Machozi ya Waziri Byabato na idadi ya watu milioni 64 wanaoongezeka kila kukicha

Steven Joel Ntamusano

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2023
Posts
5,203
Reaction score
3,913
Nimeiona video ya Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato anaonekana akilia mbele ya hadhira ya mkutano mmoja kule Bukoba.

Sauti yake pia inatembea katika mtandao wa WhatsApp akisikika kama analia wakati akidai anahujumiwa ili asiweze kutekeleza ahadi zake za 2020. Muda unaenda kasi na ahadi hazijatimizwa. Wapiga kura wanasubiri siku yao watoe majibu ya haki kwa wagombea.

Idadi ya watanzania wote kwa sasa ni milioni 64 tofauti sana na miaka ile ya 1985 wakati Mwinyi anaipokea nchi kutoka kwa hayati Julius Nyerere tukiwa watanzania milioni 20 na ushee.

Kuna ongezeko la watu milioni 44 ndani ya miaka 38 ya tangu awamu ya pili ianze. Hawa wameshakuwa watu wazima na wanajielewa hivyo uwezo wao wa kuchambua kinachofanywa na serikali ni mkubwa sana.

Uwezo wao wa kutenganisha ahadi na utekelezaji ni wa kisasa zaidi. Wengi wa watu wa kundi hili ndio wanaovaa fulana zenye maandishi ya TUNATAKA KATIBA MPYA, ni kundi la watu wenye kufikiria kisasa na wenye uwezo mkubwa wa kuhoji kinachofanywa na serikali iliyopo madarakani.

Miaka ile ya 1988-90 shirika moja linaitangaza nafasi ya kazi wanakuja waombaji ishirini wenye sifa za kuajiriwa lakini miaka hii ya 2022-23 shirika hilo hilo linatangaza nafasi ya kazi wanakuja waombaji elfu mbili wenye sifa na vigezo vyote vyenye kustahili kupewa kazi.

Watu tumeongezeka sana lakini rasilimali zinaendelea kuwa ni zile zile!, ugomvi mkubwa sana huko mtaani katika kuzigombea hizo rasilimali chache zilizopo. Binafsi naweza kukielewa kilio cha Naibu Waziri Byabato mbele ya wananchi kule Bukoba, kila akitazama anaona mambo bado bila bila na dakika zinazidi kuyoyoma.

Afanye nini ili aweze kueleweka?. Anaishia kutafuta huruma ya wapiga kura kwamba angalau mtoto wao anaweza kueleweka hata kama tatizo linakuwa juu ya uwezo wake katika kulitatua.

Ni nyakati zenye kuhitaji ubunifu mpana kwa upande wa uongozi wa kitaifa sio nyakati za kuja na kauli za jumla jumla zinazojaa dharau kama ile ya RIP Mramba akiwa waziri wa Fedha kwamba hata nyasi tutakula lakini ndege ya Rais ni lazima ije nchini.
 
Nimeiona video ya Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato anaonekana akilia mbele ya hadhira ya mkutano mmoja kule Bukoba...
Kuna ongezeko la watu milioni 44 ndani ya miaka 38 ya tangu awamu ya pili ianze. Hawa wameshakuwa watu wazima na wanajielewa hivyo uwezo wao wa kuchambua kinachofanywa na serikali ni mkubwa sana.[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeiona video ya Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato anaonekana akilia mbele ya hadhira ya mkutano mmoja kule Bukoba...
Kwa sasa watasema ni siasa ila anachosema ni ukweli mtupu. Siasa za bukoba na akina rwangisa na akina kamala haziwezi kumwacha.

Kwanza wanamwona outcast kwa sababu hakuwa katika chama aliteuliwa tu.

Bukoba ukitaka kuleta maendeleo hutoboi. Hili wanalijua kagasheki na Amani. Kagasheki analielewa sana.

Byabato kachelewa kusema hivyo itachukuliwa analilia uchaguzi ujao ila alichosema ni kweli ndio maana ela ya miradi huwa inarudi toka enzi za kagasheki.

Toka waanze kusema wanajenga soko na stand na budget inapitishwa ni toka enzi za jk.

Wahaya tumekuwa watu wa ajabu sana. Wenzetu wanyambo akina bashungwa taratibu wanaigeuzwa karagwe kuwa bomba
 
Nimeiona video ya Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato anaonekana akilia mbele ya hadhira ya mkutano mmoja kule Bukoba.

