Machinga kuwashikashika wanawake inakera sana!

Machinga kuwashikashika wanawake inakera sana!

Nna miaka kama 10 sijaenda karume aisee sijawai kuona sehem yenye karaha kama ile yani mtu atakushika mkono hataki kukuachia tafrani tupu
Usiombe muwe wawili, mwenzio ameshasonga mbele amekaribia kupotelea huko kwa watu wewe bado upo umeng'ang'aniwa mkono unavutana na mtu usiyemjua.

Kulingana na vipato vyetu tunatamani sana kwenda karume, mwenge, congo-kariakoo kununua vitu kwa bei chee lakini hapana aiseee! Wacha tubanane huku kwenye maduka wanakotupiga. Kero tupu, mtu unavutana, unajibishana, unagombana hadi utoke umechoka hoiii!
 
Ni kero sana kwakweli.
Nachukizwa sana na hii tabia. Hata kama mtu nafahamiana naye mambo ya kuparamiana paramiana kwa kushikana sipendi.
 
Ila waTz sio waelewa kabisa, nimesoma comments mtu anajiona kabisa kuwa yuko entilted kukushika eti kwasababu ukienda sehemu za starehe huwa unakubali kushikwa 😅 Kitu kinachoitwa consent ninyi hamkijui wala kukielewa kabisa?

Siku mkitoka kwenda kutembea nchi za walioendelea mtaishia kupelekwa mahakamani, Maana mtajiona mna haki ya kumgongea jirani mlango, kukatiza kwenye makazi ya watu, Kumtongoza mtu tu ukimkuta yuko pekeyake amejikalia... Jifunzeni ustaarabu aisee!
 
Usiombe muwe wawili, mwenzio ameshasonga mbele amekaribia kupotelea huko kwa watu wewe bado upo umeng'ang'aniwa mkono unavutana na mtu usiyemjua.

Kulingana na vipato vyetu tunatamani sana kwenda karume, mwenge, congo-kariakoo kununua vitu kwa bei chee lakini hapana aiseee! Wacha tubanane huku kwenye maduka wanakotupiga. Kero tupu, mtu unavutana, unajibishana, unagombana hadi utoke umechoka hoiii!
Yani adi unajuta kwanini ulienda
 
Tatizo hamchukui hatua,sheria zpo ni kuripoti mtu akamatwe n then mahakaman kisha hukumbili iwe fundisho....lkn mkiacha hvyo mkaja kulalalmika uku hakuna cha maana ....business itaendelea as usual
waote hao wanapenda kutiwa vidole chunguza machinga na wapiga debe wanavio mzoea haraka mvaa kimini na kisuruali cha kubana
 
Mimi huwa najichomoa fasta kabla mtuehajanishika
Tena akijitoa ufahamu namm najitoa hivyohivyo bila kuzungumza chochote.
Huwa nakuwa mkali kwa ishara na natembea kwa mwendokasi.

Ila hii tabia inakera sana.
chunguza uvaaji wako wale awakoseagi
 
View attachment 2539330
Mtu unajipitia zako mara umeshikwa bega, au unavutwa nguo, mkono au kiuno, dada hii inakutosha au hii itakupendeza kwani huwezi kuniambia nikasikia tukaelewana bila kunigusa?

Machinga wa Karikaoo, Karume, Mbezi ya Kimara jumlisha na wale wapiga debe ndo kuzidi kabisa, Mwenge yaani wanakera sana, mbaya zaidi wanaona sawa tu na ukiwaambia usiniguse wanakudharirisha utasikia usishikwe we nani mtu mwenyewe mbaya, au hujapendeza.

Mfano, kuna siku nilikuwa na rafiki yangu Karume tunanunua bidhaa zetu machinga mmoja akamshika rafiki yangu kwa kuchomeka kidole ndani ya belti la sketi yake eti anamuonesha urembo yafiki yangu alikasirika mpaka leo hana hamu ya kwenda Karume.

Wao wanaona kawaida kumgusa, kumkumbatia, wengine kumbusu mwanamke asiye mjua wala kuwa na mazoea naye huko babarani na watu wakaona ni kawaida hata kama mwanamke huyo hataonekana kuridhishwa na kitendo hicho.

Machinga wanaouza bidhaa mitaani huwashika wanawake ikiwa kama njia ya wao kuwatangazia bidhaa zao kitu kama hicho si sahihi kwa kuwa wanaweza kuwatangazia bidhaa bila kugusa miili yao, wengine huenda mbali zaidi pale inapotokea mwanamke akaonesha kuwa hakupenda kuguswa huanza kumdhalilisha kwa kusema unaringa kitu gani na wakati wewe ni mbaya tu, usigushwe wewe nani kwani nk.

Barabarani, kwenye vyombo vya usafiri na popote anapopita mwanamke anaweza kuvutwa nguo huo ni udhalilishaji wa makusudi kwa kuwa hakuna hatua zinazochukuliwa kumnusuru na kero hii.

Mwanamke amekuwa mhanga katika jambo hilo hali inayomyima kuwa huru kutembea maeneo mengine kwa kuwa wanaume hawaoni kuwa wana mipaka na mwili wa mwanamke wao huona kuwa mwili wa mwanamke wanaweza kuugusa wakati wowote na hakuna sheria yoyote watakayoadhibiwa nayo.

Wengine huwashika hadi sehemu nyeti za mwili na hakuna yeyote wa kumtetea mwanamke anayepatwa na adha ya ukatili kama huu hali ambayo inamwathiri kisaikolojia na kumfanya akose kujiamini kutembea akiwa huru.

Ifike hatua jamii ielewe kuwa kumgusa au kumshika mtu bila ridhaa yake ni kumvunjia heshima kwani kila mtu hupenda kuwa huru na kufanya kitu ambacho yeye binafsi karidhia.

Pamoja na kuwa kuna sheria ya kutokumgusa mwanamke na matendo kama hayo ni kosa kisheria na adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka 5 jela au faini ya sh. 300,000 lakini ukimshika zaidi maeneo nyeti kama kifuani ni kifungo cha miaka 15 je, sheria hii ni butu mbona ndio kwanza matendo yanaongezeka?

Nani anaitekeleza au juhudi gani zinafanyika katika kuwawajibisha watendaji ili waache au kuwaelimisha wajue kuwa wanatenda kosa kumshika mwanamke bila ridhaa yake?

Jamii ijue kuwa Kumshika, kumbusu, kumkumbatia au kumgusa mwanamke bila ridhaa yake ni udhalilishaji. Inabidi upigiwe kelele.
Mimi ninadhani hata kina dada nao mbadilike. Muwe wakali inaweza kupunguza tatizo. Wengi mkionesha waziwazi hasira zenu itapungua. Shida mpo weeengi,mnashikwa mnachekacheka tu. Ninadhani ni ule utamaduni wetu wa kutotaka kumuudhi aliye mbele yako kinafiki.

Halafu, mada hii ijadiliwe pamoja na unyambisi wanaotufanyia wadada kwenye misongomano. Mtu kiguo cha uchokozi,nyonyo njenje, pindo ya chupi hii hapa,hadi unaona wanamoishi ibilisi. Tako lainiii, linakugusagusa kwenye daladala. Halafu hawajikazi,gari ikiyumba huyo kajaa kifuani. Mwanaume unabaki kuingiza mkono ✋ mfukoni kuulaza mdude utulie usiibue kesi. Unafika home unaanzia bafuni.

Acheni hizo kina dada
 
Back
Top Bottom