Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Mtu unajipitia zako mara umeshikwa bega, au unavutwa nguo, mkono au kiuno, dada hii inakutosha au hii itakupendeza kwani huwezi kuniambia nikasikia tukaelewana bila kunigusa?
Machinga wa Karikaoo, Karume, Mbezi ya Kimara jumlisha na wale wapiga debe ndo kuzidi kabisa, Mwenge yaani wanakera sana, mbaya zaidi wanaona sawa tu na ukiwaambia usiniguse wanakudharirisha utasikia usishikwe we nani mtu mwenyewe mbaya, au hujapendeza.
Mfano, kuna siku nilikuwa na rafiki yangu Karume tunanunua bidhaa zetu machinga mmoja akamshika rafiki yangu kwa kuchomeka kidole ndani ya belti la sketi yake eti anamuonesha urembo yafiki yangu alikasirika mpaka leo hana hamu ya kwenda Karume.
Wao wanaona kawaida kumgusa, kumkumbatia, wengine kumbusu mwanamke asiye mjua wala kuwa na mazoea naye huko babarani na watu wakaona ni kawaida hata kama mwanamke huyo hataonekana kuridhishwa na kitendo hicho.
Machinga wanaouza bidhaa mitaani huwashika wanawake ikiwa kama njia ya wao kuwatangazia bidhaa zao kitu kama hicho si sahihi kwa kuwa wanaweza kuwatangazia bidhaa bila kugusa miili yao, wengine huenda mbali zaidi pale inapotokea mwanamke akaonesha kuwa hakupenda kuguswa huanza kumdhalilisha kwa kusema unaringa kitu gani na wakati wewe ni mbaya tu, usigushwe wewe nani kwani nk.
Barabarani, kwenye vyombo vya usafiri na popote anapopita mwanamke anaweza kuvutwa nguo huo ni udhalilishaji wa makusudi kwa kuwa hakuna hatua zinazochukuliwa kumnusuru na kero hii.
Mwanamke amekuwa mhanga katika jambo hilo hali inayomyima kuwa huru kutembea maeneo mengine kwa kuwa wanaume hawaoni kuwa wana mipaka na mwili wa mwanamke wao huona kuwa mwili wa mwanamke wanaweza kuugusa wakati wowote na hakuna sheria yoyote watakayoadhibiwa nayo.
Wengine huwashika hadi sehemu nyeti za mwili na hakuna yeyote wa kumtetea mwanamke anayepatwa na adha ya ukatili kama huu hali ambayo inamwathiri kisaikolojia na kumfanya akose kujiamini kutembea akiwa huru.
Ifike hatua jamii ielewe kuwa kumgusa au kumshika mtu bila ridhaa yake ni kumvunjia heshima kwani kila mtu hupenda kuwa huru na kufanya kitu ambacho yeye binafsi karidhia.
Pamoja na kuwa kuna sheria ya kutokumgusa mwanamke na matendo kama hayo ni kosa kisheria na adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka 5 jela au faini ya sh. 300,000 lakini ukimshika zaidi maeneo nyeti kama kifuani ni kifungo cha miaka 15 je, sheria hii ni butu mbona ndio kwanza matendo yanaongezeka?
Nani anaitekeleza au juhudi gani zinafanyika katika kuwawajibisha watendaji ili waache au kuwaelimisha wajue kuwa wanatenda kosa kumshika mwanamke bila ridhaa yake?
Jamii ijue kuwa Kumshika, kumbusu, kumkumbatia au kumgusa mwanamke bila ridhaa yake ni udhalilishaji. Inabidi upigiwe kelele.