Macho yangu yananidanganya?

Shangaa na wewe mkuu
 
Mm nimekuthibitishia kwamba alikuwa anapendwa, ss na ww thibitisha kwamba alikuwa hapendwi, mana mpk ss hujathibitisha zaidi ya kuongea chuki ulizonazo wewe binafsi dhidi yake.
 
Kuna aina ya Binadamu ni viumbe wa Rajabu sana,
 
Mm nimekuthibitishia kwamba alikuwa anapendwa, ss na ww thibitisha kwamba alikuwa hapendwi, mana mpk ss hujathibitisha zaidi ya kuongea chuki ulizonazo wewe binafsi dhidi yake.
Nilichokisema mimi ni kwamba wanaompenda sio wote na wanaomchukia sio wote. Shida iliyopo wewe umechukulia lile nyomi la watu kisha ukaamisha kundi la majority kuwa wanampenda
 
Cheki masela hawa wa bodaboda...

Huyu ndo mtu aliyekuwa anachukiwa kiasi hicho?

Am I losing my mind or something?

Punguza hisia. hawa ndio watanzania. Upepo kwao ni kitu muhimu sana. Mfano mdogo tu wakisikia mlio kama wa risasi hujongea eneo la tukio. Huwa tunapenda kuona. kifupi ni kweli pia kuwa Hayati alifanya makubwa. Alijenga lakini pia aliumiza. Amekiri mwenyewe akifa akumbukwe kwa mazuri. Alijua ana mabaya pia.
 
mkusanyiko mdogo huwakilisha jamii ndogo ya watu waloguswa/ama kufuatilia jambo fulani bt mkusanyiko mkubwa huwakilisha jamii kubwa ya watu hivo usipoteshe, majumbani tv zipo busy, mitandao ipo busy, yote hii inadhihirisha jamii kubwa imeguswa.

tukio la kuaga kitaifa limefuatiliwa na watu 3.9B duniani bt msivyo na aibu bado mnakaza mafuvu ya vichwa kuupinga ukweli.
 
Nilichokisema mimi ni kwamba wanaompenda sio wote na wanaomchukia sio wote. Shida iliyopo wewe umechukulia lile nyomi la watu kisha ukaamisha kundi la majority kuwa wanampenda
Ndiyo majority walimpenda kwn we unaonaje? Na ndiyo waliompigia kura nyingi mpk akawa Rais, Kama una uthibitisho kwamba majority hawakumpenda weka hapa.
 
Yeye hakuwa malaika mpk asiwe na mabaya. Ila tupime kati ya mazuri na mabaya yapi ni mengi.
 
Nyomi kubwa sana nimejaribu ku zoom hapo sijaona aliyevaa barakoa zaidi ya tozi kushoto aliyejifunga leso

Hii tu inatosha kupima IQ za waombolezaji na kujua ni watu wa namna gani walioudhuria
Mkuu,siku ujinga ukiisha kwa Watanzania wote,hakika hapo ndio utakuwa mwisho wa CCM kuongoza.
 
Ndiyo majority walimpenda kwn we unaonaje? Na ndiyo waliompigia kura nyingi mpk akawa Rais, Kama una uthibitisho kwamba majority hawakumpenda weka hapa.
Mimi sina uthibitisho hivyo sijui majority lipo kundi gani ila nachojua ni kwamba hakupendwa na kila mtu. Wewe uliyekiri kuwa majority wapo katika kundi la kumpenda ndio unipe uthibitisho nje ya matokeo ya uchaguzi. Kwasababu tume inayoratibu mchakato mzima wa uchaguzi inateuliwa na huyo huyo raisi anayeomba kura.
Kama kigezo chako ni kumiminika kwa watu kwenye kumuaga ndio uthibitisho basi uje na figure kamili kuwa Dar es salaam, ama Dodoma, ama Zanzibar wamejitokeza watu kadhaa kati ya watu kadhaa kwenye kuaga ni sawasawa na asilimia kadhaa.
Katika watu hao kadhaa waliojitokeza nimeona ndani ya mioyo yao wamehuzunika na msiba, na watu kadhaa nimeona mioyo yao ni wanafiki wanafanya maigizo ya kulia wakati moyo yao inafurahia ama ipo kawaida. Tupe uthibitisho wa takwimu
 
Yeye hakuwa malaika mpk asiwe na mabaya. Ila tupime kati ya mazuri na mabaya yapi ni mengi.
Mkuu nadhani hapo ndipo patakuwa pazuri sana.
Embu tutajie mema yake tuyajue kisha yalinganishwe na mabaya halafu ifanyike tathmini. Ni mema yapi aliyoyafanya?
 
