaidi. Nchi zingine wamekwama.

Sasa hapo unakasirika nini? 😅Katika hili, tukubaliane kutofautiana✍🏻
 
Itapendeza mkitoa elimu hiyo na pia dhima kuu ya siku hiyo ikabaki ilivyo na sio kumpromote Samia.

Kuna wanawake wengi walikuwepo kwenye harakati za uhuru kama kina Bibi Titi Mohamed hii ni siku yao ingepaswa waenziwe sio kuifanya siku ionekane imemezwa na Samia kama mlivyoweka vitenge hivyo.

Kwani Tanzania hamna "Iron ladies"?

Mfanye adhimisho kuna wanawake wamefanya makubwa katika afya ,siasa mazingira, habari, sheria, haki za binadamu na kadhalika.

Niko tayari kama kuna kipya cha kuelimishwa kuhusu hii siku ila msiitumie kumfanyia Samia promotion na sifa asizostahili.

Ahsante usiku mwema kwako, hapa nilipo ni mchana .
Kwanza nakupongeza kwa kuwa na fikra huru za kukubali kupokea elimu. Kule x tangu jana ilikuwa ni maswali na majibu na huku nitakuja na mwananchi space nitaenda. Mwisho wa siku historia imeshajiandika kuwa, kwenye maazimio ya ulingo wa Beijing, mwaka 1995, Tanzania ilipoahidi mojawapo ya Azimio la Wanawake na Uongozi, tumetekeleza hadi kitaifa. Tumezishinda nchi nyingi. Hili litakuwa swali la historia kwa watoto wetu vizazi na vizazi na litajibiwa. Sasa mwaka wa 5 wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya wanawake duniani kuangukia kwenye mwaka wa uchaguzi, isilete tafsiri kuwa, tuko kiitikadi, hapana, ni kitaifa, tangu mwaka 1995 hizo 5 ndiyo zimetufikisha hapa kwenye 2025.

Tukutane space siku moja ratiba inakuja. Ukweli uwe ukweli hata kama tutatofautiana...... ✍🏻
 
Ni muendelezo wa kampeni ya urais.
Siyo kweli, kama Mkutano wa Wanawake kule Beijing ungefanyika mwaka 1993 basi maadhimisho ya kitaifa ya kila miaka 5 yangeangukia mwaka 2023. Sasa mkutano ulikuwa mwaka 1995. Tuwe tunauliza historia jamani ndiyo Sasa tuje na maoni. Haya usiku mwema tuje tukutane space siku moja kwa elimu zaidi. Maswali na majibu mubashara ✍🏻
 
Kwanza nakupongeza kwa kuwa na fikra huru za kukubali kupokea elimu. Kule x tangu jana ilikuwa ni maswali na majibu na huku nitakuja na mwananchi space nitaenda. Mwisho wa siku historia imeshajiandika kuwa, kwenye maazimio ya ulingo wa Beijing, mwaka 1995, Tanzania ilipoahidi mojawapo ya Azimio la Wanawake na Uongozi, tumetekeleza hadi kitaifa. Tumezishinda nchi nyingi. Hili litakuwa swali la historia kwa watoto wetu vizazi na vizazi na litajibiwa. Sasa mwaka wa 5 wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya wanawake duniani kuangukia kwenye mwaka wa uchaguzi, isilete tafsiri kuwa, tuko kiitikadi, hapana, ni kitaifa, tangu mwaka 1995 hizo 5 ndiyo zimetufikisha hapa kwenye 2025.

Tukutane space siku moja ratiba inakuja. Ukweli uwe ukweli hata kama tutatofautiana...... ✍🏻
Haina shaka mimi siku space ikiitishwa nitajoin kuchangia mawazo yangu.
 
Ndugu yangu kwanza salaam. Halafu ujue ni hivi, kama jambo ni la msingi, na Lina hoja ya msingi kwenye ajenda ya msingi, hata kama hutalipenda, mimi huwa nalifanya kwa uhuru.

Fuatilia elimu kwa umma kuhusu historia ya mkutano wa Wanawake Beijing mwaka 1995 uone maazimio na mafanikio ya Tanzania kwenye wanawake na uongozi. Hatuko kiitikadi, tuko Kitaifa zaidi, tunaongea na Dunia kama Taifa kuwa, Tanzania kwenye eneo la wanawake na uongozi tumefika kitaifa zaidi. Nchi zingine wamekwama.

Sasa hapo unakasirika nini? 😅Katika hili, tukubaliane kutofautiana✍🏻
Kwanza nipo salama mh.Halafu nashukuru sana kwa kunijibu na kuwajibu wengine. Daima nitakupongeza kwa kuwa na muda huu wa kupitia maoni yetu yawe yawe chanya au hasi wajibu wako kama kiongozi nikuchukua yaliyo mazuri na kuyafanyia kazi,hongera sana.

