Kwa niaba ya ambao hatuna ndoa bado, naomba niwape pole mnoo wanandoa wenye changamoto!
Ndoa ni ngumu sana ukiwa na mtu asiye sahihi, na ni chungu mnoo ukiwa na mtu ambaye halingani na ubavu wako!
Asilimia kubwa sana ya wanandoa wanishi na watu ambao hawalingani na ubavu wao! Yapo yanayopelekea hayo, kwanza muda mchache wa kujuana, na kingine ni mmoja wao kufake uhalisia wake!
Huwa napenda kufananisha hatua ya kumpata mwenza kama kwenda sokoni na kununua kiatu ambacho utakivaa miaka yako yote ilobaki, sasa wewe jitoe ufahamu ununue bajaji halafu utembelee wakati wa jua na hutakiwi kukivua chini ni miiba, lazima ujute! Wapo watakao nunua rain boot kipindi cha jua ndo maumivu yake watayasikia na hutakiwi kuvua, ndo ushachagua hivyo!
Kwa sie ambao bado, tusiwe na haraka, halafu la mno tumshirikishe Mungu kwa kweeli! Hizi ndoa zinapumulia mashine! Bila sala hatutaweza peke yetu wapendwa!
Mie niwatie moyo tuu, baba ni kichwa cha familia, na mama utailinda ndoa yako kwa maombi! Kila mmoja asimame kwenye nafasi yake kikamilifu naamini mkiamua mnaweza!