Macho yangu yananidanganya?

Macho yangu yananidanganya?

Mkuu hili nililiona Live hapa Chang’ombe ,
Tukubali tu Tanzania kuna Dunia mbili Dunia ya mitandaoni na Dunia halisi nje ya mitandao
Ukisoma tu mitandao unaweza sema jamaa alikua anachukiwa sanaa
Ila ukirudi mitaani ambao ndio kwa wapiga kura halisi ni tofauti sana ,the guy is loved aisee

Wapinzani wana lakujifunza hapa ,
Watanzania wameongea kwa vitendo.
 
Kwa ware ambao maisha yao hayakiguswa ambao ni wanachi wengi wa kawaida, walimpenda sana, lkn watumishi wa serikali, wafanyabiashara, na wLe waliotendwa ktk utawala weke wakiwemo wanasiasa hawakumkubali. Binafsi mimepima kwenye mikusanyiko, hali ni tofauti. Kon zipo nyingiwmno
Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, mkoa wa Dar es salaam inawakazi 4,364,541. Embu tuambizane watu waliojitekeza katika zoezi la kuaga wanafika takribani watu wangapi? Hawezi kuchukiwa na watu wote na pia hawezi kupendwa na watu wote. Ila kama lengo ni kulinganisha mapenzi kisa tu kufuata idadi ya walijitokeza basi malizieni takwimu kwa kupata idadi ya wasiyojitokeza ili ijulikane wengi ni wapi.
 
Mkuu hili nililiona Live hapa Chang’ombe ,
Tukubali tu Tanzania kuna Dunia mbili Dunia ya mitandaoni na Dunia halisi nje ya mitandao
Ukisoma tu mitandao unaweza sema jamaa alikua anachukiwa sanaa
Ila ukirudi mitaani ambao ndio kwa wapiga kura halisi ni tofauti sana ,the guy is loved aisee

Wapinzani wana lakujifunza hapa ,
Huwezi jua moyoni kwa mtu kupoje hata kama kaonesha kitendo au kauli fulani mbele ya camera. Wapo wenye uzuni moyoni na wapo walijitokeza kwa furaha nafsi mwao. Lakini msisahau jinsi watanzania walivyo wapenda ushabiki na umbeya. Ikitokea ajali tu mahali basi kila mtu ataacha kazi yake alikuwa anafanya ili mradi akashangae apate cha kusimulia.
Kule morogoro ajali ya moto iliiyotokea kumetokea mkusanyiko mkubwa wa watu kutokana tu na tabia ya watanzania kupenda kushadadia mambo.
 
Watanzania huweka pembeni tofauti zao kwenye msiba. Usidhani majority ya Watanzania wataleta siasa kwenye msiba eti kwa kuwa huyu simkubali kisiasa basi ntasusia msiba wake!. Watanzania hawako hivyo!
 
Huwezi jua moyoni kwa mtu kupoje hata kama kaonesha kitendo au kauli fulani mbele ya camera. Wapo wenye uzuni moyoni na wapo walijitokeza kwa furaha nafsi mwao. Lakini msisahau jinsi watanzania walivyo wapenda ushabiki na umbeya. Ikitokea ajali tu mahali basi kila mtu ataacha kazi yake alikuwa anafanya ili mradi akashangae apate cha kusimulia.
Kule morogoro ajali ya moto iliiyotokea kumetokea mkusanyiko mkubwa wa watu kutokana tu na tabia ya watanzania kupenda kushadadia mambo.
Sasa nyie mnatupa uthibitisho gn kwamba alichukiwa, hebu panga hoja yako ili tupate kuelewa kwamba alichukiwa Mana wewe hii ya watu kujaa kupita kiasi, watu kuzimia, kutandindika nguo na matawi ya miti huitaki ss tuambie wewe unatushawishi vp tupate kuamini kwamba alichukiwa?
 
