Machinga: Jeshi kubwa lenye uwezo wa kuamua Mustakabali wetu kisiasa

Machinga: Jeshi kubwa lenye uwezo wa kuamua Mustakabali wetu kisiasa

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Neno Machinga linasimama hapa kwa niaba ya kada yote ya chini, yaani wavuja jasho.

Humo kuna Boda boda, wapiga debe, mama lishe, makuli, vibarua, nk, wakiwamo pia machinga wenyewe.

Machinga wanapotoa Somo, Makamanda tunakwama Wapi?

Agenda #1: (Si maneno yangu)
----------------------------------
IMG_20211104_053248_500.jpg

===================

Agenda #2:
-----------------------------------
IMG_20211104_044405_159.jpg

IMG_20211104_035911_135.jpg

IMG_20211104_044459_006.jpg

===================
Rejea:

Asili ya uzi huu ni comments #32 kama Agenda #1 na #33 kama Agenda #2 katika uzi huu:

Huyu ndiye mwanzilishi wa chama kipya cha Umoja

Credit kwako Abuu hanifa
 
wazo mfu kwa nchi kama Tanzania..... mpaka sasa tungeona juhudi za wazi kutoka kwenu ila kama juhudi ni kuanzisha chama cha sisa MMEFELI kabla ya kuanza.

by the way.... tuwape uongozi ili mrudi kufunga barabara zetu au mje na sera ileile ya kutengeneza mazingira bora????
 
Usiache kupaona pale:

1. Kuleta mabadiliko si lelemama.
2. Hawa ndiyo waliokuweza kuliko vunjika shoka lakini mpini ukabaki pale pale.
3. Zanzibar '64 ni mfano mzuri. Huko Russia, Ufaransa na China cha mtoto au vipi?
4. Haya ni maamuzi magumu.
 
Hivi tatizo kubwa la Taifa letu ni lipi?

1) Wenye kipato kidogo, aka machinga, au wasio kwenye mfumo rasmi, kudai fursa za kiuchumi?

2) Wafanya biashara kudai kodi za kutengeneza faida kubwa?

2) Asilikia 70% ya WaTz walioko vijijini kudai huduma bora za jamii (barabara, maji, elimu, nishati, nk)?

3) Wahitimu wa elimu wadai ajira?

4) Wanasiasa wanaodai demokrasia ya Uhuru usio na mipaka na Haki bila wajibu (au Katiba mpya)?

5) Wanasiasa wenye uchu wa madaraka wadai Tume huru ya uchaguzi?

6) na kadhalika
 
Nionavyo kama hao machinga wetu nao wanatoka kwenye jamii yetu hii iliyo na waoga kila upande sioni ni kwa namna gani hayo mawazo yanaweza kuwa active yakafanyiwa kazi.

Kulinganisha machinga wetu na hao wa nchi za nje ulizotaja hapo bado haileti maana kwasababu huko nje asilimia kubwa wameamka; hawana uoga wa kikondoo kama tulionao sisi, kwao mabadiliko hayamsubiri mwingine kama tufanyavyo sisi, wao wanajua mabadiliko yanaanza na kila mmoja wao.
 
Hivi tatizo kubwa la Taifa letu ni lipi?
1) Wenye kipato kidogo, aka machinga, au wasio kwenye mfumo rasmi, kudai fursa za kiuchumi?...

Tatizo kubwa la taifa letu liko hapa:

Haki, usawa, uhuru na demokrasia.

Ndiyo maana ni heri nyumbani kuliko utumwani au ugenini na nyumbani ni nyumbani hata kama ni kwenye shimo.

Kwa hakika kama wewe ni mminyaji haki uhuru na demokrasia au mnufaika kwenye kutokuwepo usawa au kutokuwapo hayo:

"vipi unaweza kuona haya ni matatizo sugu na makubwa yenye kuhitaji ugatuzi wake wa haraka ndugu mwengeso?"
 
Nionavyo kama hao machinga wetu nao wanatoka kwenye jamii yetu hii iliyo na waoga kila upande sioni ni kwa namna gani hayo mawazo yanaweza kuwa active yakafanyiwa kazi...
Umeiona Zanzibar mle mkuu? Zanzibar ni sehemu ya JMT.
 