Kuna mashinikizo yametolewa vyombo vya habari (tv na radio stations) zisipige nyimbo wala vipindi vyovyote vya kiburudani zaidi ya nyimbo za maombolezo tu sasa hapo mlaji ambaye ndio mtazamaji na msikilizaji atakuwa na uhuru gani wa kuchagua cha kuangalia na kusikiliza!. Sasa unategemea wangekengeuka? Huku malinyi kuna jamaa zangubwalikuwa wanafanya kazi saiti wamesimamishwa wasifanye kazi mpaka ipite wiki moja. Wakifanya kazi wataonekana msiba hauwahusu hivyo kitakachowakuta shauri yao.

Halafu mtu anaweza kuguswa na msiba japokuwa hakuwa akimpenda ama kumkubali marehemu
 
Mkuu nadhani hapo ndipo patakuwa pazuri sana.
Embu tutajie mema yake tuyajue kisha yalinganishwe na mabaya halafu ifanyike tathmini. Ni mema yapi aliyoyafanya?
Sipo hapa ku argue kitoto toto mm co mtoto mwenzio.
 
Nani kasema alipendwa na kila mtu? Unaongelea kuhusu tume jibu lake ni fupi tu km huiamini usiende kupiga kura au unda yako uyakayoiamini, nmalizie kwa kusema tuweni watu wa kukubali ukweli japo unauma.
 
Unasema neno majority tayari maanake unayo figure. Yaani kama mzani unakuwa umezidi upande mmoja. Sasa unatoa jibu kuwa majority wanampenda halafu hauna figure halisi ya idadi ya hao majority basi wewe unaitwa muongo
 
Unaelewa maana ya neno majolity? Majolity maana yake ni wengi, alafu kwnn nijisumbue kupoteza muda kwa kitu kilicho wazi? Naishia hapa ila ugueni pole, dunia imeona na kila mtu ni shahidi wa moyoni mwake, kwaheri.
 
Hilo haina faida kwasababu hawezi kufufuka, atazikwa na kisha atasauliwa. Inawezekana Mungu amesikia kilio na manung'uniko ya watu juu ya kauli zake za kejeli, juu ya aina ya uongozi wake wa ubabe asiotaka watu kuwa huru wa kutoa maoni, kushauri na kufungia vyombo vya habari wanaotoa habari asizotaka zitaka yeye kuzisikia masikio mwake, watu ambao familia zao zilikumbwa na kukosa ajira tokea wamalizie vyuo wanaambiwa wajiajili nawakati mitaji hawana.

Wanafunzi wengi wa vyuo wameishia kubaki mitaani na wengine wamekuwa wauzaji wa matunda kariakoo.
Watu waliokumbwa na bomoa bomoa kule kimara bila kulipwa chochote halafu wanasikia kauli kuwa Mwanza hatofanyiwa hivyo kwasababu ni wapiga kula wake. Eeh ndio niwapiga kula wake.
Waajiriwa wa serikalini wamekuwa na kilio tokea anaaingia madarakani hakuna kupandishwa daraja wala mshshara. Waliomba hilo mpaka basi lakini kwenye kilele cha Mei mosi wanaishia kupewa majibu ya kejeli.

Katika awamu ambayo muhimili wa bunge umeonekana hauna kazi basi ni awamu hii. Raisi amekuwa akifanya manunuzi bila ushirikishwaji, amefanya miradi na kuingia mikataba bila ya ushirikishwaji hivyo amekuwa mtu aliyekuwa na usiri mwingi katika mambo yaliyofanyika kama ni upigaji wa kodi ya wananchi basi umepugwa hasa.

Wafanyabiashara wakubwa wamekumbana na ongezeko la Kodi na imepelekea baadhi ya biashara kufungwa na baadhi makampuni yalipunguza idadi ya watu hivyo kuongeza idadi ya wakosa kazi mitaani.
Wakulima wa korosho waliipata vizuri
Miradi ya maendeleo huko vijijini ikawa sio wajibu wa serikali tena bali ikawa ni wajibu wa wananchu, watu wanalazimishwa kuchangia ela ili ijengwe shule, madarasa na mazahanati kamahauna ela unaweka ndani.
Tumeona uchatolization, kapeleka miradi mingi mikubwa mkoani kwake chato tena kwa kipindi kifupi tu.
Ukiachana na wamachinga, boda boda na mama ntilie, makundi mengi yaliyobakia yameisoma namba ipasavyo.

Kama unaona ufahali kuzungushwa ndio kupendwa na wengi, basi hao wachache hata wakiwa kumi tu Tanzania nzima watakuwa ni washindi kwa hilo kwasababu hata wakijaa watu Africa nzima hakuwezi kumfanya arudi. Mungu ni wa wote hakuna anayemzidi nguvu na uwezo na hakika wote kwake tutarejea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…