Mzalendo120
JF-Expert Member
- Jul 2, 2022
- 1,842
- 2,410
Yapakeni hayo makabati rangi, futeni vumbi hadi upenuni huko na vyombo mvisafishe msiache kituHivi kwa nini huwa mnaumia sana tukienda kupaka rangi huko? Huwa mnaamini nini??
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yapakeni hayo makabati rangi, futeni vumbi hadi upenuni huko na vyombo mvisafishe msiache kituHivi kwa nini huwa mnaumia sana tukienda kupaka rangi huko? Huwa mnaamini nini??
Nmekuuliza hivi, huwa mnaamini nini tukienda kupata huduma huko?Yapakeni hayo makabati rangi, futeni vumbi hadi upenuni huko na vyombo mvisafishe msiache kitu
Thanks Buddy🤣🤣🤣 I like you
Ninaona kama umekatwa mikono kiasi kwamba huwezi kusugua kucha zako bidadaNmekuuliza hivi, huwa mnaamini nini tukienda kupata huduma huko?
Kwahiyo picha lilimalizikaje sasaKuna siku nimetoka mjini na rafiki yangu nampeleka home wamfahamu,asa kufika mbezi mwisho stend wapiga debe wakaanza kumsumbua rafiki yangu naona walipenda dredi zake walikuwa wanamshobokea rasi rasiiii,wakaanza kumshika mkono heee😲😲 saa ngap rafiki yangu asikasirike,et akataka kupigana na njemba watano🙆🙆🙆.Mimi mda huo pozi limeniisha nawaza akipigana nao ataweza?,afu Mimi ni Kama best yke nitamsaidiaje na niweng siwawezi pia.Ilibidi nim bembeleze ila asira akanomalizia mimi kwann nawatetea 😪😪😪
Uliikosea sana,ningekua mimi hapo ningeinunua shoo yaani tungeungana wawili tungegaragaza hizo njemba mpaka ziite maji mmaKuna siku nimetoka mjini na rafiki yangu nampeleka home wamfahamu,asa kufika mbezi mwisho stend wapiga debe wakaanza kumsumbua rafiki yangu naona walipenda dredi zake walikuwa wanamshobokea rasi rasiiii,wakaanza kumshika mkono heee😲😲 saa ngap rafiki yangu asikasirike,et akataka kupigana na njemba watano🙆🙆🙆.Mimi mda huo pozi limeniisha nawaza akipigana nao ataweza?,afu Mimi ni Kama best yke nitamsaidiaje na niweng siwawezi pia.Ilibidi nim bembeleze ila asira akanomalizia mimi kwann nawatetea 😪😪😪
😂😂😂Daah napendaga marafiki wa hivi baaalaaaMimi huwa nawakung'uta na hamna kitu wananifanya aisee, kuna siku nimeshuka mwenge machinga mmoja akawa ananing'ang'aniza kununua nguo kwake nikamwambia sihitaji nguo akaanza kunishika,kila nikijaribu kumkwepa naona ananizonga, niliweka mkoba begani vizuri nikageuka kama naondoka nikampa teke la nyuma, hajakaa vizuri nikampa side kick, anataka kunyanyuka nikamshika shati nikamnyanyua nikamwambia sasa wewe ulikua unanishika simama hapa unishike vizuri, ikabidi wenzie wamuamulie, nikawaambia msipende kuzoea watu sisi wengine ni waalimu wa taekwondo
Watu walijaa nikasepa zangu wakabaki wanamcheka
😂😂😂 Mwenzio niliona wapo wengi,nikahofia sura yangu isije kuharibiwaUliikosea sana,ningekua mimi hapo ningeinunua shoo yaani tungeungana wawili tungegaragaza hizo njemba mpaka ziite maji mma
Kusuguliwa kucha hapana, naona kinyaa, yaani mtu mikono yake inasugua kucha za kila mtu halafu na mimi nimuwekee miguu yangu kana kwamba mie kilema, hapana huwa nanunua vifaa vyangu najisafisha mwenyewe na kujipaka rangiNinaona kama umekatwa mikono kiasi kwamba huwezi kusugua kucha zako bidada
Sasa pengine rafiki yako alikua na utaalamu wa vita ndio maana hakuogopa😂😂😂 Mwenzio niliona wapo wengi,nikahofia sura yangu isije kuharibiwa
Ila angekuwa mmoja au wawili wangekomaaaa
Ialivyo Waka hawakutegemea,mimi mwenyewe sikutegema Kama anahasira vile.Nili m bembeleza sanaaa wao wakawa washangaa naona waliogapa so tukaondoka Tena nikiwa namvuta mkono jaman alichukia sanaKwahiyo picha lilimalizikaje sasa
Wewe nimwanamke anaejielewa. Vipi shemeji hajamboKusuguliwa kucha hapana, naona kinyaa, yaani mtu mikono yake inasugua kucha za kila mtu halafu na mimi nimuwekee miguu yangu kana kwamba mie kilema, hapana huwa nanunua vifaa vyangu najisafisha mwenyewe na kujipaka rangi
