Mada maalum kwa suala la changamoto ya uzazi kwa mwanamke

Mada maalum kwa suala la changamoto ya uzazi kwa mwanamke

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,866
Reaction score
4,264
Suala la uzazi hasa kwa karne hii imekuwa ni changamoto sana. Idadi kubwa ya wanawake inakumbwa na changamoto.za uzazi kwa wakati na pengine kupelekea utasa.

Lipo jambo moja ambapo umri wa mwanamke unapoonekana kwenda sana na hakuwahi kuzaa, kuna uwezekano mkubwa apate changamoto uzazi pale anapodhamiria kubeba mimba.

Mwanamke anapofikisha miaka 35 kwenda juu hupatwa na changamoto hii kama hakuwahi kabisa kubeba mimba katika ujana wake. Daktari mmoja bingwa aliwahi kusema kuwa kubeba mimba ni afya.

Mayai huanza kuzeeka katika kipindi hiki na kusababisha urutubisho hafifu. Ukichanganya na mifumo ya maisha, nafasi ya kutunga mimba inakuwa adimu sana.

Leo napenda nizungumzie jambo moja ambalo tunaweza kulijadili. Nalo ni MSINGO wa mawazo (stress) pale ambapo mwanamke anagundua kuwa umri umeenda na chances za kuzaa ni hafifu. Hofu huzidi zaidi pale ambapo atajaribu kubeba mimba na ikashindikana.

Sttess ni kitanzi kikibwa sana kwa wanawake wanaohitaji kubeba mimba. Wengi hukataa kuwa nayo hali ambayo huoelekea kuzidisha tatizo.

Natoa rai tutumie fursa hii kuona ni jinsi gani tunawasaidia kinamama kukabiliana na msongo na hatimaye kuweza kufikia malengo yao.
 
Back
Top Bottom