Magufuli akumbukwe kwa mazuri yake na siyo kwa mapungufu yake.
Sijawahi kuwa shabiki wa Magufuli lakini kuna mambo mengi aliyoyafanya yalikuwa sahihi. Na hayo mazuri aliyoyafanya, wengi wetu hatujawahi kuyafanya na hatutayafanya.
Mimi binafsi, lililokuwa baya kabisa wakati wa utawala wake, ambalo kwa kweli lilikuwa ni doa kubwa ni matendo ya watu wasiojulikana ya kuua, kuteka na kupoteza watu.
Sina shaka hata kidogo juu ya marehemu kutamani sana nchi iwe na maendeleo japo kuna wakati zile mbinu za kufikia dhamira zake, zilikuwa na walakini. Kasoro nyingine kwenye utawla wake ni kukosekana demokrasia, kukosekana uhuru wa vyama vya siasa, kukosekana uhuru wa maoni, kukosekana uhuru wa vyombo vya habari, kukosekana kwa utawala wa kisheria, mbinu mbaya za ukusanyaji mapato ya serikali, kuua uwekezaji kutokana na harassment kwa wawekezaji bila ya sababu za msingi, n.k.
Nani atasema miundombinu siyo muhimu? Nani atasema ukarabati na ujenzi wa hospitali na zahati siyo muhimu? Nani atasema ukarabati wa viwanja vya ndege, haukuwa muhimu? Nani atasema udhibiti wa matumizi ya Serikali siyo jambo jema?
Samia aangalie mazuri ya marehemu, ayalinde na kuyaendeleza. Mapungufu ya marehemu yaachwe.