Nyamtajanyalwa
Member
- Jan 31, 2021
- 15
- 10
Mtoto huyu, aliye katika jamii kwa sasa hajui nani amwamini nani asimwamini,mtoto huyu hana pa kukimbilia, si baba,si mjomba, si kaka, si babu, sio mwalimu, si kiongozi wa dini, sio binamu, mtoto huyu anateseka, mtoto huyu wa tanzania hana pa kushika,hakuna anayemtetea kwa dhati, mtoto wa Tanzania, analawitiwa shuleni, nyumbani, mtaani hadi katika nyumba za ibada, cha kusikitisha hadi watu wake wa karibu ambao anadhani ama anaamini na jamii inaamini wanapaswa kumlinda ndio hao hao wako mstari wa mbele kupoteza kesho yake na kuzima ndoto zake, wanaharakati hawamjali wako bize na mambo yanayowaletea manufaa zaidi kuliko kumsaidia mtoto huyu,mtoto huyu anapaswa kulindwa na watu wenye hekima na hofu ya mungu, mimi kama kijana mdau wa usalama wa watoto napendekeza yafuatayo:
NINI KIFANYIKE KUMLINDA MTOTO HUYU
1. Jamii ipewe elimu madhubuti juu ya ukatili dhidi ya watoto
2. Taasisi husika kama ustawi wa jamii ziongezewe nguvu na sheria ambazo zitawawezesha moja kwa moja kushughulika na ukatili na unyanyasaji wa watoto.
3. Katika nyumba zote za ibada wawepo watu watakao iwakilisha ofisi ya ustawi wa jamii ,wawe chini ya ustawi na wawe na mafunzo stahiki juu ya ukatili dhidi ya watoto.
4. Serikali katika mtaala wa elimu katika ngazi zote watie msisitizo ama waongeze somo litakalofundishwa shuleni na vyuoni kuhusu ukatili wa watoto.
5. Katika kila shule ya binafsi na za serikali wawepo walimu wenye mafunzo stahiki juu ya kusimami ukuaji na usalama wa mtoto dhidi ya ukatili huu wa kijinsia.
6. Viongozi kuanzia ngazi ya mtaa wapewe mafunzo ya uelewa na wapewe uwezo na motisha katika kusimamia ulinzi wa mtoto kuanzia ngazi ya mtaa.
7. Wizara ya elimu iongeze usimamizi na ukaguzi katika vitabu vyote vinavyoingia nchini na kutumika katika kufundishia na kujifunzia watoto.
8. TCRA iwe mstari wa mbele katika kuzuia maudhui yoyote mtandaoni yanayochochea ama kuhamasisha unyanyasaji na ukatili dhidi ya watoto.
9. Katika ofisi zote za umma,kuanzia ngazi ya mtaa,kijiji,kata,tarafa,wilaya hadi mkoa, mashuleni, kuwekwe boksi la maoni ama la kutolea taarifa za ukatili wa watoto na ustawi wa jamii ndio wawe wasimamizi wakishirikiana na polisi.
10. Serikali iongeze kasi ya upatikanaji wa mtandao wa internet ama huduma ya mawasiliano hadi vijijini hii itasaidia katika kupata taarifa za haraka kupitia mitandao ya kijamii au internet zinazohusu ukatili dhidi ya mtoto huyu wa Tanzania.
11. Serikali, jamii na taasisi binafsi ziwaunge mkono watu ama taasisi ambazo ziko msatari wa mbele katika kumlinda mtoto wa Tanzania.
12. Wazazi waelimishwe na waongeze usimamizi dhidi ya watoto wao.
13. Katika vituo vyote vya polisi liwepo dawati maalumu linalohusu mambo ya watoto pekee.
Naweka kalamu chini naamini mtoto wa tanzania anakwenda kuwa salama

Upvote
2