Ni ajabu sana kudhani Sitting president akifa atakosa watu wa kumlilia!. It will never happen hata awe mbovu kiasi gani!.
 
Kifo cha Magufuli kilikuwa habari ya dunia.

Kwa mtu aliyekuwa hasafiri sana nje ya nchi, sikujua kama watu wa mataifa mengine walikuwa wanamfuatilia kiasi hicho.

Kifo chake kilikuwa headline news kwenye vyombo vikubwa vya habari vya kimataifa!
Corona haikuachwa kutajwa. Ni aibu!
 
Hiki kifo kimeniuma sana!! Kwa kuwa mimi kama polisi wa kisiasa huwa napenda nipate jukwaa la kusahihisha panapokosewa,huku nikifurahia ninayofanikishiwa kimya kimya,kama tu police force,polisi haji kukusifu unapojenga nyumba ya familia yako,hakusifii ukiwaletea watoto wako msosi safi,wala haji kukushukuru kwa kulipa kodi inayowalipa wao mishahara,wewe fanya mema yote wao kimya,ila siku ukimpiga mkeo unayemlisha na kumvisha na malalamiko yakawafikia basi wanakuweka kati,nilipenda magufuli aendelee kuishi sana!! Huku tukimpinga kwa baadhi ya mambo na kumkejeli wakati mwingine anapokosea,ila nilipenda amalize muda wake ili Nimsifu kwa mengi mazuri aliyoyafanya,na nimsute kwa machache aliyokosea,kama tu kikwete alivyosemwa akiwa madarakani na kuhusudiwa alipomaliza muda wake,angalia leo wale waliokesha mitandaoni kumponda kikwete ndiyo wa kwanza kumsifia alipotoka, Nita mmiss magufuli kwa sababu milioni,he was the man,regardless
 
Sasa nyie mnatupa uthibitisho gn kwamba alichukiwa, hebu panga hoja yako ili tupate kuelewa kwamba alichukiwa Mana wewe hii ya watu kujaa kupita kiasi, watu kuzimia, kutandindika nguo na matawi ya miti huitaki ss tuambie wewe unatushawishi vp tupate kuamini kwamba alichukiwa?
Uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana, haya twende unavyotaka wewe basi haya tufanye nyomi ile yote waliojitokeza wamejitokeza kwa mapenzi yao kwa Magufuli. Je hilo nyomi ni makisio ya watu wangapi ndani ya mkoa mzima? Wasioenda wanafikia asilimia ngapi? Unashindwa kufikiria kuwa hawezi kuchukiwa na kila mtu wapo watakaompenda lakini idadi zinaweza kupishana ama kulingalina. Au ulitegemea uone hakuna watu kabisa ndio utaona hapendwi? Kila kitu ni namba mkuu au unataka kuniambia idadi iliyojitojeza uwanja wa uhuru inafika nusu ya wakazi wote wa Dar es salaam?
Kuhusu kutandika nguo na matawi je hapo umeziona nafsi zao ndani zikionesha kama ni ishara ya majonzi? maana hujui nafsi ya mtu kama anayatenda hayo kwa furaha ya bora kaondoka ama ni huzuni wa kwanini kaondoka. Kwani watu wanafiki wa kwenye misiba hukuwahi kuwaona katika maisha yako? Wanaojiliza ili mradi anaonekane mbele za watu kuwa nae imemgusa hujapata kuwashuhudia?

Tukija kwenye kuzimia, kuna waliozimia kwa kukosa hewa kutokana na msongamano wa watu, na wapo wengine wamezimia kwa kuona sura ya maiti ya Magufuli (mstuko/butwaa) na hilo hasa hasa kwa wanawake ndilo limetokea kesi nyingi za kuziamia. Haya embu niambie baada ya Dodoma kubadilisha utaratibu tofauti na ilivyokuwa Dar es salaam, je ulishuhudia watu wangapi waliozimia?
Kuzimia kwenye msiba ndio umeshuhudia kwenye msiba huu? Msiba wa Kanumba ulikuwa haujazaliwa?
 
