Benjamini Netanyahu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2014
- 95,871
- 116,627
Kwahiyo sasahivi tuna mashindano ya kupendwa na kuchukiwa?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shangaa na wewe mkuuKwa nini wanaompenda Magufuli wanalazimisha wasiompenda waonekane wachache na wao ni wengi? Kigezo chao ni umati uliojitokeza kumuaga. Mbona hizo ni hesabu za kitoto tu kupata majawabu? Dar kwa mfano, ina wakazi milioni 5 na ushee. Hivi waliojitokeza Uwanja wa Uhuru na wale waliosimama barabarani wanafika hata milioni moja? Na je wote hao waliofika, wote wanampenda? Wengi walibakia majumbani, hivyo hivyo kwa Dodoma, Zanzibar na Mwanza.
Mm nimekuthibitishia kwamba alikuwa anapendwa, ss na ww thibitisha kwamba alikuwa hapendwi, mana mpk ss hujathibitisha zaidi ya kuongea chuki ulizonazo wewe binafsi dhidi yake.Waliopo mtandao wanaishi dunia tofauti na ya mtaani? Tanzania ina waajiriwa wangapi wa serikalini? Je waajiriwa wote walirizika na aina ya utawala wake? Ndio mana nilikwambia uwezo wako mdogo naongea na mtu mwenye mlengo wa kisiasa ya uccm na uchadema. Mimi sijaingia huko kwenye sababu zako za kisiasa sijui Ben Sanane n.k. nataka twende makundi yasiyo kwenye mlengo wa uchama hapa utawakuta waajiriwa serikali, wanafunzi wa vyuo, wakulima, wafanya biashara wakubwa na wadogo, sekta binafsi. Hawa ni makundi yanaguswa moja kwa moja ukiachana na itikadi za kichama.
Halafu nimekwambia hoja ya pili ya namba. Kwenye namba ndipo itahitimisha hili. Kama kigezo cha kuonesha kupendwa kwake ni lile nyomi basi tuambie lile nyomi ni makadirio ya watu wangapi? Na je hilo nyomi limefikia idadi hata ya nusu ya wakazi wa Dar es salaam?
Mimi si kipofu wala si kiziwi.
Uwezo wangu wa kuona na kusikia upo juu.
Hivi hiki ninachokiona kwa macho yangu na kukisikia kwa masikio yangu ni uongo?
Nina maruerue labda? Hayo ninayoyaona ni mazingaombwe?
Kwa nyomi hizi zinazojipanga barabarani mwili wa Rais Magufuli unapopitishwa ndo tuamini kweli alikuwa anachukiwa sana na watu walio wengi zaidi?
Nahisi kuna watu wanakabwa na mafundo kooni wakiziona nyomi zimejipanga mabarabarani jijini Dar [na bado huko kwingine] zikimpa heshima za mwisho mwana udongo huyo. Hawa watu si aiabu wangependa kuona watu wachache wanaojitokeza kumuaga. La hasha.
Huwezi kupendwa na wote. Lakini pia, Rais hakuwa anachukiwa na idadi kubwa zaidi ya watu.
Licha ya mapungufu yake mengi, watu wengi walikuwa wanamkubali, hata kama si waziwazi. Na haitochukua muda watu wataanza kum miss.
Hii ni Manzese leo wakati akielekea uwanja wa Uhuru. Huyu ndo mtu anayechukiwa na watu?
Hapa ni Mwenge jana jioni mwili ukirudishwa spitali ya Lugalo. Huyu ndo mtu aliyekuwa anachukiwa? FOH.
Hapa ni jana jioni kwenye daraja la Kijazi.
Kote huko anapita. Hakuna vurugu. Watu wanamuaga kwa heshima kabisa.
Yawezekana wapo wachache wanaomtukana au kufurahia au vyovyote vile wajisikiavyo, lakini kwa hiki ninachokiona kwa macho yangu na kukisikia kwa masikio yangu, bado sijashawishika kwamba Rais Magufuli alikuwa anachukiwa na watu walio wengi.