Wale vijana sijui hata hygine yao ipoje, huwa hawavai hata gloves, na hawachukui pre cautions wanapodeal na wateja, imagine yeye anaosha miguu ya machangudoa, mashangingi na aina mbalimbali za watu kwa kutumia kibeseni hichohicho, mikono hiyohiyo ambayo hata hatumii gloves, na vifaa hivyohivyo, halafu na wewe unaenda unaweka miguu yako hapo
Yupo hapa pembeni ananitazama kwa jicho la hubaWewe nimwanamke anaejielewa. Vipi shemeji hajambo
Basi kwa niaba ya wanajukwaa natoa pole za dhati kwakeIalivyo Waka hawakutegemea,mimi mwenyewe sikutegema Kama anahasira vile.Nili m bembeleza sanaaa wao wakawa washangaa naona waliogapa so tukaondoka Tena nikiwa namvuta mkono jaman alichukia sana
We nae uliharibu mchezoIalivyo Waka hawakutegemea,mimi mwenyewe sikutegema Kama anahasira vile.Nili m bembeleza sanaaa wao wakawa washangaa naona waliogapa so tukaondoka Tena nikiwa namvuta mkono jaman alichukia sana
Mhhh!!! Bila shaka ushashikwa matako wewe. Sasa dada, kama unajitembeza barabarani nusu uchi unataka nini? Kama sio tango? Skuzote jinsi unavojiweka ndo watu watakuchukulia hivohivo.Mtu unajipitia zako mara umeshikwa bega, au unavutwa nguo, mkono au kiuno, dada hii inakutosha au hii itakupendeza kwani huwezi kuniambia nikasikia tukaelewana bila kunigusa?
Machinga wa Karikaoo, Karume, Mbezi ya Kimara jumlisha na wale wapiga debe ndo kuzidi kabisa, Mwenge yaani wanakera sana, mbaya zaidi wanaona sawa tu na ukiwaambia usiniguse wanakudharirisha utasikia usishikwe we nani mtu mwenyewe mbaya, au hujapendeza.
Mfano, kuna siku nilikuwa na rafiki yangu Karume tunanunua bidhaa zetu machinga mmoja akamshika rafiki yangu kwa kuchomeka kidole ndani ya belti la sketi yake eti anamuonesha urembo yafiki yangu alikasirika mpaka leo hana hamu ya kwenda Karume.
Wao wanaona kawaida kumgusa, kumkumbatia, wengine kumbusu mwanamke asiye mjua wala kuwa na mazoea naye huko babarani na watu wakaona ni kawaida hata kama mwanamke huyo hataonekana kuridhishwa na kitendo hicho.
Machinga wanaouza bidhaa mitaani huwashika wanawake ikiwa kama njia ya wao kuwatangazia bidhaa zao kitu kama hicho si sahihi kwa kuwa wanaweza kuwatangazia bidhaa bila kugusa miili yao, wengine huenda mbali zaidi pale inapotokea mwanamke akaonesha kuwa hakupenda kuguswa huanza kumdhalilisha kwa kusema unaringa kitu gani na wakati wewe ni mbaya tu, usigushwe wewe nani kwani nk.
Barabarani, kwenye vyombo vya usafiri na popote anapopita mwanamke anaweza kuvutwa nguo huo ni udhalilishaji wa makusudi kwa kuwa hakuna hatua zinazochukuliwa kumnusuru na kero hii.
Mwanamke amekuwa mhanga katika jambo hilo hali inayomyima kuwa huru kutembea maeneo mengine kwa kuwa wanaume hawaoni kuwa wana mipaka na mwili wa mwanamke wao huona kuwa mwili wa mwanamke wanaweza kuugusa wakati wowote na hakuna sheria yoyote watakayoadhibiwa nayo.
Wengine huwashika hadi sehemu nyeti za mwili na hakuna yeyote wa kumtetea mwanamke anayepatwa na adha ya ukatili kama huu hali ambayo inamwathiri kisaikolojia na kumfanya akose kujiamini kutembea akiwa huru.
Ifike hatua jamii ielewe kuwa kumgusa au kumshika mtu bila ridhaa yake ni kumvunjia heshima kwani kila mtu hupenda kuwa huru na kufanya kitu ambacho yeye binafsi karidhia.
Pamoja na kuwa kuna sheria ya kutokumgusa mwanamke na matendo kama hayo ni kosa kisheria na adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka 5 jela au faini ya sh. 300,000 lakini ukimshika zaidi maeneo nyeti kama kifuani ni kifungo cha miaka 15 je, sheria hii ni butu mbona ndio kwanza matendo yanaongezeka?
Nani anaitekeleza au juhudi gani zinafanyika katika kuwawajibisha watendaji ili waache au kuwaelimisha wajue kuwa wanatenda kosa kumshika mwanamke bila ridhaa yake?
Jamii ijue kuwa Kumshika, kumbusu, kumkumbatia au kumgusa mwanamke bila ridhaa yake ni udhalilishaji. Inabidi upigiwe kelele.