Macho yangu yananidanganya?

Hakuna kama Maghufuli hilo watu wakatae wakubali nguvu ya umma inajionyesha Jana tumejipanga kijazi pale lisaa lizima tunasubiri msafara na bado mioyoni mwetu tunahisi tuna deni kubwa hatukumuenzi ipasavyo.

Huu msiba utatutafuna mda mrefu sana haitapita siku hatujamfufua kimawazo.
 
Aliyekuwa mwandishi wa habari na makala, akiandikia gazeti la RAI, la wakati ule sio hili la sasa, Muhigo Ryehemamu (spelling) aliwahi kusema. Namnukuu.

Unaweza kukuta watu wajinga milioni mbili wanafanya jambo lao la kijinga, na Kwa kuwa ni wengi , unaweza kufikiri kuwa jambo wanalofanya ni la maana sana. (Ila mimi sijasema kwamba watu wote walioenda uwanja wa uhuru leo ni wajinga. Nilimnukuu mzee Muhigo) Kwa hiyo ndugu Nyani Ngabu wingi wa watu sio kwamba wooote walikuwa wanampenda. Wengine wameenda kushangaa tu. Wapo waliokuwa wana mpenda na pia waliokuwa wanamchukia.

Tuwaache watu waonyeshe hisia zao. Hii ngoma ipo 50/50
 
Hata wakimpeleka Tarime bado watu watajitokeza kumuaga rais wao.

Kwa sasa hii MAITI ndio kitu pekee cha kupotezeapo muda kwenye nchi yetu.. (Trend)
 
Mnatafuta kila aina ya vijisababu vya kutumia kama visingizio kujiaminisha kwamba alikuwa hapendwi na walala hoi na watu wa kada za kawaida.
 
Believe me mtu design hiyo ya kutwist the truth hata leo ingekuwa ni ya Hayati Nyerere angeponda tu if not favoring her status quo. Na maana her surname is known her word would be truth na ndo maana anajua anaaminika twitter.
 
Tunaachaje kumfufua kimawazo kwa chuki aliyofanikiwa kuijenga ndani ya taifa.?

Hakuna kama yeye huko kwa wauaji na mafisadi wenzie.
 
Kumkubali ni kukubali hajatesa, kuteka na kuua watu.

Tena wapuuzi Ndugai na genge lake walipanga wamuongeze muda wa kutawala.

Namchukia mara 1000 yako.
 
Aliminya democracy na waliomchukia ni wale waliokua wanamkosoa ila mengine alikua mtu poa.
Nakubaliana na wewe, kuna mambo mengi mzee alituumiza sana, hakuwa mwema kabisa. (He was ruthless)
Lakini kuna mambo amefanikiwa kulifanyia taifa kwa muda mfupi, unawaza mpaka unabaki mdomo wazi.
Tuseme ukweli tu, Raisi Magufuli alikuwa ni CHUMA HASWAAA.
 
negligence ni ya marehemu kwa kutochukua tahadhari juu ya korona. Sayansi haitaki ubishi, ukibishana nayo itakuumbua na ndicho kilichotokea
Daktari wa korona alifikiri kila kitu ni nyungu na madaraja.
 
Kwa nyomi hizi zinazojipanga barabarani mwili wa Rais Magufuli unapopitishwa ndo tuamini kweli alikuwa anachukiwa sana na watu walio wengi zaidi?
Nyomi za kubumba kwa kuhonga elfu tano tano. Halafu wanazimia kwasabb ya njaa na baadhi wamepewa hela wakafanye Futuhi ya kuzimia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…