godson njamakuya
Senior Member
- Mar 6, 2021
- 170
- 196
Awali ya yote niusifu uongozi mzima wa Mkoa wa Arusha kwa hatua iliyochukua ya kuwatengenezea wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama Wamachinga maeneo maalum kwa ajili ya kufanya shughuli zao za utafutaji wa riziki.Kiukweli nimeona kazi kubwa iliyofanyika ya ujenzi wa mabanda ya Wamachinga, yenye kiwango cha hali ya juu hali ambayo itawafanya wafanyabiashara hao waliokuwa wamezagaa kila kona ya jiji la Arusha kufanya shughuli zao kwa utulivu pasipo kusumbuliwa na mgambo wa jiji. Nina imani kubwa kuwa hadhi ya Geneva of Africa inarudi sasa muda si mrefu.
Mimi ni mzaliwa wa Arusha eneo la Mianzini ya juu, japo kwa sasa niko Kibaha kimajukumu, lakini huwa ninapenda kufuatilia kwa karibu matukio yote yanayojiri katika Mkoa wangu,mfano juzi nilisikia Mkoa wa Arusha uliongoza kwa ukusanyaji wa mapato ya Serikali kitaifa, hii inaonyesha ni jinsi gani Mkurugenzi wa jiji Bw John Pima anavyowajibika kwenye nafasi yake. Sasa mlioko Arusha tupeni mrejesho hali ilivyo katika mitaa ya jiji la Arusha.
Nawasilisha