Snipper1698
New Member
- Apr 8, 2016
- 1
- 0
Miaka kadhaa nyuma familia ya Mzee Masega wa kijiji cha Mkata kamba ilipata mtoto mzuri wa kiume mwenye afya njema ya kuridhisha na mwenye tabasamu mwanana. Mama wa mtoto akapewa Heko na hongera nyingi kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki wa familia yake. Baba alipongezwa kwa kupata dume, dume hasa la mbegu imara yenye afya ya kiafrika, jembe la kazi. Wakamuita Kanyanga.
Baba na mama Kanyanga walipambana sana kulea mtoto wao kwa hali na mali kuhakikisha mtoto wao mpendwa anapata mahitaji yake yote ya muhimu ya kiafya na kijamii. Wakilima mazao na kuuza baadhi huku wakijiwekea sehemu ya kipato chao kidogo kwa ajili ya gharama za shule za Kanyanga atakapofika umri wa kuanza shule.
Miaka kadhaa ikapita na Kanyanga akaanza shule katika shule ya kijiji cha Mkata Kamba, akionekana kuwa na akili sana kiasi cha kupendwa na walimu wake Muhura wa kwanza tu baada ya kuanza shule. Akaanza kuongoza wanafunzi wenzake kwenye matokea kwa kuwa wa kwanza kwenye masomo yote. Hali iliyojaza kikombe cha furaha ya familia ya mzee Masega. Hali iliyoongeza upendo kwa mtoto wao huyo wakipata matumaini ya kusaidiwa naye atakapomaliza masomo yake na kupata ajira wakati wao wakiwa wazee.
Kanyanga aliendelea vyema na masomo yake na kuwa kinara wa matokeo ya darasa la saba na kufanikiwa kuchaguliwa shule ya sekondari ya vipaji maalum iliyoitwa Kalunzu iliyopo katika mkoa wa Kanzia.
Familia ya baba yake mzee Masega ikafanya sherehe ndogo ya kumpongeza mtoto wao kwa mafanikio yake. Na mgeni rasmi alikuwa mwenyekiti wa mtaa. Katikati ya sherehe mgeni rasmi alitoa neno lake akasema hongera kijana umeleta heshima kwa kijiji chetu kwa kufaulu vizuri soma uje utusaidie kujenga kijiji chetu.
Sisi kama wanakijiji na wanafamilia tunakupongeza sana. Kanyanga alitoka machozi ya furaha kuona kila mmoja anafurahia mafanikio yake. Mwisho wa sherehe alipewa zawadi mbalimbali kutoka kwa waliohudhuria sherehe.
Safari ya kwenda shule ikaanza mnamo mwezi januari, ambapo baba yake alitumia akiba ambayo aliiweka muda mrefu kwa ajili ya elimu ya mwanaye (Kanyanga). Baada ya miaka minne alifanya mtihani akafaulu vizuri sana akapata daraja la kwanza la pointi 7 akazidi kuishangaza jamii yake kwa ufaulu wake.
Baba akafurahi sana kwa ufaulu mzuri wa mwanaye. Akijipiga kifua akisema asante Mungu nimezaa jembe hasa, muda si mrefu mwanangu atanisaidia nami nitapumzika shida zangu za kufanya kazi ngumu za shamba. Kanyanga akapangiwa kwenda shule ya sekondari ya juu iitwayo Katenzi kwa ajili ya masomo ya kidato cha tano na sita.
Muda ukafika anaripoti shuleni huku akisindikizwa na mama yake mama akamuaga huku machozi yakimtoka, akamwambia mwanangu nakutegemea sana usome kwa bidii yako kama ya awali ufanikiwe ili uje utukomboe na shida za maisha ya kijijini. Nakupenda mwanangu, nakuomba kwa Mungu ufanikiwe baba. Kanyanga aliposikia maneno ya mama yake alijawa na machozi huku akisema mama nakuahidi lazima nifanikiwe , nitapambana mpaka tone la mwisho la damu ili nije kukukomboa wewe na baba. Mama akasema sawa usituangushe. Akaondoka tayari kwa kurudi kijijini kwao.
Mungu si athumani, Kanyanga alianza elimu yake na baada ya miaka miwili akafanya mtihani wa kidato cha sita akafaulu kwa ufaulu wa daraja la kwanza la pointi 3. Hali iliyoongeza furaha kwenye familia yake. Baba yake na mama yake walifurahi sana wakamshukuru Mungu kwa ajili ya mtoto wao. Bahati njema wakati Kanyanga anahitimu elimu yake ya kidato cha sita serikali ilikuwa imeshatangaza huduma ya mikopo ya elimu ya juu kwa wanaojiunga na vyuo vikuu.