Umeiona Zanzibar mle mkuu? Zanzibar ni sehemu ya JMT.
Machinga wa Zanzibar waliwahi kufanya nini? au ndio yale mapinduzi yao ya 1964? hii kitu siiamini bado kama ili ufanikiwe utekelezaji wake unategemea kundi fulani tu la watu huku wengine wakiwa watazamaji.
 
Mkuu Zanzibar 1964 "Lumpen Proletariats" waliyakataa manyanyaso.

Pamoja na kuwa waliokuwa wengi walishinda katika chaguzi zote zilizokuwa zikifanyika - wizi, ghiliba na janja janja zilitamalaki kuzuia mabadiliko.

Hakukuwa na haki, uhuru, usawa wala demokrasia. Utawala uliokuwapo ukiendekeza utwana na ubwana. Matabaka ya walio navyo dhidi ya wasio navyo yakiendelea kushamiri.

Hali kama hii hii unayoiona kwetu leo.

Kumbuka siasa ndiyo kila kitu.

Haki, usawa, uhuru na demokrasia havitapatikana kupitia Jembe la mkono, kuchapa kazi au kujenga uchumi.
 
Acha uchochezi, mbona Mama anatatua matatizo ya wananchi? Ajira zimeanza kumwagwa bado projects kibao zinakuja.
 
Acha uchochezi, mbona Mama anatatua matatizo ya wananchi? Ajira zimeanza kumwagwa bado projects kibao zinakuja.

Ninakazia:

"Haki, usawa, uhuru na demokrasia havitapatikana kupitia Jembe la mkono, kuchapa kazi au kujenga uchumi."

Wewe huoni hivyo ndugu mjumbe?
 
Tatizo kubwa la taifa letu liko hapa:

Haki, usawa, uhuru na demokrasia...

Taasisi ndogo kabisa duniani ni familia (Baba, mama na watoto). Ustawi wa hiyo taasisi unategemea dhana yako hiyo ya Haki, usawa, uhuru na demokrasia? Ufafanuzi wako utatoa mwanga kitaifa ni nini tatizo la msingi, kwa kuwa Familia hujenga Jamii ambayo hutengeneza Taifa
 
Hivi tatizo kubwa la Taifa letu ni lipi?

1) Wenye kipato kidogo, aka machinga, au wasio kwenye mfumo rasmi, kudai fursa za kiuchumi?

2) Wafanya biashara kudai kodi za kutengeneza faida kubwa?

2) Asilikia 70% ya WaTz walioko vijijini kudai huduma bora za jamii (barabara, maji, elimu, nishati, nk)?

3) Wahitimu wa elimu wadai ajira?

4) Wanasiasa wanaodai demokrasia ya Uhuru usio na mipaka na Haki bila wajibu (au Katiba mpya)?

5) Wanasiasa wenye uchu wa madaraka wadai Tume huru ya uchaguzi?

6) na kadhalika
Kwa haraka haraka nikiwa ninesimama kwenye daladala....

Tatizo kubwa tulonalo ni kukosa dira kama taifa.

Dira, vision, compass...

Ndege ikikosa dira itapoteza mwelekeo, ndege ikikosa dira itapotea mwelekeo. Taifa likikosa dira litapotea mwelekeo.

Taifa likishakuwa na dira, litatengenezia imani (itikadi) ya kufika tuendako.

Baadae litatengeza Sera, baadae mipango, mwisho kutakuwa na utekelezaji.

Dunia ya Leo ili ufanikishe haya yahitaji taifa litengeze imani (itikadi) itakayoweza kuyashirikisha makundi yote yanayounda taifa hili.

Machinga ni jeshi kubwa lenye mchanganyiko wa watu wenye vipawa na weledi.

Ndilo jeshi pekee naliamini lina uwezo wa kulivusha taifa
 
Taasisi ndogo kabisa duniani ni familia (Baba, mama na watoto). Ustawi wa hiyo taasisi unategemea dhana yako hiyo ya Haki, usawa, uhuru na demokrasia? Ufafanuzi wako utatoa mwanga kitaifa ni nini tatizo la msingi, kwa kuwa Familia hujenga Jamii ambayo hutengeneza Taifa

Ukweli hukabiliwa haisaidii kuukimbia:

"Haki, uhuru, usawa na demokrasia havipo nchini."

Hili ni tatizo kubwa, la msingi lenye kuhitaji ufumbuzi wa dharura.
 
Back
Top Bottom