Sauti yake pia inatembea katika mtandao wa WhatsApp akisikika kama analia wakati akidai anahujumiwa ili asiweze kutekeleza ahadi zake za 2020. Muda unaenda kasi na ahadi hazijatimizwa. Wapiga kura wanasubiri siku yao watoe majibu ya haki kwa wagombea.

Idadi ya watanzania wote kwa sasa ni milioni 64 tofauti sana na miaka ile ya 1985 wakati Mwinyi anaipokea nchi kutoka kwa hayati Julius Nyerere tukiwa watanzania milioni 20 na ushee.

Kuna ongezeko la watu milioni 44 ndani ya miaka 38 ya tangu awamu ya pili ianze. Hawa wameshakuwa watu wazima na wanajielewa hivyo uwezo wao wa kuchambua kinachofanywa na serikali ni mkubwa sana.

Uwezo wao wa kutenganisha ahadi na utekelezaji ni wa kisasa zaidi. Wengi wa watu wa kundi hili ndio wanaovaa fulana zenye maandishi ya TUNATAKA KATIBA MPYA, ni kundi la watu wenye kufikiria kisasa na wenye uwezo mkubwa wa kuhoji kinachofanywa na serikali iliyopo madarakani.

Miaka ile ya 1988-90 shirika moja linaitangaza nafasi ya kazi wanakuja waombaji ishirini wenye sifa za kuajiriwa lakini miaka hii ya 2022-23 shirika hilo hilo linatangaza nafasi ya kazi wanakuja waombaji elfu mbili wenye sifa na vigezo vyote vyenye kustahili kupewa kazi.

Watu tumeongezeka sana lakini rasilimali zinaendelea kuwa ni zile zile!, ugomvi mkubwa sana huko mtaani katika kuzigombea hizo rasilimali chache zilizopo. Binafsi naweza kukielewa kilio cha Naibu Waziri Byabato mbele ya wananchi kule Bukoba, kila akitazama anaona mambo bado bila bila na dakika zinazidi kuyoyoma.

Afanye nini ili aweze kueleweka?. Anaishia kutafuta huruma ya wapiga kura kwamba angalau mtoto wao anaweza kueleweka hata kama tatizo linakuwa juu ya uwezo wake katika kulitatua.

Ni nyakati zenye kuhitaji ubunifu mpana kwa upande wa uongozi wa kitaifa sio nyakati za kuja na kauli za jumla jumla zinazojaa dharau kama ile ya RIP Mramba akiwa waziri wa Fedha kwamba hata nyasi tutakula lakini ndege ya Rais ni lazima ije nchini.
Mambo ni mengi muda mchache.
1. Huyu Byabato mwaka jana alilia machozi.

3. Mwaka huu Nape alimuahidi Tsh 300 Milioni.

4. Nape aliyemuahidi katenguliwa juzi na Samia

5. Na yeye Byabato alikuwa Naibu Waziri katenguliwa pia

Je tutegemee machozi ya damu mwaka 2025??

Samia akihutubia baada ya kuwaondoa kina Makamba na Nape kasema 'sasa uncle zetu wale waliokasirishwa na hizi teuzi tunaomba tu watusamehe' sentensi moja tu inabeba ujumbe mzito.

Kwamba Mzee Makamba Baba mzazi wa January amsamehe Samia kwa kumtumbua mtoto wake. Urafiki hufika mahali ukakosa mashiko kwenye shughuli nyeti za kitaifa.

Huyo Byabato ni kijana mdogo sana kiumri na katika siasa za Tanzania.
 
Binafsi naweza kukielewa kilio cha Naibu Waziri Byabato mbele ya wananchi kule Bukoba, kila akitazama anaona mambo bado bila bila na dakika zinazidi kuyoyoma.

Afanye nini ili aweze kueleweka?. Anaishia kutafuta huruma ya wapiga kura kwamba angalau mtoto wao anaweza kueleweka hata kama tatizo linakuwa juu ya uwezo wake katika kulitatua.

Kilio cha Byabato ni uoga baada ya kugundua kuwa akina Bashiru wamna mpango na jimbo lake.
 
Back
Top Bottom