Hebu wacheni kujiongopea msije mkafa kwa sonono, sisi tunaishi huku mtaani nyinyi mnaishi mitandaoni, jamaa alikuwa anapendwa kabla hajafa, msitake kulazimisha kitu kisichokuwepo, watu wameumia sn na ndiyo ukweli mtake msitake na wameonesha kwa vitendo.

Ni kweli huwezi kupendwa na wote cz hata mitume hawakuwahi kupendwa na wote na ndiyo maana wachache walikuwa hawampendi km wewe, ukiwauliza sababu watakuambia Ben saa8, Azory Gwanda, but tukiwaomba uthibitisho hamna, pia mtasema uhuru wa habari wakati mnakesha humu, twitter na facebook mkitukana bila shida yoyote.

Au mkienda mbali mtasikika mkisema mlihitaji maendeleo ya watu sio ya vitu lkn tukiwaambie mtueleze maendeleo ya watu yanakujaje bila vitu majibu hamtupi. Ss kwa tunaoelewa haya mambo ni kwamba tunawaacha tu kwn huwezi kupendwa na wote lkn pia muda utaongea but msitake kulazimisha kwamba hakupendwa na wengi wkt mambo yapo hadharani.

Kuendelea kubishia ukweli ni kujiumiza tu.
 
Jamaa alikuwa anapendwa tuwe wakweli Tu kama watu wanapita mpka kwenye njia zisizo halali pale taifa ili kumuaga Tu Mheshimiwa basi wanaosema alikuwa anachukiwa Wana lao Jambo japo ni kweli huwezi pendwa na kila mtu

Kuna kitu niliwahi kujiuliza siku moja. Kuna jamaa mmoja alikuwa mtaani anajulikana kama jambazi. Kuna siku wakaenda kuiba sehemu wakavamiwa na polisi na yeye kuuawa. Watu walijaa sana kwanza pale maiti ilipokuwa kabla ya kuondolewa, na mwisho msibani mpaka mazikoni. Nilichojiuliza ni kuwa, kama huyu ni jambazi na aliogopwa na kila mtu kwanini watu wengi walijaa na kwenda kumzika?
 
Kwa nini wanaompenda Magufuli wanalazimisha wasiompenda waonekane wachache na wao ni wengi? Kigezo chao ni umati uliojitokeza kumuaga. Mbona hizo ni hesabu za kitoto tu kupata majawabu? Dar kwa mfano, ina wakazi milioni 5 na ushee. Hivi waliojitokeza Uwanja wa Uhuru na wale waliosimama barabarani wanafika hata milioni moja? Na je wote hao waliofika, wote wanampenda? Wengi walibakia majumbani, hivyo hivyo kwa Dodoma, Zanzibar na Mwanza.
 
Waliopo mtandao wanaishi dunia tofauti na ya mtaani? Tanzania ina waajiriwa wangapi wa serikalini? Je waajiriwa wote walirizika na aina ya utawala wake? Ndio mana nilikwambia uwezo wako mdogo naongea na mtu mwenye mlengo wa kisiasa ya uccm na uchadema. Mimi sijaingia huko kwenye sababu zako za kisiasa sijui Ben Sanane n.k. nataka twende makundi yasiyo kwenye mlengo wa uchama hapa utawakuta waajiriwa serikali, wanafunzi wa vyuo, wakulima, wafanya biashara wakubwa na wadogo, sekta binafsi. Hawa ni makundi yanaguswa moja kwa moja ukiachana na itikadi za kichama.
Halafu nimekwambia hoja ya pili ya namba. Kwenye namba ndipo itahitimisha hili. Kama kigezo cha kuonesha kupendwa kwake ni lile nyomi basi tuambie lile nyomi ni makadirio ya watu wangapi? Na je hilo nyomi limefikia idadi hata ya nusu ya wakazi wa Dar es salaam?
 
Back
Top Bottom