Nilichokisema mimi ni kwamba wanaompenda sio wote na wanaomchukia sio wote. Shida iliyopo wewe umechukulia lile nyomi la watu kisha ukaamisha kundi la majority kuwa wanampendaMm nimekuthibitishia kwamba alikuwa anapendwa, ss na ww thibitisha kwamba alikuwa hapendwi, mana mpk ss hujathibitisha zaidi ya kuongea chuki ulizonazo wewe binafsi dhidi yake.
Cheki masela hawa wa bodaboda...
Huyu ndo mtu aliyekuwa anachukiwa kiasi hicho?
Am I losing my mind or something?
mkusanyiko mdogo huwakilisha jamii ndogo ya watu waloguswa/ama kufuatilia jambo fulani bt mkusanyiko mkubwa huwakilisha jamii kubwa ya watu hivo usipoteshe, majumbani tv zipo busy, mitandao ipo busy, yote hii inadhihirisha jamii kubwa imeguswa.Kwa nini wanaompenda Magufuli wanalazimisha wasiompenda waonekane wachache na wao ni wengi? Kigezo chao ni umati uliojitokeza kumuaga. Mbona hizo ni hesabu za kitoto tu kupata majawabu? Dar kwa mfano, ina wakazi milioni 5 na ushee. Hivi waliojitokeza Uwanja wa Uhuru na wale waliosimama barabarani wanafika hata milioni moja? Na je wote hao waliofika, wote wanampenda? Wengi walibakia majumbani, hivyo hivyo kwa Dodoma, Zanzibar na Mwanza.
Ndiyo majority walimpenda kwn we unaonaje? Na ndiyo waliompigia kura nyingi mpk akawa Rais, Kama una uthibitisho kwamba majority hawakumpenda weka hapa.Nilichokisema mimi ni kwamba wanaompenda sio wote na wanaomchukia sio wote. Shida iliyopo wewe umechukulia lile nyomi la watu kisha ukaamisha kundi la majority kuwa wanampenda
Yeye hakuwa malaika mpk asiwe na mabaya. Ila tupime kati ya mazuri na mabaya yapi ni mengi.Punguza hisia. hawa ndio watanzania. Upepo kwao ni kitu muhimu sana. Mfano mdogo tu wakisikia mlio kama wa risasi hujongea eneo la tukio. Huwa tunapenda kuona. kifupi ni kweli pia kuwa Hayati alifanya makubwa. Alijenga lakini pia aliumiza. Amekiri mwenyewe akifa akumbukwe kwa mazuri. Alijua ana mabaya pia.
Mkuu,siku ujinga ukiisha kwa Watanzania wote,hakika hapo ndio utakuwa mwisho wa CCM kuongoza.Nyomi kubwa sana nimejaribu ku zoom hapo sijaona aliyevaa barakoa zaidi ya tozi kushoto aliyejifunga leso
Hii tu inatosha kupima IQ za waombolezaji na kujua ni watu wa namna gani walioudhuria
Mimi sina uthibitisho hivyo sijui majority lipo kundi gani ila nachojua ni kwamba hakupendwa na kila mtu. Wewe uliyekiri kuwa majority wapo katika kundi la kumpenda ndio unipe uthibitisho nje ya matokeo ya uchaguzi. Kwasababu tume inayoratibu mchakato mzima wa uchaguzi inateuliwa na huyo huyo raisi anayeomba kura.Ndiyo majority walimpenda kwn we unaonaje? Na ndiyo waliompigia kura nyingi mpk akawa Rais, Kama una uthibitisho kwamba majority hawakumpenda weka hapa.
Mkuu nadhani hapo ndipo patakuwa pazuri sana.Yeye hakuwa malaika mpk asiwe na mabaya. Ila tupime kati ya mazuri na mabaya yapi ni mengi.
mkusanyiko mdogo huwakilisha jamii ndogo ya watu waloguswa/ama kufuatilia jambo fulani bt mkusanyiko mkubwa huwakilisha jamii kubwa ya watu hivo usipoteshe, majumbani tv zipo busy, mitandao ipo busy, yote hii inadhihirisha jamii kubwa imeguswa.
tukio la kuaga kitaifa limefuatiliwa na watu 3.9B duniani bt msivyo na aibu bado mnakaza mafuvu ya vichwa kuupinga ukweli.
