Machinga waanza kumlilia Hayati Magufuli

Ni wapi machinga walimpiga mfanya biashara ngumi? Hapa ni kwamba serikali imekurupuka kuwahamisha pasipo kuwatengea maeneo maalamu ya kufanya biashara waanze kwanza kuwaandalia maeneo ya kufanya biashara kisha wawahamishe pasipo hii ya kuwahamisha pasipo kuwaandalia sehemu yao maalamu.

Tunachoiomba serikali ni kufanya maamuzi sahihi pasipo kuwaonea hawa vijana walioamua kujiajiri kupitia umachinhnga.
 
Mkuu kichwa chako kiko sawa ?
Wapi nimeandika machinga walimpiga mfanyabiashara ngumi?
 
Mkuu kichwa chako kiko sawa ?
Wapi nimeandika machinga walimpiga mfanyabiashara ngumi?
Serikali imesikia kilio chetu wananchi tulionyang'anywa kwa nguvu haki ya kutumia barabara na wamachinga.
Haki ya machinga ni kutumia barabara kutembea na si kumwaga chini takataka zake.
Mkae mkijua kabisa wananchi walio wengi hatukubaliani na uvamizi wa machinga usiojali sheria.
Wewe unajijali binafsi hujali wengine, uhuru wako usiingilie uhuru wa mwenzio, machinga pimeni mizani msitumie hoja ya nguvu bali nguvu ya hoja.
 
Naona dalili za sisiemu kupoteza uchaguzi ujao.
kama ushindi wa ccm unategemea kuwalinda watu wanavunja na taratibu ns kukera wengine basi usipatikane tu, ila kumbuka kuna sisi pia tunaokereka na wamachinga kivamia maeneo yasiyostahili tutakaoipigia kura ccm!!
 

Hivi unadhani hawajatengewa maeneo..? fwatilia vyombo vya habari kabla ya kukurupuka. Kwanza ilitakiwa washtakiwe kwa kuvunja sheria wapigwe na faini kabisa. Huwezi ukafanya biashara barabarani eti tukuite mnyonge
 
Machinga wenzangu tujitahidi kuwahi maeneo tuliyopangiwa na sirikali.
 
maeneo ya Mwanza naona tayari washapungua barabarani.... wengine wametelekeza meza zao
Hawa wa Mwanza nawafahamu vizuri sana. Nilikuwa mmoja wa watu waliowashauri waipigie kura CCM 2020 kwa Rais na Mbunge Mabula (tena huyu labda aanze kuaga kabisa kama suala la machinga litaendeshwa hivi). Hivyo, kwenye kampeni za 2025 usishangae wanatelekeza mikutano ya kampeni kama walivyotelekeza meza zao leo. Na sijui kama Mh. Mabula atakuwa na ubavj wa kuwashawishi tena nikifikiria kazi kubwa tuliyoifanya ya kumrudisha 2020.
 
Jpm alikua na file mirembe
 
Wanamlilia mtu aliyewaruhusu kuvunja sheria??? Tena kwa kufanya biashara hata kwenye barabara za mwendo kasi???
Kama aliwapenda kwann hajawaruhusu wakatandike biashara kwenye kuta za Ikulu???
 
Wanamlilia mtu aliyewaruhusu kuvunja sheria??? Tena kwa kufanya biashara hata kwenye barabara za mwendo kasi???
Kama aliwapenda kwann hajawaruhusu wakatandike biashara kwenye kuta za Ikulu???
Aliwalea sana yaani wafanyabiashara wanaolipa kodi, walionekana yatima nchi hii!!tena mimi nashauri wale watakaokaidi kuhama, hili zoezi lisimamiwe na MP kabisa!!!kwani wakitumia siasa hili zoezi litashindikana hasa kwa dar, kwani wao ndio wanajiona manunda sana!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…