Kanyanga akawaambia wazazi wake na mchakato wa kupata mkopo ukaanza, Kutokana na huduma ya intaneti kutokuwepo kijijini kwao ikamlazimu Kanyanga kupanda basi mpaka wilayani ambapo kuna huduma hiyo, huku baba yake akimpa kiasi cha fedha kwa ajili ya maombi hayo.
Mchakato wa maombi ukakamilika na Kanyanga akarudi kijijini kusubiri majibu. Ukafika wakati wa kuomba vyuo Kanyanga akaomba na kupata chuo kikuu cha Kampama ambacho ni miongoni mwa vyuo bora nchini kwao. Kanyanga alifurahi sana, ila ghafla furaha yake ikakatishwa na majina ya waliopata mkopo baada ya kukosekana jina lake, akajisemea moyoni, nimekosea wapi, kwa nini mimi!!
Baba yake akamshika bega na kumwambia, usijali mwanangu chuo utaenda na utasoma, lazima usome mwanangu wewe ndiyo mkombozi wetu, mimi na mama yako tuko tayari kufanya kazi ngumu na kuuza kila kitu ili tu wewe ufanikiwe kwenye maisha yako. Baba yake akauza shamba lake moja aliloachiwa urithi na baba yake.
Kanyanga akapata pesa ya kuanzia chuo huku akisoma kwa kujibana na kwa shida sana, akiamini akimaliza kusoma atapata kazi na kuisaidia familia yake kuondokana na wimbi la maisha magumu na umasikini. Miaka ikasogea baba akiendelea kukopa pesa kwa watu ili kulipa ada ya mtoto wake.
Hatimaye Kanyanga akamaliza chuo na kufaulu vizuri akipata daraja la kwanza. Baba alifurahishwa na matokeo ya mwanaye hali iliyomsahaulisha kwa muda madeni anayodaiwa kutokana na pesa aliyokopa ili mwanaye asome. Maisha baada ya chuo yakaanza ambapo Kanyanga alisaidiana na wazazi wake kufanya kilimo ili kusaidia kulipa madeni waliyokopa wazazi wake.
Habari njema; serikali ikatangaza ajira kwa waliohitimu vyuo mbalimbali, Kanyanga aliona mlango wake wa mafanikio umefunguka kwa haraka sana akamwambia baba yake naye akampatia pesa kidogo kwa ajili ya kutuma maombi. Baada ya miezi kadhaa majina ya waliopata ajira yalitoka na jina la Kanyanga halikuwepo. Huzuni ikatawala akili yake huku akibubujikwa na machozi. Kwa nini mimi!!!
Akijiuliza! Muda ukapita ikatokea nafasi nyingine ya kuomba akaomba tena huku akiamini labda hii ingekuwa bahati yake, nayo alikosa nafasi, huzuni, mawazo, kukata tamaa kukazidi kuzitafuna nguvu zake, akanyong'onyea akiwa haoni matumaini tena ya kupata kazi. Akalia sana, mara mama yake anaingia chumbani na kumkuta mwanaye analia, akamuuliza nini tatizo baba yangu!
Kanyanga akaanza kusema kwa kwikwi, hivi mama kwa nini wengine wanapata kazi mimi kila nikiomba nakosa, kwa nini mimi! Kwa nini mama!! Mama yake akiingiwa na huzuni ajimjibu mwanaye na kumwambia"simama uinuke mwanangu kuna maisha baada ya shule, naumia sana kwa ajili yako napoona ndoto zako na matarajio yako hayajakamilika baba, tulitoa kila kitu kwa ajili yako ili usome mwanangu, jitahidi uwe imara, naumia napoona unalia na kukata tamaa, machozi yako yananiliza.
Kuna haja ya mabadiliko makubwa kufanyika kwenye mfumo wetu wa elimu, ili wataokosa ajira ya moja kwa moja waweze kunufaika na elimu zao. Maana wazazi, ndugu na jamaa wanawekeza sana kwenye elimu za wanafamilia wao ili kufanikisha malengo yao kielimu. Lakini changamoto wanazokutana nazo wasomi baada ya kumaliza elimu zao ndizo hutupa shaka kama ni kweli elimu yetu ina msaada wa moja kwa moja kwenye jamii yetu nje ya kupata ajira. Kuna haja ya serikali kuangalia hili jambo kwa jicho la tatu.

Upvote
0