Machozi ya mtoto wa jirani yangu yamenisikitisha sana

Machozi ya mtoto wa jirani yangu yamenisikitisha sana

Sipendi watoto wa watu waje nyumbani kwangu hata kuangalia TV Nimejenga nyumba kubwa sana huwa wanasem hawa wachaga wana misukuke. Mtoto akiumw tu wanaleta maneno Kifup sitak waje wakae huko kwao🙃
Sawa kabisa kila mtu ana namna yake ya kuishi kwangu mimi nilikua nimepanga na niliruhusu wawe sehemu ya furaha yangu now naishi kwangu na bado nikiwa na hata sherehe ya mwanangu lazima niwaalike watoto wa mtaani kwangu waje wale wafurahi na wenzao. Kwahiyo sipingi kabisa mfumo wako wa maisha maana unajiepushia mambo mabaya kwa mtazamo wako ila kwangu mimi sijawahi kutana na baya lolote kwa kuwaruhusu watoto kuwa karibu yangu.
 
Sawa kabisa kila mtu ana namna yake ya kuishi kwangu mimi nilikua nimepanga na niliruhusu wawe sehemu ya furaha yangu now naishi kwangu na bado nikiwa na hata sherehe ya mwanangu lazima niwaalike watoto wa mtaani kwangu waje wale wafurahi na wenzao. Kwahiyo sipingi kabisa mfumo wako wa maisha maana unajiepushia mambo mabaya kwa mtazamo wako ila kwangu mimi sijawahi kutana na baya lolote kwa kuwaruhusu watoto kuwa karibu yangu.
Jambo la kumshukuru Mungu👍Hata Yesu alisema waacheni watoto wadogo waje kwangu. Hata mimi napenda watoto na ningependa waje ila hapana Hata sikukuu huwa nawanunulia soda majiran na watoto zao kiroho safi. .
 
Oh masikini O 😭
C72CF180-ECF7-4203-BA61-91123950F312.jpeg
 
Sawa umetoa 30k 0 apate zawadi ya pasaka, ila nakuhimiza fanya hivo hivo kwa wazazi kama wapo, au ndugu yako yoyote mkuu mwenye uhitaji walau wafurahie pasaka

Kama una ndugu kijijini mpe priority aisee Kule maisha ni magumu! Aisee kipindi Cha mvua nilifanya kilimo nikawa nimeweka nyapara asimamie kazi zangu aisee Kule maisha ni magumu, ukipewa kazi ya buku Tano lazima jasho litoke mpaka kwenye Tako, nikajifunza kitu, huku mjini tunajifanya wa kishua kutoa favours kwa wadada izi 50 50 wakati Tuna ndugu wengi kijijini wanataabika


Naamini hukosi ndugu kijijini ambae ukimtumia 30k atapata furaha isiyo na kifani na milango ikafunguka!! Ni ushauri tu mkuu maana najua pesa ni za kwako usije nishukia kama mwewe
Wachache sana watakuelewa ila Mimi mtoto wa Mkulima Nimekuelewa
 
Kweli uliishi nao vyema.
Mm nakumbuka kuna jirani yangu nilikua namuita mama mkwe na mumewe baba mkwe Wana watoto watatu wa kike mmoja yupo std7 mwingine yupo std4 na wamwisho yupo std1 basi huyu wa mwisho nilihamia hapo kakiwa kadogo hakawezi kuongea kwahyo kalivyoanza kuongea nikakaambia mimi naitwa baby basi kakazoea jina hilo.
Tuliishi pale mpka kakaanza kusoma kipindi hiko nipo na genge basi asubuhi nakapa hela ya maandazi kanafurahi kweli kakitoka kanakuja gengeni nilipo tunakaa na kucheki cartoons mpka kanalala basi kakanizoea kweli mm nakaita mchumba kenyewe kananiita baby.

Siku nasema nahama alooo kwanza kalikua shule nikatoa vitu vyangu vyote nikawa nimebakiza kuja kukabidhi chumba basi nikaja jioni nikakutana na mwenye nyumba nikakabidhi na kuagana nae sasa mama yake akamwambia baby wako anaondoka dah nilikua na pikipiki kila nikiwasha ndio anaongza kulia ikabidi nikae mpka alale ndipo niondoke ila niliumia sana siku ile. Kuna siku nipo kwenye mizunguko yangu kkoo akaniona weeee aliita kwa nguvu babyyyy babyy mpka nikamsikia watu wanashangaa hawa vipi mtoto na mtu mzima 😂😂😂😂😂😂 alifurahi sana hana la kusema anacheka tu ila sio siri niliishi vyema sana na ile familia ilifika kipindi nikitaka kusafiri nawaachia chumba na mumewe ni boda namuachia pikipiki anapigia kazi. Mpka leo mchumba kakua nikimwambia ulikua unaniita baby anakataa namuonyesha videos na picha anacheka tu. Kuishi na watu vyema kunafungua baraka nyingi.
Uliweka bond nzuri na uyo mtoto ata kuja kukusahau, upendo unaishi.

Kuna kauli napendaga kusema
Mtoto ni malaika moyo wake hauna chuki una upendo tu.

Mazoea lazima yawe na limit dunia ya Sasa imeharibika
 
Kwa hili wimbi la upinde linavyo vuma hata kukaa na kuleta mazoea na watoto wa wengine, mtu unawaza mara mbili mbili na kuhofia maneno ya mtaani..

Maana wanoko hawakawii kusema unawafundisha upinde[emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom