Macho hayajadanganya.Ni kweli JPM alikuwa anapendwa hata tangu akiwa Waziri kwani alikuwa mtu wa matokeo hasa yanayoonekana.Kukariri kwake takwimu kulimfanya hata akiwa waziri wa ujenzi bajeti yake kupitwa bila mikwara yoyote.
Na ndio maana wengi tunabaki kujiuliza kwa kupendwa kule na huku kwa leo tunakokuona palikuwa na haja gani ya ,
- Kunyima uhuru wa vyama vingine vya siasa?
- Kuvuruga uchaguzi wa serikali za mitaa
- Kuvuruga uchaguzi mkuu?
Jambo moja ni wazi na limepata uthibitisho katika kipindi hiki ni kuwa "Watanzania ni wanafiki wa kupindukia"Sorry to say that!!!