Nanyi mmezidi kila kitu mama mama pungezeni uchawa na mmwambie ukweli hapendwi na watanzania na wewe unalijua hili ndio maana mmepitisha kimagumashi.Mlijua wazi hata kama angeshindanishwa nawewe zamani za kale ungemshinda.Kwani uongo?
 
Magufuri alitumaliza mjinga yule
Huwa nawadharau sana wapumbavu kama wewe mnaomlaumu mtu ambaye ameshakufa kwa upuuzi unaofanywa na awamu hii ya samia.

Huwa nawadharau mno na kuwaona nyie ni wapumbavu wa mwisho na dhaifu sana kwa kushindwa kuchukua hatua yoyote kwa jambo ambalo hamfurahishwi nao awamu hii.

Kwanza hata hili jina lako halikufai eti "wagumu tunadumu" una ugumu sana wewe mchumba tu mtoto laini laini kama kende za mtoto mchanga.
 
Ndugu yangu kwanza salaam. Halafu ujue ni hivi, kama jambo ni la msingi, na Lina hoja ya msingi kwenye ajenda ya msingi, hata kama hutalipenda, mimi huwa nalifanya kwa uhuru.

Fuatilia elimu kwa umma kuhusu historia ya mkutano wa Wanawake Beijing mwaka 1995 uone maazimio na mafanikio ya Tanzania kwenye wanawake na uongozi. Hatuko kiitikadi, tuko Kitaifa zaidi, tunaongea na Dunia kama Taifa kuwa, Tanzania kwenye eneo la wanawake na uongozi tumefika kitaifa zaidi. Nchi zingine wamekwama.

Sasa hapo unakasirika nini? 😅Katika hili, tukubaliane kutofautiana✍🏻
Sasa mheshimiwa habari ya usiku huu? Haya mbona hiki ulichokiandika hakina uhusiano na kiini cha mada?

Kuna uhusiano gani hiyo siku ya wanawake na uwepo wa picha ya samia kwenye hivyo vitenge?

Na pia unajaribu kulinganisha mafanikio ya wanawake kiongozi hapa nchini kwetu na wengine kisha una hitimisha eti hao wengine wamekwama una maanisha hasa ikiwa kama huyu wetu tuliyenaye hapa huo uraisi wenyewe aliuokota tu na hakuna aliyemtarajia kama kuna siku atakalia hicho kiti?

Sisi tunatofauti gani na hao unasema wamekwa ikiwa bado kuna ombwe kubwa la uongozi kati ya ke na me hasa kwenye nafasi za kuchaguliwa?
 
Kuna mda nahisi hata Samia mwenyewe akikaa peke yake anacheka sana na kufurahi kuongoza watu wapuuzi , wajinga wasiojitambua
Hata mimi huwa naamini kabisa yeye mwenyewe hakutegemea kama majitu ya bara yatakuwa yana msujudia kijinga jinga hivi mpaka yana utweza utu wao.
 
Sasa mheshimiwa habari ya usiku huu? Haya mbona hiki ulichokiandika hakina uhusiano na kiini cha mada?

Kuna uhusiano gani hiyo siku ya wanawake na uwepo wa picha ya samia kwenye hivyo vitenge?

Na pia unajaribu kulinganisha mafanikio ya wanawake kiongozi hapa nchini kwetu na wengine kisha una hitimisha eti hao wengine wamekwama una maanisha hasa ikiwa kama huyu wetu tuliyenaye hapa huo uraisi wenyewe aliuokota tu na hakuna aliyemtarajia kama kuna siku atakalia hicho kiti?

Sisi tunatofauti gani na hao unasema wamekwa ikiwa bado kuna ombwe kubwa la uongozi kati ya ke na me hasa kwenye nafasi za kuchaguliwa?
Swali lako zuri kuhusu Kwa nini picha ya Rais kwenye kitenge; naomba nikuelimishe, ni kwa Sababu kwenye Azimio la Beijing la wanawake na uongozi, tumepata alama ya mwanamke kiongozi ngazi ya kitaifa kuanzia cheo cha Makamu wa Rais na Sasa Rais. Inabidi Dunia ijue kuwa tumetekeleza. Hivyo kwenye eneo hili sasa, ngazi ya juu kabisa ya kiongozi mwanamke ni Rais ambaye anakuwa sasa alama ya mafanikio kwenye Azimio hilo. Ikumbukwe, hata kama tungeadhimisha miaka 30 ya Beijing mfano mwaka 2020, bado alama ingekuwa ya Makamu wa Rais enzi hizo. Tutaendelea kuelimisha zaidi kuna kipindi kimeandaliwa kuhusu safari ya utekelezaji wa maazimio ya Beijing na mafanikio yake
 
Back
Top Bottom