Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lakini huu upuuzi wa kuruhusu machinga kila sehemu hadi wameziba barabara ufike mwisho kabisa. Nchi haiwezi kuendelea kwa upuuzi huo. Kilometre moja ya lami ni billion 2. Inatumika kuuza bidhaa za machinga. Watumie hata robo ya hela hiyo kuwajengea sehemu zao.Ikiwa bado tu hayati Magufuli hajazikwa, Machinga na wafanya biashara wadogo katika stend ya Magufulu kwa mabasi yaendayo mikoani teyari wameaanza kushikishwa adamu na mgambo wa jiji
Kiufupi hawatakiwi kufanya biashara zao ndani na nje ya stendi...namba inasomwa kweli kweli
Wapi huko mkuu, tukaamishe wapangaji wetu?Kuna maeneo naona bomoa bomoa imeanza ghafla.
Bar niliyokuwa nalinda ya Peace imebomolewa nimekua jobless.Wapi huko mkuu, tukaamishe wapangaji wetu?
Nilipita soko flani nikakuta wafanyabishara wengi wakiwa kinamama wamepanga nyanya, mbogamboga, ndizi nk chini, nilikuwa na jamaa yangu.Ni aibu kwa jinsi wanavyovamia kila mahala yaani kimsingi hakuna utaratibu kabisa ni zaidi ya manzese huo umataifa wa mbezi luis haupo tena ni kituko kabisa
Nilipita soko flani nikakuta wafanyabishara wengi wakiwa kinamama wamepanga nyanya, mbogamboga, ndizi nk chini, nilikuwa na jamaa yangu.
Nikamwambia jamaa niliyekuwa naye, "soon hawa wataondoka hapa wapende wasipende" kumbe mmojawapo wa wale wamama akasikia, akaanza kunirushia lugha mbaya.
Ikiwa bado tu hayati Magufuli hajazikwa, Machinga na wafanyabiashara wadogo katika stendi ya Magufulu kwa mabasi yaendayo mikoani tayari wameaanza kushikishwa adabu na mgambo wa jiji
Kiufupi hawatakiwi kufanya biashara zao ndani na nje ya stendi. Namba inasomwa kweli kweli
Sawa sawa bwana punyet Babel. Pale Kuna frem za Bei mbaya halafu unaruhusu machinga wafanye biashara zile zile. Unategemea Kuna atakayelipa Kodi?Mgambo wa jiji wameshika hatamu
Subiri kukuche mgambo tunakuja. Na safari hii tunayaifisha mzigo na chinga Keko.Machinga wamejaa Kama wote nipo stend hapa
Wengine wanakuja na bidhaa pick up nzima. Mmachinga gani huyo?Hiyo ni stand sio soko, yaani hii awamu ya washamba imeharibu wamachinga wanajiona wana haki hata kupanga bidhaa mbele ya ofisi yako...sasa waambie watoe uone moto wao
Umenena vema. Kuna haja ya kutenga maeneo rafiki kwa ajili yao. Nchi nyingine wamefanikiwa. Tunaweza piaWawekwwe complex yao pembeni wafanye biashara habari ya umechoka na safari unashindwa hata kukatiza vizuri na begi lako kisa msongamano sio poa. Mbona airport mambo shwari
Sasa hapa Chadema imeingiaje?Hapa chadema watashangilia sana kwamba wamemkomoa Magufuli, watoto wake wamelala njaa
La kuwaachia wamachinga wachafue miji JPM aliteleza kweliMagufuli alikua mjanja alijua akisema kila kitu cha wanyonge atawin na kweli aliwin. Kwa sababu hao ndio wapiga kura yani hawajali kukaa masaa 8 kusubiri foleni kumpigia mtu wao, na ndio hao wamejitokeza maelfu kumlilia na kukimbia kilometers kibao kwenye kumuaga. So alijua akiwa na hawa wasio jua ku-argue atatoboa.