Sipo hapa ku argue kitoto toto mm co mtoto mwenzio.Mkuu nadhani hapo ndipo patakuwa pazuri sana.
Embu tutajie mema yake tuyajue kisha yalinganishwe na mabaya halafu ifanyike tathmini. Ni mema yapi aliyoyafanya?
Aliyetoa hoja ya kupima mabaya na mazuri si ni wewe mwenyewe? Sasa hoja hiyo hiyo iendelezwe unaikimbia tenaSipo hapa ku argue kitoto toto mm co mtoto mwenzio.
Nani kasema alipendwa na kila mtu? Unaongelea kuhusu tume jibu lake ni fupi tu km huiamini usiende kupiga kura au unda yako uyakayoiamini, nmalizie kwa kusema tuweni watu wa kukubali ukweli japo unauma.Mimi sina uthibitisho hivyo sijui majority lipo kundi gani ila nachojua ni kwamba hakupendwa na kila mtu. Wewe uliyekiri kuwa majority wapo katika kundi la kumpenda ndio unipe uthibitisho nje ya matokeo ya uchaguzi. Kwasababu tume inayoratibu mchakato mzima wa uchaguzi inateuliwa na huyo huyo raisi anayeomba kura.
Kama kigezo chako ni kumiminika kwa watu kwenye kumuaga ndio uthibitisho basi uje na figure kamili kuwa Dar es salaam, ama Dodoma, ama Zanzibar wamejitokeza watu kadhaa kati ya watu kadhaa kwenye kuaga ni sawasawa na asilimia kadhaa.
Katika watu hao kadhaa waliojitokeza nimeona ndani ya mioyo yao wamehuzunika na msiba, na watu kadhaa nimeona mioyo yao ni wanafiki wanafanya maigizo ya kulia wakati moyo yao inafurahia ama ipo kawaida. Tupe uthibitisho wa takwimu
Unasema neno majority tayari maanake unayo figure. Yaani kama mzani unakuwa umezidi upande mmoja. Sasa unatoa jibu kuwa majority wanampenda halafu hauna figure halisi ya idadi ya hao majority basi wewe unaitwa muongoNani kasema alipendwa na kila mtu? Unaongelea kuhusu tume jibu lake ni fupi tu km huiamini usiende kupiga kura au unda yako uyakayoiamini, nmalizie kwa kusema tuweni watu wa kukubali ukweli japo unauma.
Unaelewa maana ya neno majolity? Majolity maana yake ni wengi, alafu kwnn nijisumbue kupoteza muda kwa kitu kilicho wazi? Naishia hapa ila ugueni pole, dunia imeona na kila mtu ni shahidi wa moyoni mwake, kwaheri.Unasema neno majority tayari maanake unayo figure. Yaani kama mzani unakuwa umezidi upande mmoja. Sasa unatoa jibu kuwa majority wanampenda halafu hauna figure halisi ya idadi ya hao majority basi wewe unaitwa muongo
Hilo haina faida kwasababu hawezi kufufuka, atazikwa na kisha atasauliwa. Inawezekana Mungu amesikia kilio na manung'uniko ya watu juu ya kauli zake za kejeli, juu ya aina ya uongozi wake wa ubabe asiotaka watu kuwa huru wa kutoa maoni, kushauri na kufungia vyombo vya habari wanaotoa habari asizotaka zitaka yeye kuzisikia masikio mwake, watu ambao familia zao zilikumbwa na kukosa ajira tokea wamalizie vyuo wanaambiwa wajiajili nawakati mitaji hawana.Unaelewa maana ya neno majolity? Majolity maana yake ni wengi, alafu kwnn nijisumbue kupoteza muda kwa kitu kilicho wazi? Naishia hapa ila ugueni pole, dunia imeona na kila mtu ni shahidi wa moyoni mwake, kwaheri.