Mindi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2008
- 3,523
- 4,992
Kwamba hakusafiri sana nje ya nchi haina maana kwamba hakuwa na impact kubwa katika jumuiya ya kimataifa. Siasa zake za pekee mara moja zilimtangaza. Misimamo yake ya pekee kuhusu covid pia ilimtangaza sana.Kifo cha Magufuli kilikuwa habari ya dunia.
Kwa mtu aliyekuwa hasafiri sana nje ya nchi, sikujua kama watu wa mataifa mengine walikuwa wanamfuatilia kiasi hicho.
Kifo chake kilikuwa headline news kwenye vyombo vikubwa vya habari vya kimataifa!
Kwamba msomi wa kiwango cha PhD, tena ya Chemistry, anadiriki kudisprove kipimo cha covid, kwa kutumia sample za mapapai na oil?
Kwamba anakejeli chanjo ambazo nchi za ulaya wametengeneza hasa kwa ajili ya raia zao, kwamba hazina utafiti wa kutosha, ambapo si kweli, halafu hapohapo anahimiza matumizi ya nyungu na madawa 'mbadala' ambayo hayajafanyiwa utafiti wa aina yoyote?
Rais ambaye anatangaza kuishinda covid, simply kwa kupiga marufuku utoaji takwimu za covid. Methali ya wazanaki ndio imemuumbua. Mfichaficha maradhi....
Kwa misimamo yake, analinganishwa na rais Trump wa USA na yule wa Brazil
Bila shaka Rais wa aina hiyo atakuwa maarufu saaana.
Bila shaka, atatangazwa sana ili kuonyesha kwa wengine wanaofikiria kufuata nyayo zake, mwisho wa kudharau na kuipuuza sayansi